Tuesday, November 30, 2010

"MJADALA ULIOVUNJA REKODI KATIKA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO MWEZI SEPTEMBER 2009"

Ndugu wasomaji wa blog hii ya MAISHA NA MAFANIKIO, katika kupitia mada mbalimbali nilizowahi kuweka humu ili kupata ile ambayo ilivuta hisia za wasomaji wengi na kuleta changamoto , nimevutiwa na mada hii ambayo ilileta vuta ni kuvute miongoni mwa wadau wa blog hii.
Kwa hiyo basi nimeichagua mada hii kuwa ndio mada iliyovunja rekodi kwa mwezi september 2010. Natoa shukrani kwa wadau wote mlioshiriki katika kuichangia mada hii.
Naomba muungane nami katika kujikumbusha kile kilichotokea katika mjadala huu.

WANAUME NA KAULI HIZI: 'HUYO SIO WA KUOA, NI WA KUCHEZEA TU'

Bila shaka wewe msomaji unayesoma hapa utakubaliana na mimi kuwa umeshawahi kuzisikia kauli hizi kutoka kwa wanaume pale anapozungumziwa mwanamke mzuri kwa sura na umbo.

Kwa kawaida vipimo vya uzuri wa mwanamke kwa wanaume vimegawanyika. Wanaume wengi hupima uzuri wa mwanamke kwa sura au umbo, lakini linapokuja swala la kuoa, suala la tabia na mwenendo hupewa nafasi kubwa.

Na ndio maana wakati mwingine unaweza kushangaa kukuta mwanaume ambaye ni hodari wa kuchagua wanawake wazuri, lakini ukija kumuona mke aliyemuoa, utakuta ni mbaya kwa sura na umbo, lakini kwa upande mwingine utakuta mke huyo ni mzuri katika maeneo mengine kama vile, tabia nzuri,upendo, wema, na anayemudu malezi ya watoto katika familia.

Sifa nyingine ni zile za kumkubali mwingine kirahisi, kuwa tayari kusaidia yanapojitokeza matatizo katika familia, mpenda amani na kumfanya mume wake aone kuwa hakukosea kumchagua yeye kuwa mke wake. Kwa kifupi wanawake wa aina hii hata kama wangekuwa ni wabaya kwa sura na umbo bado wako kwenye nafasi ya kuonekana kuwa ni wazuri, na huolewa kirahisi zaidi.

Wanawake wazuri kwa sura na umbo ambao tabia na mienendo yao hairidhishi wako kwenye nafasi kubwa ya kuishi bila kuolewa, na kwa bahati mbaya zaidi wanawake wengi wanaohesabika kuwa ni wazuri, tabia na mienendo yao ni ya kutilia mashaka. Wanaume wengi huvutiwa na wanawake hao kujenga uhusiano nao hasa wa kimwili tu na si vinginevyo, na ndio maana wanawake wazuri kwa sura na umbo wanalo soko kubwa sana kwa wanaume, lakini huishia kuchezewa zaidi kuliko kuolewa.

Wanaume nao kwa upande wao wamejenga dhana kwamba wanawake wazuri sana sio wa kuoa na hivyo kuwaogopa. Wanaamini kwamba wanawake wazuri sana ni wasumbufu, kitu ambacho kina ukweli kwa kiasi fulani. Wanaume wanaamini kwamba wanawake wazuri sana kwa sura na umbo huwasababishia waume zao maradhi ya moyo,shinikizo la damu na wakati mwingine hata kuwafanya kupata matatizo fulani ya kiakili, na hiyo inatokana na waume hao kuwa katika mashaka ya wake zao kuchukuliwa na wanaume wengine wakati wowote kutokana na uzuri wao. Hata hivyo wanawake wazuri nao huwaendesha waume zao wakijua kuwa ni wazuri na soko lao liko juu na waume zao nao huwanyenyekea wakihofia kuachwa.

Na ndio maana usishangae kuona kuwa wale wanawake ambao watu wamekuwa wakiamini kuwa ndio wabaya kwa sura au umbo lakini tabia na mienendo yao ni mizuri ndio wanaoolewa na hata ndoa zao zinadumu, tofauti na za wale wanaoonekana kuwa ni wazuri sana kwa sura na umbo na ambao tabia na mienendo yao si mizuri, ndoa zao hazina umri mrefu.

Na maoni yake yalikuwa kama ivyoatavvyo hebu tujikumbushe ndugu zanguni:-

Fadhy Mtanga said...
Mimi niseme nini? Yote umemaliza weye. Maneno mengi ntaharibu utamu. Habari ndo hiyo.
Usichoke.!
Godwin Habib Meghji said...
kwa hili sina uhakika, itabidi nifanye utafiti kwanza ndio nikubaliane na wewe au kukupinga
Candy1 said...
Nobody is perfect sio...au kila mtu ana kasoro, labda wapo wachache ambao wazuri kwa umbo na kitabia vile vile though ni kama kutaka kwenda kuchimba almasi DAR (lol)...true said sister, mwenzio ana hiki wewe huna na ulichonacho wewe mwenzio hana...
Ramson said...
dada yasinta naomba kwanza nikupongeze kwa mada hii nzuri, maana umepiga bakora kwa wanaume na wanawake.

Labda nikuulize swali dada yangu, hebu ninong'oneze, ili watu wengine wasisikie, hivi na wewe unaangukia katika sifa ipi? maana kila nikiangalia picha yako hapo kibarazani, Mashaallah... umejaaliwa kwa sura na umbo..sasa mzee mzima, baba watoto wako hapati Presha kuwa ataporwa siku moja?.....LOL.

Ni hivi mimi nitatoa maoni tofauti kidogo, kusema ukweli kama unazungumzia wanawake wazuri kwa sura na umbo si kwamba tu wanayo matatizo katika ndoa zao bali pia hata huko mashuleni na vyuoni wana kazi kweli kweli...

