Thursday, November 25, 2010

UTAFITI: KUNYONYESHA HUZUIA KANSA YA MATITI KWA ASILIMIA 25-60

Tusiacha kunyonyesha vichanga wetu jamani
Mara nyingi nimekuwa najiuliza hivi kwa nini akina mama hapa hawapendi kunyonyesha watoto wao. Utakuta mtoto ana miezi mitatu amekwisha achishwa kunyonya. Anapewa hii mipira (kidanganyio) kutwa nzima kisa eti akima mama wanaogopa matiti yao yatakuwa kama chapati....kwa mimi wala sielewi kabisa . Ebu soma hii makala hapa chini.......
Ambayo nimeipata kutoka kwa kaka Matondo nikaona si mbaya kama tukijikumbusha na pengine kuna waliokosa kuisoma.
----------------------------------------------------------------------------------------------
Mbali na ukweli kwamba kunyonyesha ndiyo chanzo cha lishe bora kabisa kwa mtoto, wanasayansi sasa wanadai kwamba kunyonyesha pia kunaweza kupunguza uwezekano wa mama kupata kansa ya matiti kwa asilimia 25 hadi 60.

Hizi ni habari njema kwa akina mama wa Afrika ambao kimsingi huchukulia kunyonyesha kama mojawapo ya wajibu wao baada ya kupata mtoto. Pengine hii inaweza kuwa ndiyo sababu iliyofanya saratani ya matiti isijidhihirishe sana Afrika.

Wasiwasi wangu ni juu ya kizazi kipya ambacho kinaiga mambo ya Kimagharibi kwa pupa. Nimeshasikia kwamba mabinti wengi sasa hawana hamu tena ya kunyonyesha vichanga vyao wakichelea kuharibu matiti na miili yao. Ukijumlisha na vitu vingine vinavyoingia Afrika vikiwemo vyakula vilivyolimwa "kisayansi", madawa na mabadiliko mazima ya mfumo wetu wa maisha, sitashangaa kama kansa itafumuka na kuwa ugonjwa wa kawaida tu muda si mrefu ujao. Hili likitokea, atakayefaidika bila shaka ni makampuni ya madawa ya nchi za Kimagharibi - na naamini kwamba hiki ndicho wanachotaka. Tuweni waangalifu na tuache mambo ya kuiga vitu kiholela bila kuelewa hasa kiini chake.
Ukitaka kusoma zaidi gonga hapa.

17 comments:

Upepo Mwanana said...

Da Yasinta acha kuchekesha watu!!
Yaani watotot wakinyonya sana matiti yanakuwa kama chapati???
Ha ha haaaa, hiyo ni imani potofu kabisa. Hao wana sababu nyingine

Koero Mkundi said...

Mie naomba nije na swali kuhusiana na mada hii maana ndio naelekea ukubwani sasa na siku si nyingi nitaitwa mama....LOL. Hivi mtoto anatakiwa kunyonya maziwa ya mama kwa maika mingapi ndio aachishwe ziwa? naomba majibu yawe ya Kisayansi na sio TABOO

chib said...

Yasinta ndo mwenyewe kwa jibu maalum kwa Koero.
Miezi 6 ya mwanzo, kama inawezekana mtoto aishi kwa maziwa ya mama tu, pia anaweza kuendelea kupata maziwa akichanganya na milo mingine hadi miaka 2 kama unampendelea au unampenda au kujalia afya njema ya mtoto! Ila kwa shughuli za kina mama wa kazi, na mijumuiko ya watoto, ratiba hii huonekana ngumu

Israel Saria said...

Kunyonyesha nani? Baba au mtoto?

Koero Mkundi said...

Saria......LOL..... hivi kumbe baba naye huwa ananyonya ziwa la mama? kaaaaazi kweli kweli.....
Lakini mie sidhani kama hiyo ni kweli au wadau wengine mnasemaje?

Duh! sipati picha dume zima kama Ng'wanambiti, Kamala, Markus, Kitururu, Fadhy, au kaka Chib ananing'inia kwenye titi la mama na kunyonya, ha ha ha ha haaaaaaaa...... Saria una mambo weye....

Israel Saria said...

Dada yangu Koero..kuuliza si ujinga ukijifanya unjua kila kitu..utajikuta hujui kitu...kuna mibaba inanyonya na uzee wao...hao uliowataja sina uhakika kama wananyonya..uzilianzishe..mie simo!!

Simon Kitururu said...

@Koero:

Watoto wakubwa a.k.a MADUME RIJALI wananyonya.


Kwani unafikiri wanaume wapenda matiti ya akina DADA mapenzi yao ni ya kuyatumbulia macho tuuu?

