Monday, November 15, 2010

CHEMSHA BONGO YA JUMATATU YA LEO!!!

Katika kijiji kimoja kulitokea kuwa na penya wengi sana. Na wanakijiji wakaona wampe paka mmoja na rafiki zake kazi ya kuua wale panya. Baada ya mwaka mmoja paka waote walikuwa wameua idadi ya panya sawa, jumla walikuwa wameua panya 1111111, na kila mmoja paka aliua zaidi ya idadi ya panya zaidi kuliko idadi ya paka walikuwa. Je? Ni paka wangapi walikuja kijijini?

13 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

ngoja kwanza nkatafute ugimbi! Nitarudi kaa hapo hapo kwani wengine vilaza...bila ugimbi waweza usiambulie jibu hata kwa mkong'oto....lol!

Fita Lutonja said...

nimegwaya ngoja nikumbushie njia ya kukokotoa niliyofundishwa na mwalimu wangu wa shule ya msingi Maguluwangu hapo labda nitafanikiwa kupata jibu

Unknown said...

we dada Yasinta una bahati sana leo sina mawani yangu. Hii hesabu rahisi kama nini!!! Ngoja nitafute mawani yangu, nikiipata narudi hapa!!! LOL!!

Subi Nukta said...

hata mimi siyo kwamba sina majibu, sema tu leo sitaki kujumlisha, teh teh, ila nina swali, hao paka wote umewapataje na unawatunzaje?

Yasinta Ngonyani said...

Ha ha ha haaaaaa! wote mnasema tutarudi mara mnataka ugimbi kwanza na mwingine miwani...mara nikamuulize mwalimu wangu wa shule ya msingi...na wewe Subi eti sitaki kupiga hesabu leo..lol kaazi kwelikweli...

Albert Kissima said...

Majibu nitayaleta taratibu taratibu.
Nianze na sehemu ndogo kabisa ya jibu. Paka haishii tu kuua, hula pia panya waliouliwa.
Nitarejea tena, pole pole ndio mwendo.

Ila mfalme kama anavaa miwani, anaonesha amekula chumvi nyingi, atalijibu kwa uzoefu, amuombe mjukuu wake amsomee swali!!

Mija Shija Sayi said...

Ngoja nikatafute kalikuleta yangu kwanza nami nitarudi..

Penina Simon said...

mh!!

Unknown said...

ToA jibu plz dada

Unknown said...
This comment has been removed by the author.
Unknown said...

Apo umesema kijiji kilikua na penya wengi alafu panya

Unknown said...

Apo umesema kijiji kilikua na penya wengi alafu panya

ukomboz blog said...

admin hata yeye hajui jibu , maana toka 2010 mpaka leo hajatupatia majibu ..... kama anabisha kuwa hajui aje hapa atupatie majibu