Takwimu zisizo rasmi zinaonesha kuwa wanawake wenye sura maumbo mazuri kusoma kwao kunakuwa ni kwa kusuasua sana ukilinaganisha na wale wanawake wanaosemwa kuwa wana sura ngumu, yaani sio wazuri kwa sura na umbo, hawa huelekeza nguvu zao zaidi katika masomo na kwa kuwa hawabughuziwi na wanaume wakware wanakuwa huru na hujisomea kwa bidii na mwishowe hufaulu. lakini wanawake warembo kwa sura na umbo muda mwingi wanahangaikia uzuri wao na kuwa bize na wanaume kwa kuwa soko lao liko juu, kila mtu anawataka, na badala ya kutumia muda mwingi kusoma hutumia muda mwingi kuzunguka na wanaume na matokeo yake wote tunayajua...lakini hata hivyo wsiku hizi wamekuwa ni wajanja sana wengi hutumia miili yao kuwahadaa waalimu au maprofesa kwa kuwapa ngono ili wawezeshwe kufaulu katika mitihani na ndio maana likaibuka neno la Digrii za chupi,msichana anaonekana kabisa hana uwezo darasani lakini mwisho wa siku unamuona amefaulu na kusonga mbele. Digrii za chupi siku hizi ziko kila mahali na hata katika ajira zetu mambo ni hayo hayo....wanatumia miili yao kila mahali kuanzia shuleni, katika ajira mpaka kupanda vyeo..na hili madhara yake wote tunayajua.

Naomba nieleweke hapa sisemi kuwa wanawake wote wazuri kwa sura na umbo wana matatizo hayo, nimesema baadhi yao.
kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...
Ramson na uzuri wa Yasinta, heri mimi sijasema, amina

ila sijui kama kuna wanaume wanaomchezea mwanamke. kama ni kuchezea basi wanachezeana. mkwani wakati mwanaume anamchezea mwanamke anakuwa anafanya nini? si anafurahia mchezo tena anadansi kabisa? si mwanamke (hasa wa mujini) anacheza zaidi? iweje asingiziwe mwanaume> acha hizo
viva afrika said...
m speach less, viva blogers, viva MAISHA.
Mwanasosholojia said...
Leo naona dada Yasinta tumeamka na mawazo yanayofanana, umekwenda mbali zaidi, mi nimeishia jirani kidogo kibarazani kwangu, ila maswali yanabaki yale yale na ugumu wake katika kuyatafutia ufumbuzi...masuala ya mahusiano yana utata wake kutokana na utata walionao wanaoingia katika mahusiano! Hongera dadangu kwa mada nzuri
Master said...
"You cannot find a man who is right, you need to make the man right!"
Huwa nawaambia wadada ambao nawakuta wanahaha na waume zao.
Usemi huu unawafanya wasite kidogo, watafakari kwa makini.
Nakosea nini?
Namkosea ama ananikosea?
Nimeshindwa ama tunashindwana?
Atabadilika kweli? Nitambadilisha kweli? Au nibadilike?

Ndoa ni changamoto, inahitaji kila kukicha utunge mkakati mpya kutokana na "actions, which create equal and opposite reactions". Samahani, hiyo ina tafsiri ya Kiswahili kweli?

Ok, kwahiyo hakuna "right man" je, kuna "perfect woman?"
Usemi utakuwaje hapo sasa?

Je, ni kwanini 'uzuri" unasababisha watu wawe tofauti, wajisikie,wabweteke, wawe wenye dharau na madaha, wajithaminishe zaidi?
Nadhani ni kwasababu almasi hutokana na mkaa, lakini hutoka ng'avu zaidi, yenye thamani zaidi.
Hivyo mtu mzuri hujitenga na kujiona wa thamani na pekee zaidi.

Si ajabu tangu utotoni, mtoto anayeelekea kuwa mzuri atasikia "eh, mtoto mzuri huyu jamani!" kisha atapewa zawadi na kubebwa, atakuwa katikati ya macho na mwangaza wa kila mtu.

Tabia zinazoweza kujijenga ni zile za dharau na tamaa. Wazungu wanaita vanity. Tamaa ya kuwa zaidi ya zaidi. Kujisikia binafsi, kutothamini wengine, kukubali yule tu ambaye atatoa au kugawa vitu na vito vya thamani ya urembo alionao!

Si ajabu, mwanamke na hata mwanaume mzuri huharibika haraka. Ni wachache wanaoweza kujizuia kujisikia.

Kuwa na hakika kwamba utampata mwanamke mzuri na mwema pia, ni sawa kweli na kuchimba almasi Dar es salaam!

Lakini jamani, si tunafahamu kwamba hata almasi inabidi isuguliwe kupata mng'ao safi na unaoipa thamani zaidi?!

Hivyo, ukiopoa kizuri, endelea kusugua mwenzangu, futa vumbi kila dakika, sugua na mate ikibidi na hakikisha unajiona kwenye mng'ao!
Usipojiona, wengine watakuja na vichubulio maalumu....
Kissima said...
Du! Mengi yamesemwa,lakini naimani hayajaisha, hata kama nikiyarudia.


