Wednesday, March 3, 2010

AHSANTE MUNGU KWA KUITENDEA FAMILIA YA MZEE NGONYANI MIUJIZA

Nakumbuka mwaka 1996, kuna tukio la kushangaza kidogo lililotokea katika tasnia ya Michezo kule nchini Italia na kuushangaza ulimwengu.
Tukio hilo lilimtokea mchezaji wa Kimataifa aitwae Nnwanko Kanu. Huyu alikuwa ni mchezaji wa Timu ya taifa ya Nigeria, ambaye alikuwa akichezea timu ya Ajax ya Uholanzi.

Ni baada ya Kuiwezesha nchi yake kutwaa kombe la Olympic, hapo mnamo mwaka 1996, ndipo alipopanda kilele cha mafanikio na kununuliwa na timu maarufu ya kule Italia inayoshiriki ligi ngumu ya almaarufu kama Serial A.

Mchezaji huyu alinunuliwa na timu ya Inter Milan na ni wakati alipokuwa akifanyiwa vipimo vya afya,(Medical Check Up) ndipo matokeo ya vipimo hivyo vilipoushangaza ulimwengu. Nnwanko Kanu aligundulika kuwa na matatizo ya moyo na alitakiwa kufanyiwa upasuaji haraka sana ili kunusuru afya yake.

Ikumbukwe kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa akishiriki ligi za kimataifa, akichezea timu ya Ajax ya Uholanzi pamoja na kuchezea timu yake ya Taifa ya Nigeria na kuiwezesha kutwa kombe la Olympic, lakini katika kipindi chote hicho haikuwahi kugundulika kuwa na tatizo hilo. Hata hivyo kulikuwa na kupingana kwingi kitaalamu kati ya madaktari wagunduzi wa tatizo hilo na wale wa Uholanzi, lakini hatimaye alifanyiwa upasuaji na kurejea katika anga za michezo na kupata mafanikio makubwa.

Nimelikumbuka tukio hili kutokana na kile kilichomtokea mdogo wangu Asifiwe, huyu ni mdogo wetu wa mwisho kuzaliwa. Tukiwa tumezaliwa wanaume watano na wanawake wawili, yaani kati ya watoto saba wa Mzee Ngonyani na mama Ngonyani tuko watoto wakike wawili tu, yaani mimi na huyu mdogo wangu Asifiwe.

Akiwa darasa la sita ndipo alipoanza kuugua, ghafla, na tatizo kubwa lililokuwa likimsumbua ilikuwa ni tatizo la kukosa nguvu ghafla na kubanwa na kifua, lilikuwa ni tatizo ambalo kule Songea katika Hospitali ya Peramiho hawakuweza kugundua kuwa ni tatizo gani lakini kwa juhudi za madaktari aliweza kupewa tiba ambayo hata hivyo ilimletea nafuu badala ya kumponyesha.


Ni mwaka jana mwezi wa pili nilipokuwa nyumbani Tanzania ndipo nilipokata shauri tumpeleke katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi. Ni hapo ndipo tulipo shangawa na matokeo ya vipimo kuwa mdogo wetu Asifiwe anayo matatizo ya Moyo na anatakiwa kufanyiwa Upasuaji nchini India.

Naamini hata wewe unayesoma hapa unaweza kuhisi ni kwa kiasi gani nilikuwa naumia kwa kile kilichomtokea mdogo wetu.

Hata hivyo baada ya kushauriana na madakatari alipangiwa kuwa awe anakuja pale Muhimbili kwa ajili ya matibabu yaani kliniki huku mchakato wa kufanyiwa upasuaji nchini India ukiendelea.

Kwa hiyo akawa anakuja Muhimbili na kurudi Songea (Ruhuwiko). Lakini mara hii ya mwisho yaani mwezi wa kwanza mwaka huu alipofika Kliniki aliandikiwa kufanyiwa upasuaji hapa hapa nchini na hivyo kulazwa pale Muhimbilli akisubiri kufanyiwa upasuaji.

