Friday, November 19, 2010

NIMEUPENDA UBINIFU HUU!!!!

Hakika usingoja kila kitu kununua tu angalia hapa mama ametumia akili zake pia busara na kupata chupa ya mtoto(chuchu) Kujitegemee ni vizuri......Ijumaa njema jamani!!!!

7 comments:

Simon Kitururu said...

Si utani! Ubunifu muhimu!

Tatizo kiitwacho maendeleo kinafunda watu wengi tu kuwa ujanja ni kununua na ununuacho ghali zaidi ndio ushahidi wewe mjanja zaidi au tu BAb KUBWA kuliko ukiwa unatatua mambo mwenyewe kiubunifu wako mwenyewe.

Kwa mfano siku hizi BONGO(mijini) unakuta hata manati watoto wanataka wanunuliwe.

Ukilinganisha naenzi zetu ukipenda kuchezea magari unajitengenezea kwa waya au hata makopo na ikibidi unaiba ndala nyumbani ukachonge matairi ikiwa ni kutatua tu tatizo la kutaka kucheza gari kibunifu ambalo unajua Mzazi anaweza asikununulie.

Tunako kwenda sijui nini kitatokea kama ubunifu ni jinsi ya kununua na wapi pa kununua wakati mengi tu unaweza kubunia na kutatua mwenyewe.

Fikiria hata chakula kwenye menu za bongo ubunifu hafifu sana. Ni yale yale CHIPSI mayai, ugali kwa maharage na kadhalika... wkati kibano kilitakiwa kitengeneze ubunifu kama kibano cha uhaba wa chakula kilivyowaleta ubunifu wa PIZZA kwa waitaliano masikini.


Nawaza tu kwa sauti!

Anonymous said...

UBINIFU ......

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Mt, umenena hapo kwa kuwa akina siye tunaotumia vitu vya asili tunaonekana waporipori :-(

Anonymous said...

Huu sio "Ubinifu"....naona ndio hasa tulikoanzia, kabla ya kuanza kutumia mipira(sio condoms) au chupa za plastiki na vioo..hii ndio original

Rachel Siwa said...

Nikweri kaka Simon hata sisi wakike tulikuwa tunatengeneza watoto wa udongo,vitambaa na tukitaka wakusuka tunatengeneza watoto wandizi.

Da Yasinta nami mimeupenda.

Anonymous said...

Kwakweli ata mimi nimeupenda saaaaaaaaaaana.

Penina Simon said...

aisee hata mm amenivutia mno, inapendeza