Wanawake wazuri kwa umbo na sura wengi wao wanaishia kuwa na watoto ambao kila mmoja anakuwa na baba yake,huishia kutelekezwa na wanawake wa aina hii ni vigumu sana kuolewa.Kwa hili, ninamifano hai kabisa ya kina dada wa aina hii na maswahibu yanayowakumba, yani ukiwakuta barabarani huwezi tambua kuwa wameshazaa na kuzaa,watoto wanaachwa kwa bibi zao na babu zao, wao wanapeta mtaani.
Shabani Kaluse said...
Hii mada ya leo dada Yasinta Kaaazi kweli kweli.....
naona walionitangulia wamemaliza kila kitu sina cha kuongeza ila RAMSON, MASTER NA KISIMA.... KAAAAZI KWELI KWELI KWELI.....
Haya mjadala uendelee, naona hapa sijamuona mzee wa changamoto..LOL
chib said...
Nimefurahia maoni ya wadau
Mzee wa Changamoto said...
Beres aliimba akasema "step aside now, another man wants to take over, cause you don't know what you got and now it's time to loose it"
Sina hakika na MAANA ya UZURI, lakini najua kuwa yategemea na upande uliosimama kuangalia uangaliacho. Kwani KUOA na KUCHEZEA vyatofautishwa na nini? MTAZAMO. Unaweza kuchezea unachooa ama kuoa ulichochezea. Kwa hiyo pengine kuoa na kuchezea ni HATUA za KIMTAZAMO anazokuwa nazo mtu na SIO SIFA ANAYOZALIWA NAYO AMA ANAYOAMBATANA NAYO MTU. Anayeonekana kuchezewa hapa, anaweza kuolewa pale na akawa bora kuliko anavyodhaniwa. Kwenye ndoa (poleni ambao hamjazionja) kuna mengi ya kujifunza (kama utakuwa tayari kjifunza) na kama ilivyo kwa kitu chochote kile kihusichacho mtu zaidi ya wewe mwenyewe, kuna kupoteza kitu il uongeze kitu" Na hii yaweza kuwa muda, fikra, upendo, michezo na mengine mengi.
Kwa hiyo asiye tayari kukubaliana na UZURI wa alie mbele yake anaweza kudhani huyo ni wa kuchezea na ni kwa kuwa hajaamua KUPOTEZA FIKRA HIZO ili aweze KUONGEZA FIKRA ZA UZURI WA NDANI ALIONAO ALIYE MBELE YAKE basi atakaa kutotambua thamani ya kilichopo mbele yake.
Hakuna mtu anayeweza kuonesha UZURI WAKE HALISI kwa yule ambaye hana hakika kama ni wake na hakuna anayeweza kutoa kla alichonacho kama hadhani anaweza kuwa salama asipobaki na kitu.
Kwangu kusema kwa "ni wa kuchezea" ni kujidhihirishia kuwa huna uwezo wa kusoma kilicho ndani ya aliye mbele yako.
Na ndoa njema ni ile ambayo Mume na Mke wanajuana mapungufu yao na wanaweza kuwianisha kwa kusaidia wakijua ni wapi pa kumsaidia nani ili awe anavyotaka kuwa. HAKUNA ALIYEKAMILIKA na sote hatuna mapungufu ya aina moja. Kwa maana nyingine ni kuwa ukiwa na mtu , na ukabahatika kukuta wewe ni jasiri katika mapungufu yake na yeye ndiye jasiri katika mapungufu yako hapo utakwa umepata MATCH ambayo itadumu. Lakini kabla hamjajuana hivyo, ni lazima kudhihirishiana na katika "stage" hii ndipo mmoja anapodhani yu-zaidi ya mwingine na kusema huyo hamfai na hawezi kumuoa ama kuolewa naye hivyo ANAMCHEZEA TUUU.
Kama una uhusiano ama unataka kuoa ni lazima ukmbuke kuwa wanasema ndoa inakupa maximuma 80% ya ulichotaraji (kama utawekeza) na nyingine 20% utaziona nje. Suala ni kujitahidi kuchukua hizo 20% kuziweka ndani ya 80%, lakini mara nyingi tunaona watu wanaacha 80% na kukimbilia 20%. Wakitambua hilo, ni KILIO CHA MBWA (MDOMO JUU). Ndio maana mapenzi ya "kimada" huvutia ukiwa na mke na ukimuacha na yeye "anatema".
Ni upungufu wa fikra.
Naacha
PASSION4FASHION.TZ said...
Yasinta hakika leo umeamua kusema,hakika mada ya leo kiboko,haipendelei upande wowote mmm! kama mdau mmoja kasema speechless,sina la kuongeza nitaharibu.
mumyhery said...
kumbe!!!
Yasinta Ngonyani said...
Kwanza nnapenda kusema nimeyapenda sana maoni yenu.Na ninawapendeni wote.
Ni kweli hii mada imekuwa si ya kubagua, nimeandika kwa kuangalia pande zote. Kwani mara nyingi wengi wengi wamekuwa wakisema napendelea upande mmoja.

Nawashukuru wote kwa mchango wenu nami nimezidi kujifunza mengi toka kwenu ambayo sikujua. Ni kweli hakuna hapa duniani aliye sawa kabisa, kila mtu ana kasoro yake.
Ni kweli pia ukiwa na sura nzuru na umbo zuri kazi kwelikweli. lakini mimi sioni kama kuna watu WABAYA na WAZURI. Kama nakumbuka vizuri muimbaji mkongwa dr. Remmy Ongala aliimba kama wewe ni mbaya basi oa mke mbaya na kama wewe ni mzuri basi ou mke mbaya. hapo utakuwa umepunguzi mgogoro wa kusema mimi MZURI na mimi MZURI.

Na mwisho napenda kumjibu kaka Ramson! kwanza asante kwa swali, pili asante kwa sifa uliyonipa, tatu hizo picha zote ni mume wangu ndiye mpigapicha wangu, nne katika ndoa yetu kuna neno liitwalo KUAMIANA. Kuporwa siku moja.....Lol.

karibuni tena na tena !!!!!!
Chacha Wambura said...
Da Yasinta (of course na wadau wengine), hivi yule mwanamziki aloimba ule wimbo ulopigiwa kelele saaaana kuwa 'wanawake wazuriwazuri wameolewa wamebaki manungaembe' alikuwa na maana gani?.

Kwa mujibu wa maada yako wazuri hawaolewi na kwa mujibu wa muziki huo wazuri ndo wanaolewa. Mbona nachanganyikiwa?

Mnijuze wajameni!!!

Tumalize mwezi na maswali haya Je? uliwahi kuzitumia hizi? ama kuziona tu?

Shilingi Mia moja
Na shilingi mia moja tena.
Penye wengi hapaharibiki kitu, ina wezekana ulitumia kwa kutumwa dukani... na labda kuna walioziona tu...!!!! NAWATAKIENI MWISHO WA MWEZI MWEMA:-)

Monday, November 29, 2010

Nyumbani ni nyumbani...


