Monday, November 30, 2009

NYIMBO ZA MCHAKAMCHAKA/KUMBUKUMBU

Leo nimekumbuka wakati nasoma shule hasa shule ya msingi saa kumi na moja alfajiri kuwahi shule kisa nini? Kuwahi namba na kukimbia mchakamchaka huku mnatweta kama nini na mkiimba nyimbo:- Kwa mfano:-
1. Panda mlima panda, panda, panda, pasnda usichoke........x2
2. Iddi amin akifa mimi siwezi kulia nitamtupa kagera awe chakula cha mamba.x2
3.Jua lille literemke mama, mwezi nao uteremke mama haiyahiyaaa hiyaa hiyaa mamaaaa.....x2
4. Alisema, alisema, alisemaaa Nyerere alisema vijana wangu wote mwalegea shart tuanze mchakamchakax2.....

Kama kun mtu anakumbuka wimbo mwingine basi karibu kuongezea hapa.

22 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hpa ndo huwa nakufaga na hasa nikitembelea vibada (shule) au madarasa tuliyosomea enzi zetu mnakimbia mchaka mchaka harafu darasani mpaka jioni bila kuoga wala nini

Fadhy Mtanga said...

Da Yasinta umenipa raha. Nilikuwa nikipenda mchakamchaka hakuna tena. Leo niwaonapo watoto wa shule wakiwa goigoi husikitika sana. Mchakamchaka ulitufanya kuwa na miili imara na akili zenye kuchemka. Najua kuna watu hawakuupenda ndo maana huwa wanauponda.
Pia nyimbo zake zilikuwa ni zenye kueneza sera fulani.
Umenifurahisha sana leo.

EDWIN NDAKI (EDO) said...

mchaka mchaka ulikuwa safi sana.Kwanza mwanafunzi inamsaidia mwili kuwa katika hali nzuri.

ilikuwa safi sana

Nampangala said...

Hivi kwani siku hizi hakuna mchakamchaka? nimepitwa na habari hizi. Ulikuwa safi sana ni kweli alivyosema Mr Edwin apo juu. kwakweli Mlongo unatukumbusha mbali sana nimejikuta naanza kuimba na kukumbuka ennzi za shule na kale kabaridi ka lilambo ilikuwa inatusaidia kupata kajoto kabla ya kuingia dalasani.

Mzee wa Changamoto said...

Kuna mengi ya kukumbushana enzi zetu za CHANDIMU na michezo ya kiBabaBaba na Kombolela naa.....

Bennet said...

Siku hizi kwa kweli sio mchaka mchaka tu bali hata michezo mingi kama kidali, kibaba baba, mdako, kombolela/butua
Watoto wako busy na video games hawajui hata kutengeneza magari ya makoa au midoli ya kufinyanaga na udongo, mipra ya chandimu na mengineyo, hii ni kwa sababu ya mabadiliko au maendeleo ya nchi

MARKUS MPANGALA said...

Weeeee Nampangala ndiyo nani?????? jieleze kwa jina lako hilo harakaaaaaaa.


Mmmmh dada Lelu unihokonywili kweliiiiiiii, mwenga kotokunihokonyola nahaa wenga, raha weeeee

Mija Shija Sayi said...

1. Bandaa wa Malawi.. katuvalia ngozi ya simba.. kututishia watanzaniaa, hatujali hatujali..

Mchaka-mchaka chinja, alinselema alija...

Unknown said...

Jamani mambo haya.......
kaazi kweli kweli

John Mwaipopo said...

@ yasinta ... umoja wimbo/ uwingi nyimbo.

nilikuwa nasubiri nani ataukumbuka 'mchaka, mchaka chinja, alinselema alija'. nimejua hivi karibuni kuwa wimbo huu wengi tulikuwa tukiukosea. ni wa asili ya kisukuma ndio maana Mija kaupatia. unatokana na mapigo ya waendesha mitumbwi. uwongo? sie tulikuwa tukiimba 'alinselema adija'

mwe!

Anonymous said...

'mchaka, mchaka chinja, alinselema adija'...hapo umeniacha hoi-nakumbuka sana.

Kwakweli warejeshe mchaka mchaka,lakini sio kuleta tena ile dizaini ya kumalizia kila kitu na"kidumu chama cha mapinduzi".

P.s. kuna mwimbo mwingine wavita vya Kagera/ nduli Idd Amin ambao nimeusahau.Ulikua unaanza na "lile,lile lilelee"halafu katika unaingizia kwamba alitaka kuiba Kagera "ambayo ndio mali ya Watanzania"...sijui kuna anayeukumbuka?

Mija Shija Sayi said...

Lile lile lilembeee,...x3 lile lile lile lilembe, ni mshenzi sana Aminii.., kafikiria sana kashindwaa.. kaona achukue Kageraa ambayo ni mali ya watanzaniaa...

*Anony hapo juu wimbo huo, mi inabidi tufanye utaratibu wa kuzirekodi ili historia isipotee, hebu ona tunavyohangaika kuzikumbuka.

John Mwaipopo said...

mija tunakupa shuguli hii rasmi. nina uhakika imetua katika mikono salama.

AGNESS ANDERSON said...

teh teh teh....abana daah! umenikumbusha mbali kweli kweli huku na ufagio mkononi... ha ha ha. ahsante mama,,,,

Faith S Hilary said...

Nyimbo number 3..ilikuwa mara yangu ya kwanza kuchelewa shule na ya mwisho! maana dah...

Mija Shija Sayi said...

Mwaipopo shughuli ipi unayonipa ndugu yangu?

John Mwaipopo said...

"mi inabidi tufanye utaratibu wa kuzirekodi ili historia isipotee"

mija hapo vipi?

Mija Shija Sayi said...

Nilitaka kuandika ... mi naona inabidi tufanye utaratibu wa kuzirekodi, Mwaipopo unaonaje tukamwomba Jide aokoe jahazi?

John Mwaipopo said...

kwani mija mambo ya sanaa siku hizi umeyaweka kando? au wewe kuimba si kihiiiivyo. Lakini nadhani tumifika pahala pazuri. ushauri wa ufundi tutachukua kwako. kuhusu nani aimbe pemgine ni vema tukawamobile watoto fulani hivi (mfano wa vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu) ili sauti hasa siwe za kitoto/watoto. hapa sidhani tutakosa msaada kutoka wizara za elimu, habari na maliasili. au?

Mija Shija Sayi said...

Nimekukubali Mwaipopo. Nitalifuatilia suala hili.

Yasinta Ngonyani said...

Ni furaha ilioje kuna wengi mmefurahia kukumbuka enzi zile na nyimbo za mchaka mchaka. Na nimefurahi kusoma ya kuwa mnataka kufanya mikakati na kuzirekodi hizi nyimbo ili ziwe kumbukumbu zaidi kwa wajukuu wetu. Mie nipo tayari kuziimba..lol. Ahsanteni sana kwa maoni yenu.

Abdon Kanuti said...

Imagine leo ndo nimeona comments. Mchakamchaka ilikuwa raha sana