Na kuna wadada WENGI TU wapendao kunyonywa NYONYO na wapenzi wao a.k.a WATOTO WAKUBWA , kwa kuwa husaidia kuwaandaa maeneo mengine muhimu kukaa mkao wakupokea shughuli KIUNYEVUNYEVU wa UVUNGU katika TENDO ambalo kwa wafuata dini fulani kama hujaoa au kuolewa eti ni dhambi .:-(

Koero Mkundi said...

Kaka Mfumwa Kitururu.....! Swali la kizushi, Je maziwa ya mama aka Matiti ni mali ya mtoto au ya baba?
Ni nani ana haki zaidi ya kumiliki eneo hilo muhimu la mama?

Amos Msengi said...

Kunyonya sio mwisho wa safari, suala la kujiuliza ni je Mtoto MKUBWA akinyonya humeza au hutapika? Je anyonywae hujisikiaje?
Ni kweli kunyonyesha kunapunguza upatikanaji wa kansa,bila kujali ni mtoto wa umri upi kanyonya.

frozia adinani said...

dada yasinta waambie hao wenzetu wanaoendekeza ujana mimi kama mimi siamini kama kweli matiti yanakua kama malapa hiyo ni wewe mwenyewe unavojiweka mbona mimi nimezaa na ninamtoto wangu na siona kama nimebadilika sana katika kifua changu tena baada ya mwanangu kuacha kunyonya nilikua najisikia vibaya sana kwani niliona kama namnyima haki yake vile mpaka baba ake alipoareange kumtoa mtoto nyumbani kwa muda wa wiki moja ndio nikazoea na baada ya hapo bado naonekana vizuri.
kwakifupi hata usiponyonyesha mtoto muda ukifika lazima yawe malapa kwani unazani utakua kijana siku zote mpaka kufa? tumewaona wangapi ambao hawajabahatika kuzaa na maziwa yao yamelala hebu tuachane na hizo mila potofu kwani hakuna kutu kizuri kama kunyonyesha mtoto wako akakua vizuri na watu wakakusifia mtot wako mzuri kumbe ni ile lishe anayoipata kutoka kwako na ile ya nyongeza kutoka kwenye vitu anavyokula
Have a nice day my sis.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

KOERO: Umechakachua mada hii...tafadhali tutake radhi!

Koero Mkundi said...

Ng'wanambiti wa kulaumiwa ni Saria, ndiye aliyeanza kuchakachua mada, mie ni miongoni mwa wadadisi wa mambo, na ndio maana nilishikwa na tashwishwi ya kutaka kujua mengi.... lakini Mtakatifu naye ndiye kazidisha kuichakachua na kama umjuavyo kwa manenno yake ua hovyo.....LOL

Any way kama nimekukwaza nisameee kaka, maana sikuwepo mtandaoni kwa muda mrefu isije ikawa nimerudi kuondoa utulivu.....LOL

Naomba wachangiaje muendelee kutoa maoni yenu na muachane na upuuzi wangu.....LOL

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

koero ushindwe na ulegee na unyonyeshe li baba ili ujue,

mimi maifaifu amejitahidi mieizi sita kiijana ataishi kwa ziwa tu na baada ya hapo ndo milo mpaka mwaka mmoja hivi

ila mimi sinyonyi, labda likizo

Simon Kitururu said...

@Koero: Maziwa ya mama ni mali ya mama.

Toto na toto kubwa ni uamuzi wa mama kuwagea kinukta mvujo kinunacho kwenye baridi.


Halafu nimestukia unanisakizia nimezidisha uchakachuaji wa mada kwa kuwa wadai eti naongea hovyo.:-(

Yasinta Ngonyani said...

nataka kujibu swali lako Koero kwa vile umesema si muda mrefu utaitwa mama...lol ni kwamba binafsi kama mama nilinyonyesha wanangu kwa muda wa miak miwili miwili. miezi 6 ya kwanza walinyonya tu maziwa ya mama na baadaye nikaanza kuwapa chakula kidogo kidogo. natumaini nimejibu kama ulivyotaka:-)

Israel Saria said...

Mtoto wa kwanza daima ni Baba, naye ndie anayesababisha madhara ya hayo maziwa(matiti)..sio rahisi kuzuia maziwa kutumika kwenye Warm-up ya mahusiano, japo kuna wengine wanayatumia vibaya..just handle with care!!
Au kama kuna wenye mifano tuwekeeni hapa tuone..

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Asante dada Yasinta kwa kuuweka utafiti huu hapa.

Mimi sitaki kuingilia mjadala ambao inaonekana "umechakachuliwa."