Nadhani wote tumeianza Jumatatu vizuri, binafsi nipo salama na siku yangu imeanza vizuri na ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunilinda na nimeiona siku ya leo.

Sunday, November 28, 2010

LEO NI JUMAPILI YA KWANZA YA MAJILIO/IDAG ÄR FÖRSTA ADVENT!!!!!

Jumapili ya kwanza ya majilio/Först Advent!!!

Nimeipenda sala hii ya kaka Baraka Chibiriti na nimeona ni vizuri kuitumia jumapili hii ya leo.Ukizingatia ni jumapili ya kwanza ya majilio haya hebu tusali kwa pamoja.

Nia yangu naileta kwako Bwana Mungu wangu, nakuomba Bwana unisikie ninalia kwa uchungu. Nakuomba uipokee sala yangu, sikiliza na sauti ya kilio changu. Ninajua Bwana siku zote wewe hupatikani kwenye gasia, ninajua siku zote wewe hupatikani kwenye vurugu.
Bwana nijaie utulivu wa moyo na nipe nguvu nimshinde mwovu shetani, shusha roho wako anipe faraja. Bwana niongoze ili nitimize nia yangu ya kuwa mtumishi wako mwema!

Ee Bwana upo wapi mimi ninakutafuta, nitazame kwa huruma nateseka Mungu wangu...nakuomba uipokee sala yangu na uisikilize sauti ya kilio changu.
Hata kama nipo kama takataka mbele za watu...lakini mbele yako mimi nina thamani kubwa sana siku zote, kwa hili niajua na ninauhakika kwamba wewe pekee ndiwe wenye kunithamini, nakuomba uipokee sala yangu na uisikilize sauti ya kilio changu.
Ee Bwana wangu nijalie nikabili njia zangu, nimshinde huyu mwovu shetani hanifai kabisa. Bwana Mungu wangu wewe ndiwe tegemeo la maisha yangu yote hapa Duniani, nitausifu na kuku tegemea wewe daima siku zote za maisha yangu!

Saturday, November 27, 2010

UJUMBE WA JUMAMOSI YA LEO!!Halafu angalia/sikiliza na hii hapa kaaazi kwelikweli

Friday, November 26, 2010

Je umewahi kuona Maajabu haya hapa ni Njombe: Mwamba Wenye Ramani ya Afrika

Mwamba huu wenye ramani ya bara la Afrika unaitwa Lwivala, upo katika pori la hifadhi ya msitu Lwivala kijiji cha Igodivaha Wilaya ya Njombe, inaweza isiwe rahisi kuamini lakini huo ndio ukweli wenyewe. Picha kutoka Mjengwa.

Ijumaa njema!! UHURU, hivi ni lini mtu anakuwa huru???Wimbo huu kila nikiusikiliza napatwa na furaha lakini pia napatwa na huzuni kiasi kwamba natokwa na machozi. Sijui wenzangu pia mnajisikia hivyoo:-( HATA HIVYO NAWATAKIENI MWISHO WA JUMA MWEMA !!!!!!!

Thursday, November 25, 2010

UTAFITI: KUNYONYESHA HUZUIA KANSA YA MATITI KWA ASILIMIA 25-60

Tusiacha kunyonyesha vichanga wetu jamani
Mara nyingi nimekuwa najiuliza hivi kwa nini akina mama hapa hawapendi kunyonyesha watoto wao. Utakuta mtoto ana miezi mitatu amekwisha achishwa kunyonya. Anapewa hii mipira (kidanganyio) kutwa nzima kisa eti akima mama wanaogopa matiti yao yatakuwa kama chapati....kwa mimi wala sielewi kabisa . Ebu soma hii makala hapa chini.......
Ambayo nimeipata kutoka kwa kaka Matondo nikaona si mbaya kama tukijikumbusha na pengine kuna waliokosa kuisoma.
----------------------------------------------------------------------------------------------
Mbali na ukweli kwamba kunyonyesha ndiyo chanzo cha lishe bora kabisa kwa mtoto, wanasayansi sasa wanadai kwamba kunyonyesha pia kunaweza kupunguza uwezekano wa mama kupata kansa ya matiti kwa asilimia 25 hadi 60.

Hizi ni habari njema kwa akina mama wa Afrika ambao kimsingi huchukulia kunyonyesha kama mojawapo ya wajibu wao baada ya kupata mtoto. Pengine hii inaweza kuwa ndiyo sababu iliyofanya saratani ya matiti isijidhihirishe sana Afrika.

Wasiwasi wangu ni juu ya kizazi kipya ambacho kinaiga mambo ya Kimagharibi kwa pupa. Nimeshasikia kwamba mabinti wengi sasa hawana hamu tena ya kunyonyesha vichanga vyao wakichelea kuharibu matiti na miili yao. Ukijumlisha na vitu vingine vinavyoingia Afrika vikiwemo vyakula vilivyolimwa "kisayansi", madawa na mabadiliko mazima ya mfumo wetu wa maisha, sitashangaa kama kansa itafumuka na kuwa ugonjwa wa kawaida tu muda si mrefu ujao. Hili likitokea, atakayefaidika bila shaka ni makampuni ya madawa ya nchi za Kimagharibi - na naamini kwamba hiki ndicho wanachotaka. Tuweni waangalifu na tuache mambo ya kuiga vitu kiholela bila kuelewa hasa kiini chake.
Ukitaka kusoma zaidi gonga hapa.

Tuesday, November 23, 2010

Ni muhimu kufanya mazoezi !!!!

Ni muhimu kufanya mazoezi, ni kwamba unauweka mwili wako safi na pia unaepuka ma magonjwa madogo madogo.Bibi anasema, usidhani wewe tu unaweza , hata mimi naweza usidhani umri ni kitu ha ha ha ha:-)!!!! Mmmmmhhh!! nawaza kwa sauti hivi huyu bibi ana mifupa kweli?
Monday, November 22, 2010

MAONI YA MTAKATIFU SIMON KITURURU KUTOKA KWENYE MADA/PICHA YENYE KICHWA CHA HABARI:- NIMEUPENDA UBUNIFU HUU!!