Ni katika kipindi hicho sala na maombi vilifanyika kumuomba mungu afanikishe upasuaji huo ili mdogo wetu apone na kurejea shule kuendelea na masomo.
Mnamo tarehe 16/02/2010 mdogo wetu Asifiwe alifanyiwa upasuaji wa moyo na kwa uwezo wa Mwenye Enzi Mungu upasuaji ulikwenda vizuri na ijumaa tarehe 27/02/2010 ametolewa nyuzi zake na tarehe 01/03/2010 jumatatu ameruhusiwa.

Leo napenda kumshukuru Mwenye Enzi Mungu, Madaktari, Manesi na watu wote kwa Juhudi zao katika kumuhudumia mdogo wetu Asifiwe, sisi tunasema kwamba kwa uwezo wake ameweza kuisimamia kazi hiyo ya madaktari na kufanikisha upasuaji huo.Pia shukrani nyingi sana kwa daktari Mrs. Mushi wa kule Peramiho yeye ndiye aliyetupa ushauri wa kumpeleka Asifiwe, Kwanza katika kliniki moja hapa Dar ya Dr. Johnson M. Lwakatare. na ndipo tukapata rufaa ya kwenda Muhimbili .

Sisi tunaamini ni mungu pekee kwa kupitia mikono ya madaktari wale pamoja na manesi ameweza kufanikisha upasuaji huo. Nakumbuka siku tatu kabla ya kufanyiwa upasuaji huo nilizungumza na mdogo wangu, na kwa huzuni alinijulisha kuwa watoto wawili wa kike ambao walitangulia kufanyiwa upasuaji kabla yake wamepoteza maisha, ni watoto ambao walikuwa wana umri wa chini ya miaka 10, na walihitaji bado kuishi lakini Mwenye Enzi Mungu aliwapenda zaidi, na hivyo kuwatwaa. Ila namsifu Asifiwe, yeye hakuwa mwoga isipokuwa hakupenda kama ingetokea bahati mbaya kutuacha sisi nduguze.

Tulifanya maombi kwenye simu na nilimpa moyo mdogo wetu kuwa yote tumuachie Mungu kwani tunaamini atatenda miujiza. Lakini hata hivyo upasuaji uliahirisha tena kutokana na ziara ya ghafla ya mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete alipotembela hapo hospitali ya Muhimbili kuzungumza na madaktari.

Leo hii kwa niaba ya familia ya mzee Ngonyani napenda kuchukua nafasi hii kusema Ahsante Mungu kwa kuitendea familia ya Mzee Ngonyani Muujiza, Pia ningependa kuwashukuru wote mliokuwa nasi katika sala, katika kutupa moyo wakati tulipokuwa na mawazo. Na shukrani nyingi zimfikie kaka yetu Ngonyani na mkewe wa pale Kinondoni Kinondoni Mkwajuni kwa kuwa karibu nasi wakimhudumia mdogo wetu katika kipindi chote alipokuwa akija kliniki na hata wakati wa kufanyiwa upasuaji. Ninawashukuru kwa kuwa walitumia muda wao mwingi kwenda na kurudi Muhimbili ili kuhakikisha mdogo wetu Asifiwe hajisikii mpweke.
Na pia napenda kumpongeza yeye mwenyewe Asifiwe kwa kutoonyesha uoga.

Ningependa kuzisindikiza shukrani hizi kwa wimbo wa Upendo Nkone uitwao Hapa nilipo.







31 comments:

Fadhy Mtanga said...

Dada Yasinta, napenda kuwapeni pole nyingi kwa kipindi chote ambacho kilikuwa kigumu sana kwenu. Nakumbuka niliongea nawe siku moja kabla ya operesheni. Nakiri hali uliyokuwa nayo ilinipa nami maumivu makubwa.

