Thursday, November 5, 2009

DAWA YA MAPENZI.......... HADITHI.!!!!!

Palitokea Mwanamke, aliyekuwa ametolewa, akashindwa kuishi vizuri na mumewe. Kwa hivyo mumewe hakuridhika naye akaamua atafute mwanamke atayemfaa zaidi, aishi naye. Kwa wivu, yule mke wa kwanza, akatafuta dawa ya kuweza kumrudisha mume wake. Akatafuta dawa aina nne. Aina ya kwanza, ilikuwa ya kujipaka mwilini, aina ya pili, ya kutilia yule mawanaume kwenye chakula, aina ya tatu, ilikuwa ya kuoganayo, aina ya nne, ilikuwa ya kuchoma kwa moto. Hizo dawa aliamini zitamfanya mume wake, amwache mke wa pili, na kwamba mapenzi yao yataongezeka, kwa hivyo wataishi pamoja tena. Baada ya kuzipata dawa hizo na kuzitumia kikamilifu, bado hali ikawa ile ile, hakuna lililobadilika. Mumewe akaendelea kuishi na mkewe wa pili.

Yule mke wa kwanza, akaenda kwa bibi kizeemmoja ambaye alisifiwa kuwa mganga hodari akamwomba amsaidie. Bibi kizee hakusita akamwambia akatafute ubongo wa Fisi, yaani akamuue Fisi ampasue na kuuleta ubongo ukiwa bado mzima! Ubongo huo, ndio utatumika kutengenezea dawa ya mapenzi.

Mwanamke akarudi nyumbani akaanza kufikiria jinsi atakavyomtega Fisi na kumuua. Akapata wazo la kununua nyama na kuikata vipande, kuviweka njiani ambapo fisi hupendelea kupita mara kwa mara. Kesho yake akakuta ule mtego mtupu, na nyama imeliwa. Akanunua nyama kwa wingi akaiweka toka pale alipotega jana yake njiani pote mpaka nyumbani kwake. Fisi walipofika, kwa uroho na ujinga wao kana tunavyowafahamu, wakaanza jula vile vipande vya nyama mpaka ndani ya nyumba ya yule mwanamke. Akamkuta yule mwanamama amejitayarisha vizuri na shoka. Kwa nguvu zake zote. Akampiga kipigo kimoja tu na yule Fisi akafa hapo hapo. Akampasua kicwani akatoa ubongo, na akaenda nao kwa bibi kizee mganga.

Alipofika, bibi kizee akauliza: “Mwanangu, umeniletea ile dawa niliyokutumia?” Mwanamama akajibu. “Ndiyo mama, lakini nimeipata kwa shida sana!” Akamkabidhi bibi kizee ule ubongo wa Fidi. Alipokwisha upokea akakaa kitako akafikiri sana. Halafu akasema: “Mwanangu, sasa nitakueleza kila kitu vizuri sana umetumie akili na ujuzi mwingi, kutega Fisi na kumwua. Sasa nenda ukatumie akili na ujuzi wako wotw ulionao, ili uweze kupata mapenzi ya mumeo, ili uweze kupata mapenzi ya mumeo tena. Nina maanisha kusema, lazima uwe msafi, uvae vizuri na upikie chakula kizuri mume wako. Vile vile, jaribu kujipendezesha kwa mume wako kwa kila hali. Utaona mumeo anarudi nyumbani na kumuacha mke aliyekuwa naye sasa hivi, na mataishi kwa amani na furaha.

Aliporudi nyumbani, akafanya, yote aliyoambiwa na yule bibi kizee. Haukupita muda, mumewe akamfukuza mke wa pili na akarudi nyumbani kwa mke wake wa kwanza. Wakaishi vyema kwa mika mingi sana mpaka vifo vikawatengenisha.

FUNDISHO:- Inaaminika kuwa, watu wanapoishindwa kuishi pamoja katika ndoa, hutumia dawa za kienyeji kwa sababu ya kusitawisha maisha yao.