Ya nini kupoteza pesa kuwanunulia watoto vifaa vya kuchezea wakati inawezekana kutengeneza. Yaani hapo vitu vunavyohitajika ni dungu baada ya mafita ya kula kwisha, mwanzi, ndala zilichoka kwa ajili ya matairi bila kusahau ufundi. Haya basi kimbia gari halimgoji mtu Erik ndiye dereva ...tena bei nafuu kabisssssaaaaaaaaaaaaaaa-
natafuta kitoweo kwa manati:-)
Nimeyapenda maoni haya ambayo yanasemaukweki wa sasa na ule wa zamani. nakumbuka wakati nilipokuwa mdodo/kabinti nilikuwa nabeba kigunzi au kile kilixhokuwa kwenye mkungu wa ndizi kama mtoto. Zamani tulikuwa hatununuliwo vitu kama sasa. Ukitaka kujikumbusha ni picha gani basi bonyeza ubunifu. Ahsante sana Mt. Simon Kituiruru- Na hivi ndivyo alivyoanza mt. Simon:-

Si utani! Ubunifu ni muhimu!

Tatizo kiitwacho maendeleo kinafunda watu wengi tu kuwa ujanja ni kununua na ununuacho ghali zaidi ndio ushahidi wewe mjanja zaidi au tu Bab KUBWA kuliko ukiwa unatatua mambo mwenyewe kiubunifu wako mwenyewe.

Kwa mfano siku hizi BONGO(mijini) unakuta hata manati watoto wanataka wanunuliwe.

Ukilinganisha na enzi zetu ukipenda kuchezea magari unajitengenezea kwa waya au hata makopo na ikibidi unaiba ndala nyumbani ukachonge matairi ikiwa ni kutatua tu tatizo la kutaka kucheza gari kibunifu ambalo unajua Mzazi anaweza asikununulie.

Tunako kwenda sijui nini kitatokea kama ubunifu ni jinsi ya kununua na wapi pa kununua wakati mengi tu unaweza kubunia na kutatua mwenyewe.

Fikiria hata chakula kwenye menu za bongo ubunifu ni hafifu sana. Ni yale yale CHIPSI mayai, ugali kwa maharage na kadhalika... wakati kibano kilitakiwa kitengeneze ubunifu kama kibano cha uhaba wa chakula kilivyowaletea ubunifu wa PIZZA kwa Waitaliano masikini.


Nawaza tu kwa sauti!

Sunday, November 21, 2010

Heri ya siku ya kuzaliwa Watoto Audrey na Christian !!!

Watoto hawa ni mapacha ni watoto wa rafiki/mlongo yangu/wangu dada Anastacia Felbo. Wao wanaishi nchini Danmark Leo hii wanatimiza miaka miwili mapacha hawa, napenda kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awalinde wawe na afya njema pia. Pia nawatakieni kila jema katika makuzi yenu. Na halafu napenda kuwaombea wazazi/walezi wenu wawe na nguvu daima ya kuwatunza na nyinyi pia muwe wasikivu/watiifu pia. HONGERA SANA KWA SIKU YENU YA KUZALIWA Audrej na Christian(VANA VANGU)!!!!!! na jumapili njema pia wandugu:-)

Saturday, November 20, 2010

MUWE NA JUMAMOSI NJEMA NA WIMBO HUU!!!Wimbo huu nimeupenda ni mdogo wangu ndiye aliye niambia kuwa kuna kawimbo kazuri na nilipokasikiliaza nikavutiwa nako sana. Natamani kuwa na wewe.... Jumamosi njema wajameni!!!!

Friday, November 19, 2010

NIMEUPENDA UBINIFU HUU!!!!

Hakika usingoja kila kitu kununua tu angalia hapa mama ametumia akili zake pia busara na kupata chupa ya mtoto(chuchu) Kujitegemee ni vizuri......Ijumaa njema jamani!!!!

Thursday, November 18, 2010

BADILIKA, JIONDOE AU KUBALI ILI UISHI.

Huwezi kupingana na hali halisi

Yapo makosa matatu ambayo mtu huwezi kuyafanya bila kujua athari zake. Makosa hayo ni kulaumu, kuunga mkono na kulalamika. Makosa ambayo mtu anaweza kuyaepuka kwa kuona ukweli kwamba ni yeye anayewajibika kwa nafasi yake.

Lipo swali moja kubwa ambalo watu huuliza, nalo ni: ‘Ni vipi nitadhibiti kile kinachonitokea ama kile watu wengine wanachoweza kusema ama kufanya?’ Jibu ni wazi, nalo ni kwamba huwezi kudhibiti kile kinachokutokea.

Kitu pekee uwezacho kudhibiti ni jinsi unavyokabiliana na hali iliyopo mbele yako. Wapo wanaopenda kukabiliana na matatizo yao kwa kulaumu watu wengine ama kujaribu kuunga mkono na kutetea kile ambacho wao walifanya kabla ya hali hii kutokea, ama kulalamika kuhusu hali hiyo.

Uamuzi wa kubadili, kuacha ama kukubali hali iliyopo ndilo jibu sahihi la makosa matatu ambayo watu hufanya.

Ni wazi, chaguo hili linatakiwa kufanyika tu wakati unapokuwa kwenye hali usiyoipenda. Unawezaje kuamua kuachana ama kubadili hali ambayo kwako wewe imezoeleka? Watu wengi wanafanya hivyo na mara nyingi bila kujua. Wakati unapojikuta kwenye hali usiyoipenda, fikiria mambo haya matatu kabla ya kuanza kulaumu, kushutumu ama kujilazimisha kukubali:

BADILI: Unapojikuta kwenye hali usiyoipenda, unaweza kufanya jitihada za kuibadili au kubadili mtazamo wako kuhusu hali hiyo . Ikiwa uko katika uhusiano unaodhani haukusaidii kwa mfano, unaweza kwenda kwa washauri nasaha, unaweza kuzungumza na mwenzi wako na kujaribu kuufanya uhusiano huo uwe bora zaidi ama waweza kubadili mtazamo wako wa namna uhusiano wenye faida unavyotakiwa kuwa.

