Thursday, November 4, 2010

WIMBO HUU NI KWAKO DA´MIJA!!!!

Da´Mija

Najua utajiuliza kwa nini da´Mija aimbiwe wimbo lakini yeye nadhani anajua:-
Haya Mija tuimbe pamoja:-)
Shilingi ya Nyerere katikati kuna mwenge x2
Aah doilidoli aah doli Somora eeeh x2-
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Haya hapa nimekumbuka nyimbo nyingine za utotoni:-
Twendeni tukawinde vipepeo x2
Aiya mama vipepeo vipepeo x2
Askari eeh vitani eeh x2
Kiongozi :- Wanabeba
Wote:- Wanabeba bunduki, bisi kibuyu cha maji vitani eeh x2

Kiongozi: Tumefika
Wengine: Bado. Mkifika mnakoenda mnaitikia tumefika

Kiongozi :-Nyama x2
Wengine:- wanaitikia nyama
Kiongozi anasema:- ya mbuzi,
wengine mnaitikia:- Nyama .....unaendelea hivyo kutaja wanyama woteeee. Wimbo huu ni mzuri naupenda kwani sio wimbo tu, pia unafundisha watoto kujua majina ya wanyama kwa urahisi.
Jamani mwenzenu nimekumbuka kweli zamani/utoto. Nawaombeni wote endelezeni hizi nyimbo kwa vizazi vyetu. Binafsi nawaimbia wanangu hasa wimbo huu TUMEFIKA, BADO ni pale watoto wanaonapo uvivu kufanya kitu fulani kwa mfano kwenda kulala au kupiga mswaki, basi tunaimba huu wimbo tunajipanga mstari huku tumeshikana mikono mabegeni na vichwa tumeinamisha chini isipokuwa yule wa kwanza atakuwa kiongozi na safari inaanza ........ujanja eeh!! Kama kuna anayejua nyimbo nyingine za utotoni karibu kutushirikisha na pia unaweza kugonga hapa kwa kupata nyimbo nyingine hasa za mchakammchaka wakati ule mwaka 1947:-)

8 comments:

Mija Shija Sayi said...

Haaaaaa..!!Nimekupata mwanawane Yasinta, Basi nilimsimulia Da, Nyanzala jinsi ulivyonilingishia kwa doli doli Samora, jamani alicheka mno. Nyanzala ni mmoja wa watu wanaokupenda sana anasema wewe ni mtundu sana..

Bless you Dada Yasinta.

Yasinta Ngonyani said...

Naona umefurahi kweli dadangu Mija. Msalimie Nyanzala...ila kama kawida ningependa kujua Nyanzala ni nani?

Upendo Daima.

emu-three said...

At last dada Yasinta umeonekana, kama sikosei siku nzima ya jana hukuwa hewani!
Nyimbo za utotoni nyingi ni nzuri kwasababu zilikuwa zikiimbwa kwa mantiki fulani!

Mija Shija Sayi said...

Nyanzala ni mdogo wangu, mtafute pale kwangu utamuona.

Pamoja.

Simon Kitururu said...

Mmmh!

chib said...

Kama Simon, Hmhhhh!!!!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kwa nini usiniimbie mimi?

Bennet said...

Sasa hivi watot hamna michezo kabisa wanaishia kwenye video games na kucheza mipira barabarani hizi nyimbo nahisi zinaanza kupotea