Wapo akian mama wengi amabao wanaamini kabisa kwamba kuna dawa ya mapenzi.
Lakini ukweli ni kwamba, dawa ya mapenzi ni moja tu nayo ni: Kuhakikisha kwamba, kina mama wanaheshimu ndoa zao na kutii waume zao. Nyumba yenye mapenzi, inamfanya mume apende kukaa nyumbani, na asitembee tembee ovyo.

Nimeitoa katika kitabu cha HADITHI na visa kutoka Tanzania.

9 comments:

WIM said...

Dear Yasinta. Natembelea blog yako mara kwa mara. Leo nimeona picha ulizopiga za nyumbani tumezipenda sana. Inanikumbusha nilfika Songea miaka ya late 80's. Karibu sana Tampere, Finland.

SIMON KITURURU said...

Si nasikia kuna wanaume walafi tu na kama pendo lao linakunwa na dogodogo, hata aliyezeeka AU TU KUANZA KUZEEKA awe anatii mume kiasi gani ,anaheshimu ndoa ile mbaya na kujipendezesha mdoli umesingiziwa -si bado INASEMEKANA lipendalo DOGO DOGO mali mpya makaratasi watoa mwenyewe litadai dogodogo ndiye mtamu?

Halafu si nasikia kuna wachokao kila siku chai na maandazi tu?


Nachojaribu kusema LABDA fundisho la hadithi hii lategemea tu mtu na mtu!

NI hilo tu!

Chacha oWambura said...

Mtakavitu Simon, kwa kiasi nakubaliana nawe katika hili "Nachojaribu kusema LABDA fundisho la hadithi hii lategemea tu mtu na mtu!"

Lakini nakubaliana na Yasinta kuwa wanawake wanapaswa kuwa WATII. Katika miaka yangu ya ubaba-paroko na mpaka sasa hivi nikiwa mstaafu, sijawahi kukutana na kesi ya ndoa ambapo mama analalamika kuwa mumewe hamtii wala baba kulalamika kuwa mkewe hampendi bali kinyume chake....lol

kama biblia inavosema katika waraka wa Mt.kitururu sura ya.... kwamba "enyi waume wapendeni wake zenu kama nanihii alivolipenda kanitha lake..."lol

na 'enyi wake watiini waume zenu...lol

Ukiangalia kwa ukaribu kwa mujibu wa Yasintha, vitu alivoelezwa yule mke bwege ni va kutekeleza utii kwa mumewe...lol

I wish wanawake wote wa kikuyra wangekuwa wanasoma blog hii...lol

Bennet said...

Tatizo wanawake wengine wakisha zaa tu basi wanajisahau na kujiweka hovyo hovyo tofauti na wakati ule mapenzi yalipoanza

Chacha o'Wambura said...

Bennet, kwani humkumbushi akichakaa?...lol

Koero Mkundi said...

Wewe chacha unasema wanawake wawatii waume zao basi na hao waume wawatii wake zao pia na waache ulafi wa nyumba ndogo, wanaume siku hizi hata wakilambwa miguu watatoka tu kuonjwa vya nje, hawaridhiki na haweatosheki....!@#$% na ndio maana siwataki....LOL

Chacha o'Wambura said...

Da Koero, nadhani Mt Simoni kasema vema kabsaa ya kuwa inategemeana na mtu na mtu...lol

Kinachohitajika ni utii (mwanamke) na upendo(mwanamme). Vyote hivo nadhani ni complement kwa kila moja...lol

na kutokana na ninavosoma btn the lines hapo juu inaonesha kuwa pamoja na kuwa 'huwataki' lakini bado unawa'penda'...lol

What a fallacy...lol Ni kama ile story ya sizitaki mbichi hizi...lol

Habari ndo hiyo...lol

Yasinta Ngonyani said...

Napenda kuchukua nafasi hii na kuwashukuruni wote kwa kunitembele na pia kwa maoni yenu mazuri. Naomba mjadala uendelee.

salva george said...

badilisha fikra,badilisha maisha

http://scottlove.weebly.com/