Mara nyingi huu ni uchaguzi mgumu sana kuufanya kwa sababu inaweza ikalazimu kumkabili mtu mwingine kutoka katika tabia isiyo na faida kwako. Kubadilika kunatuondoa kwenye nafasi yetu tuliyoizoea na ambayo tunaiona inatufariji na kunahitaji ujasiri mkubwa kufanya hivyo.

Kuamua kuacha kumtegemea mpenzi kukupa furaha na kutafuta furaha kutoka vyanzo vyenye kuaminika zaidi siyo jambo rahisi, lakini ni muhimu.

JIONDOE: Kama umeshindwa kubadili hali kwa sababu yoyote ile umeshindwa kumfanya mtu abadili tabia yake kwa mfano,ni bora kujiondoa, ondoka kabisa.
Kujiondoa kunakufanya uondokane na hali isiyofurahisha na kunasafisha njia kwako kwa ajili ya kuchagua jambo jingine mbadala.

Ni wazi,watu wengi hukimbilia kuchagua njia hii, hukimbilia kujiondoa kwa sababu huogopa sana kujaribu njia ya kwanza ya kubadili hali ama kubadilika wao wenyewe.

Lakini ingawa kukimbilia hatua hii bila kujaribu ya kwanza si busara, kuna wakati ambapo kujiondoa ni hatua pekee ifaayo kuchukua. Hata hii nayo inahitaji ujasiri mkubwa kwa sababu, mara nyingi akili zetu hutuweka katika nafasi ya kutumia methali ya ‘Zimwi likujualo’ kama utetezi wa kuendelea kuvumilia madhila yasiyo muhimu tunayokumbana nayo.

KUBALI: hatua ya mwisho unayoweza kuchukua kukubali. Ziko hali ambazo huwezi kuzibadili na kukwepa ukweli wa jambo hilo, ni sawa na wendawazimu. Hebu mfikirie mfungwa wa kisiasa kama ilivyokuwa kwa mzee Nelson Mandela wa Afrika Kusini na wenzake.

Wakati alipokuwa akishikiliwa jela, asingeweza kuibadili hali ile, wala asingeweza kuamua kuondoka. Hakuna jingine aliloweza kufanya ila kukubali hali halisi na kufanya kila analoweza kuishi katika hali hiyo.

Kuna wakati kukubali linakuwa ni chaguo la kwanza tunalopaswa kuelekeza macho yetu, wakati tukiwa tunafikiria njia bora ya kubadili hali au kujiondoa.

Nina hakika kila mtu anapotazama mambo yanayozunguka maisha yake, atakutana na moja ambalo haridhishwi nalo kwa asilimia 100. Utafanya nini kushughulikia hilo, utajaribu kubadili hali au mtazamo wako wa hali? Uko tayari kujiondoa ikiwa una hakika huwezi kubadili hali au uko tayari kubadili mtazamo wako kuhusu jambo hilo ili uweze kuendelea nalo? Uko tayari kukubali kile ambacho huna uwezo wa kukibadili na wala huwezi kujiondoa?

Nafasi ni yako kutumia busara zako kuchagua.

Kumbuka, maisha unayoishi ni chaguo lako mwenyewe, ingawa ni vigumu kuliona na kukubali jambo hilo.
Makala hii nimeitoa kwa kaka Shabani kaluse. nimeipenda na nimeona si vibaya kama tukirudia tena si mnakumbuka au mnajua kuridia kitu ndo kujifunza zaidi.

Wednesday, November 17, 2010

Mwanamtindo wa wiki hii!!!!

Kuna watu watundu, napenda kumshukuru dada Mumyhery ndiye aliyeitengeneza picha hii nami nimeipenda sana na nimeona iwe picha/mwanamtindo wa wiki hii.

Tuesday, November 16, 2010

TUKUMBUKE KUTAMKA HAYA,

Sijui kuna wangapi huwa wanasema haya maneno mara kwa mara kwa mara. Kama kawaida yangu Kapulya mdadisi leo nimedadidi kitu kwa msomaji wa Maisha na mafanikio na mnimepata jibu na nimeona ni vema niwape elimu hii na wenzangu. Haya endelea hapa chini.

Ukiona jambo zuri watakiwa kusema “mashaallah”, yaani mapenzi ya mungu yatimizwe.
Ukiahidiwa jambo unatakiwa kusema “Inshaallah”, yaani litawezekana kwa utashi wa mungu.
Ukihisi maumivu unatakiwa kusema “laailaha illa allah” hakuna mwingine ila ni wewe mungu wangu.
Ukiahidi jambo unasema “bi idhinillah” kwa idhini ya mungu
Ukipata neema unasema “alhamdu lillah” yaani nakushukuru ewe mungu wangu
Ukikasirika unasema “ Audhubillah” yaani mungu niepushe
Ukistaajabu unasema “subhanallah’’ ewe mungu ndiye mpangaji wa yote.
Ukitendewa wema unasema “jazakallah” yaani mungu akuongezee.

Angalia fahari ya Tanzania hii ni Ngorongoro!!!!

Chui angalia jinsi anavyopendeza
Simba, jamani nisaidieni kuna aduiiiii

Ah! ngoja nipumzike kidogo Kifaru anasema!!!
Picha hizi nimetumiwa na msomaji wa blog ya Maisha na Mafanikia ambaye pia ni mdogo wangu wa hiari raha heeee!!!!Naipenda sana nchi yangu na ufahari tulionao.

Monday, November 15, 2010

CHEMSHA BONGO YA JUMATATU YA LEO!!!

