Monday, November 8, 2010

Nilipotea nyumbani kwa mngoni.

Rafiki yangu mngoni alinielekeza kwake ili siku nikitembelea maeneo yale nimsalimie.maelekezo yenyewe sasa,pali pali kumpitimbi nyumbi hii bombi hii utikuti jogoo mweupi anikunywi maji basi ndio umifiki(palepale mpitimbi nyumba hii bomba hili utakuta jagoo mweupe anakunywa maji basi ndio umefika).Siku nilipotembelea maeneo yale nikakuta jogoo amechinjwa na mimi nikapotea njia.
Nimeipenda habari hii kuhusu wangoni nimeipata Jamii Forum na nikaona si vibaya kuiweka hapa Maisha na Mafanikio. Kwani Kapulya ni mgoni pia.

6 comments:

Baraka Chibiriti said...

Nikasikia mwungurumu vuuuuuhh...nikazani gari, kumbe Isuzu bwana.

Kazi kweli kweli...!!!!
Isuzu si gari...hao ni ndugu zangu na watani zangu wa jadi. Bombi nyumbi hii!!!

Unknown said...

Hii ya leo kali kweli. Nimecheka mpaka basi!!!

John Mwaipopo said...

hapo usipopotea basi wewe ni malaika. hapa ndipo tulipoanza kuwaita ndugu zetu 'nyumbi-bombi'.

maelekezo haya yanaweza kukufikisha pahala husika endapo utaambiwa muda na umbali katika mita ama kilomita muafaka. pengine sasa saba ndipo jogoo husika hunywa maji.

kazi ipo

Anonymous said...

Thanks dada yangu kwa kupitia angalau kautani kangu maana na mimi ni mpenzi mkubwa wa blog yako big up sis.

Simon Kitururu said...

:-)

emu-three said...

Hahahah....kweli hicho kichekesho!
Lakini mmmmh, Mngoni? inatokana na neno mgoni? Unajua haya maneno wakati mwingine yamefumbwata na kisa fulani, sina uhakika na hilo nawaza tu!
Kuhusu huko kupotea nakumbuka wanasema unaweza ukaruka kitu wanaita `mdudu' hata kama umeelekezwa vipi, utatembea mpaka uchoke dawa yake ni kugeuza shati, najua utaniuliza kama mwanamke kavaa gauni ataligeuzaje na wakati yupo njiani?