Wednesday, November 4, 2009

KARIBUNI KANDA YA KUSINI TUCHEZE MGANDA-RUVUMA/SONGEA



Kama unatamani nyumbani fanya kama mimi sikiliza ngoma za asili na ikibidi cheza pia, haya karibu tuungane kwa ngoma hii ya mganda.

6 comments:

Chacha Wambura said...

Ningependa saana kucheza mganda lakini sina nao hamu kwa sababu binafsi nadhani ni ngoma ya wazembe ndo maana wanakuwa smati na hivo kucheza kizembe...lol

Si unajua tena ngoma za kikurya kama mbegete, zeze na ritungu ni ubabe ubabe tu.....lol

wa kunyumba msikasirike lakini, ha!...lol

John Mwaipopo said...

aaah! sie hii tunaiita 'ling'oma'. si unajua tulicopy kwa ndugu zetu hawa mlipokuwa mnashuka kutoka melini pale itungi port? cha ajabu pamoja na juhudi zangu zoote za kutaka kujifunza kucheza ling'oma mpaka leo siwezi. ha! ha! ha!

chib said...

Kucheza ngoma ni fani Kaka Mwaipopo

Anonymous said...

Mlongo, unifikishi kunyumba,
pale Nangombo- mbamba-bay niliwai kuona mganda wa kukata na shoka ukiongozwa na mjomba wangu wenyewe walimuita Maelufi. ni miaka sasa imepita toka nifike uko lakini nikiona ngoma hii si ishi kukumbuka uwo mji. hiyo kanisa la peramio apo nimekaa miaka 4 enzi za shule ni mji mzuri sana kuna kila kitu. asante mlongo kwa kutukushakumbusha

Yasinta Ngonyani said...

Chacha Wambura acha fujo sema tu huwezi stepu zake maana mganda unahitaji stepu za maringo na wewe huna...lol

Mwaipopo nawe, sema hukuwa na nia, ha! ha! ha! ha!.

Kaka Chib hapo umenene, Mwipopo upo wapi njoo usema kitu hapa...lol.

Mlongo wenga yaani namwuyaku nikumbuki kweli kunyumba ndi maana nivikili ngóma hii. Ngati una ngóma yingi unogela nijovelayi. Karibu sana pa luvanja hapa.

John Mwaipopo said...

nimeenda kariakoo kutafuta shati leupe la nailoni (sio kama ya shule au ya ofisini) na kaptula nyeupe pia. upande wa filimbi nitakata mirija ya majani ya mpapai kisha nitafunga nailoni upande mmoha kwa kutumia rubber band. mbona hamniulizi soksi nyeupe za kufika magotini ... Ha! ha! ha!!!