Katika kijiji kimoja kulitokea kuwa na penya wengi sana. Na wanakijiji wakaona wampe paka mmoja na rafiki zake kazi ya kuua wale panya. Baada ya mwaka mmoja paka waote walikuwa wameua idadi ya panya sawa, jumla walikuwa wameua panya 1111111, na kila mmoja paka aliua zaidi ya idadi ya panya zaidi kuliko idadi ya paka walikuwa. Je? Ni paka wangapi walikuja kijijini?

Friday, November 12, 2010

UJUMBE WA IJUMAA HII!!!!

je huu ni upendo wa kweli?
There was a blind girl who hated herself because she was blind.
She hated everyone, except her loving boyfriend. He was always there for her.
She told her boyfriend, 'If I could only see the world, I will marry you.'

One day, someone donated a pair of eyes to her. When the bandages came off, she was able to see everything, including her boyfriend.

He asked her,'Now that you can see the world, will you marry me?'
The girl looked at her boyfriend and saw that he was blind. The sight of his closed eyelids shocked her. She hadn't expected that. The thought of looking at them the rest of her life led her to refuse to marry him.

Her boyfriend left her in tears and days later wrote a note to her saying: 'Take good care of your eyes, my dear, for before they were yours, they were mine.'

This is how the human brain often works when our status changes.
Only a very few remember what life was like before, and who was always by their side in the most painful situations.

Life Is a Gift

Today before you say an unkind word -
Think of someone who can't speak.

Before you complain about the taste of your food - Think of someone who has nothing to eat.

Before you complain about your husband or wife - Think of someone who's crying out to GOD for a companion.

Today before you complain about life -
Think of someone who went too early to heaven.

Before you complain about your children -
Think of someone who desires children but they're barren.

Before you argue about your dirty house someone didn't clean or sweep -
Think of the people who are living in the streets.

Before whining about the distance you drive
Think of someone who walks the same distance with their feet.

And when you are tired and complain about your job -
Think of the unemployed, the disabled, and those who wish they had your job.

But before you think of pointing the finger or condemning another -
Remember that not one of us is without sin and we all answer to one MAKER.

And when depressing thoughts seem to get you down -
Put a smile on your face and thank GOD you're alive and still around.
God Bless You.
Habari hii kanitumia mdao mmoja. Nami kama kawaida yangu sipendi kuwanyima ndugu zanguni.
Napenda kuwatakieni wote mwisho mwema wa wiki huku mkitafakari ujumbe huu!!! Ijumaa njema jamani:-)

Thursday, November 11, 2010

Jamani huu kweli ni Uungwana?/ BOT tunaomba mkopo kujenga hii shule Tafadhali,

Hekalu Takatifu la kifisadi, wakati wadogo zetu huko Kigoma na kwingineko wanasoma kwenyevumbi
wakitafuta Kifua Kikuu na magonjwa mengine. Hii ni nyumba ya watu wawili,

Hekalu la Gavana wa BOT......why all these greediness?

Billioni moja nyumba ya Gavana wa Banki Kuu, wadogo zetu wanasoma kwa kudra, mvua ikinyesha shule inafungwa. Kweli jamani tutafika?


Kama tunaweza kutumia Billioni moja kujenga nyumba ya gavana wakati magavana wa baadaye ndo hawa wanasoma kwenye darasa kama hili, nini hatima ya nchi yetu. tunaipeleka wapi nchi yetu jamani. Nawaomba mniambie kama gavana angeishi kwenye apt halafu tukajenga hii shule hata kwa makuti, Mungu si angetuongezea hata mibaraka jamani.

Picha na habari nzima nimeizipata hapa. baada ya kuziangalia roho imeniuma sana na nikaona si vibaya nikiziweka hapa Maisha na Mafanikio hata kama tumesiona lakini kurudia kuziona kunaleta mafundisho zaidi.

Wednesday, November 10, 2010

Brrrrrrr! Msimu wa baridi umeanza/theluji imeanza kuanguka tangu jana jioni na inaendelea!!!

Sasa kimeanza kipindi kile cha baridi theruji imeanza kuanguka tangu jana jioni hapa ni leo asubuhi saa moja na nusu hivi. Yaani hapa kaazi kwelikweli natamani ningekuwa napigiwa na jua....
Na hapa babu Erik anajiandaa kwa kwenda shule na baiskeli yake. Ni saa mbili kasorobo asubuhi hii.

Hapa saa tatu asubuhi. Mmmm baridi we acha tu.


Na hapa mzee wa nyumba naye anaaga ni saa tatu na nusu kuelekea anakowajibika.Tuesday, November 9, 2010

Dangerous - Must read..!!!

Habari hii nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio ebu soma na labda inaweza ikakupa mawili matatu. Sitaki kuwa mchoyo wa elimu:-) Picha hapo juu sio yenyewe ila nimeweka tu kama mfano.

A couple lost their 25 year old son, Arun Gopal Ratnam, in a fire at home on June 4th. The son who had graduated with MBA from the University of Wisconsin-Madison two weeks earlier had come home for a while. He had lunch with his dad at home and decided to go back to to clean up his hostel room.His father told him to wait, to meet his mother, before he went back for a few days. Arun decided to take a nap while waiting for his mom to come back home from work.

Some time later their neighbors called 911 when they saw black smoke coming out of the house.Unfortunately, 25 years old Arun died in the three year old house. It took several days of investigation to find out the cause of the fire. It was determined that the fire was caused by the lap top resting on the bed.
When the lap top was on the bed cooling fan did not get the air to cool the computer and that is what caused the fire. He did not even wake up to get out of the bed because he died of breathing in carbon monoxide.

The reason I am writing this to all of you is that I have seen many of us using our lap top while in bed. Let us all decide and make it a practice not to do that. The risk is real. Let us make it a rule not to use the lap top on bed or put the computer on bed with blankets and pillows around.

Please educate as many people as you can.

Monday, November 8, 2010

Nilipotea nyumbani kwa mngoni.

Rafiki yangu mngoni alinielekeza kwake ili siku nikitembelea maeneo yale nimsalimie.maelekezo yenyewe sasa,pali pali kumpitimbi nyumbi hii bombi hii utikuti jogoo mweupi anikunywi maji basi ndio umifiki(palepale mpitimbi nyumba hii bomba hili utakuta jagoo mweupe anakunywa maji basi ndio umefika).Siku nilipotembelea maeneo yale nikakuta jogoo amechinjwa na mimi nikapotea njia.
Nimeipenda habari hii kuhusu wangoni nimeipata Jamii Forum na nikaona si vibaya kuiweka hapa Maisha na Mafanikio. Kwani Kapulya ni mgoni pia.

Sunday, November 7, 2010

Ahsante Mungu!!

Ni wiki moja sasa imepita tangu uchaguzi ufanyike Tanzania yetu pia Zanzibar.
Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuufanya uchaguzi kuwa wa amani pia utulivu. Kwani katika uchaguzi kunaweza kutokea mengi.


Saturday, November 6, 2010

JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE!!! AMKA AFRIKA!!NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAMOSI NJEMA NA PIA MWISHO WA JUMA MWEMA KWA WOTE NA PIA WOTE MNAPENDWA!!!!!

Friday, November 5, 2010

DUKA LA MTANDAO

Habari njema kwa Ndugu zangu Watanzania mnaoishi nje ya Tanzania, Tumefungua Duka la Mtandao(Onlineshop) la kuuza Chai na Kahawa ya Tanzania tuu. linaitwa Chai & kahawa Online Shop(www.chaikahawa.com) na liko Stockholm, Sweden.tunaweza kuuza na kusambaza chai na kahawa kwa mteja yeyote aliyopo nchi yeyote duniani. wote mnakaribishwa Kununua na kujivunia bidhaa zetu.

Kwa Mawasiliano,Maoni,Ununuzi wasiliana nasi kwa kutumia email info@chaikahawa.com au piga simu,tuma ujumbe mfupi(sms) + 46762878341.

NB:website iko kwenye Flash, kama utapata tabu kuifungua download flash adobe

Thursday, November 4, 2010

WIMBO HUU NI KWAKO DA´MIJA!!!!

Da´Mija

Najua utajiuliza kwa nini da´Mija aimbiwe wimbo lakini yeye nadhani anajua:-
Haya Mija tuimbe pamoja:-)
Shilingi ya Nyerere katikati kuna mwenge x2
Aah doilidoli aah doli Somora eeeh x2-
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Haya hapa nimekumbuka nyimbo nyingine za utotoni:-
Twendeni tukawinde vipepeo x2
Aiya mama vipepeo vipepeo x2
Askari eeh vitani eeh x2
Kiongozi :- Wanabeba
Wote:- Wanabeba bunduki, bisi kibuyu cha maji vitani eeh x2

Kiongozi: Tumefika
Wengine: Bado. Mkifika mnakoenda mnaitikia tumefika

Kiongozi :-Nyama x2
Wengine:- wanaitikia nyama
Kiongozi anasema:- ya mbuzi,
wengine mnaitikia:- Nyama .....unaendelea hivyo kutaja wanyama woteeee. Wimbo huu ni mzuri naupenda kwani sio wimbo tu, pia unafundisha watoto kujua majina ya wanyama kwa urahisi.
Jamani mwenzenu nimekumbuka kweli zamani/utoto. Nawaombeni wote endelezeni hizi nyimbo kwa vizazi vyetu. Binafsi nawaimbia wanangu hasa wimbo huu TUMEFIKA, BADO ni pale watoto wanaonapo uvivu kufanya kitu fulani kwa mfano kwenda kulala au kupiga mswaki, basi tunaimba huu wimbo tunajipanga mstari huku tumeshikana mikono mabegeni na vichwa tumeinamisha chini isipokuwa yule wa kwanza atakuwa kiongozi na safari inaanza ........ujanja eeh!! Kama kuna anayejua nyimbo nyingine za utotoni karibu kutushirikisha na pia unaweza kugonga hapa kwa kupata nyimbo nyingine hasa za mchakammchaka wakati ule mwaka 1947:-)

Tuesday, November 2, 2010

Fikirisho la jumanne hii(Kapulya mdadisi)

Nipo katika Fikra hapa

Leo nimeamka huku nikiwa na fikra kama hizi ni hivi :- Je? umewahi kufikiria kwanini watu hatuli chakula aina moja tu kila siku?
Au kwanini hatuvai nguo moja tu kila siku?
Na halafu kwa nini tuwe/tuitwe (na) jina moja tu wakati wote? kwa nini tusibadili majina yetu pia kila siku?
Baada ya kuwaza hivi sikutaka kuwaza tu, au kuwaza peke yangu nimeamua kuwashirikisha nanyi ndugu zangu/ wasomaji wa Maisha na Mafanikio. Haya tufikiri/Tutafakari kwa pamoja.......

Monday, November 1, 2010

HUU NDIO WEMA!

Jirani kala nini?

Huu ndio wema! Unapotenda wema usitegemee fadhila. Unapokuwa na marafiki, ndugu, na jamaa wa karibu, watendee wema bila kudhamiria kupata fadhila kutoka kwao. Ninapoongelea wema na kutoa ninamkumbuka mama Theresa wa Calcutta ambaye kwa umri na maisha yake angelikuwa Bilionea lakini kwa kujitolea kwake alikufa masikini, lakini akiwa ni tajiri wa nafsi. Nina maana alikufa akiwa na ridhiko, kwani kazi aliyotaka kuifanya aliifanya tena kwa kufaulu. Je wewe hufurahii kuwa kama yeye?
Kumbuka amri kuu isemayo “mpende jirani yako kama unavyojipenda” Je unapokula na kusaza huwa unajiuliza kuwa jirani kala nini?

Tafakari……… hii aliandika mdogo wangu wa hiari Koero Mkundi.