Lakini sasa nafurahi kuona Mungu ametenda miujiza. Hakika Mungu ni mwaminifu na msikilizaji wa maombi yetu. Lakini twapaswa kufahamu kuwa pamoja na maombi yetu, mapenzi yake Mwenyezi Mungu ndiyo hutimizwa. Tunajifunza kumshukuru Mungu katika yote.

Hatupaswi kuwa na hofu, maana tunasema,
"Nijapopita katika bonde la giza kuu, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe ee Mwenyezi Mungu u pamoja nami.
Zaburi 23:4"

Hivyo tunamshukuru Mungu kwa kumsaidia ndugu yetu na kumponya. Nimtakie afya njema na maisha marefu sana.

Pamoja daima.

Mija Shija Sayi said...

Kwanza poleni kwa kuwa roho juu kipindi chote tangu aanze matatizo ya moyo na Sasa hongereni kwa uponyaji. KWELI MUNGU AHIMIDIWE.

ASANTE MUNGU WETU.

Anonymous said...

Mwenyezi Mungu amjalie afya njema Asifiwe na familia nzima ya Ngonyani iwe na heri nyingi. Naam, nafikisha habari hii kunako wahusika (jikoni kwenyewe).
Thx for sharing this Yasinta.

Koero Mkundi said...

Nakumbuka ulinijulisha juu ya uwepo wa mdogo wetu Asifiwe pale Muhimbili kabla sijasafiri kuja huku Arusha. Niliwasiliana na Asifiwe kwa njia ya ujumbe wa simu mara kadhaa kabla ya kufanyiwa upasuaji. Niliwahi kumtumia sala ya kuomba ili mwenye enzi mungu atande miujiza.
Nashukuru kwamba hili limetendeka, na sasa Asifiwe ameruhusiwa na yuko nyumbani. Ni jambo la kumshukuru mungu kwa muujiza huu, na ninaamini kuwa kama ilivyotokea kwa huyo mchezaji Nnwanko Kanu, wa Nigeria, hata Asifiwe atarejea shule na kusoma kwa bidii hadi chuo kikuu, na hivyo familia ya Mzee Ngonyani kujivunia kuwa na mtoto Asifiwe.

PASSION4FASHION.TZ said...

Poleni sana na hongera,kwa kweli hizi ni habari zenye mchanganyiko wa huzuni na furaha,huzuni ni kipindi cha kusubiria upasuaji ufanyike hiki huwa nikipindi kigumu sana kwa mgonjwa na kwa wanafamilia,lakini mungu ni mwema ukimtanguliza yeye kwa kila jambo huwa hamtupi mtu,furaha yangu ni kwa jinsi mungu alivyotenda huo muujiza wa uponyaji na nafurahi sana kusikia kuwa Madaktari wetu wanaweza kufanya uapasuaji kama huo kwa kweli wanastahili pongezi za hali ya juu kabisa,mungu aendee kubariki kazi zao kila penye ugumu apafanye pepesi pawezekane hakuna kisicho wezekana kwa imani kila jambo lawezekana.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kama nilivyogusia katika post yangu ya jana, tunao madaktari wazuri sana nyumbani. Tatizo kubwa lilikuwa ni ukosefu wa vitendea kazi na kutothaminiwa kwao ikiwemo mishahara midogo na kutoruhusiwa kwao kuwa na kliniki/hospitali zao binafsi. Inatia moyo kwamba sasa mambo yameanza kubadilika na hizi safari ghali za kukimbilia India au Afrika kusini baada ya mtu kupata "heart attack' zitapungua.

Ni jambo jema kwamba Asifiwe amepona. Mungu Asifiwe!

Anonymous said...

Dada Yasinta its soo touchind msg huwezi amini machozi yamenitoka nina mtt nae anatundu ktk Moyo naomba umwombee ma only gal ...Asifiwe mdogo wetu mungu akuoe nguvu hakuna lisilowezekana kwa mungu.......Wimbo huu wa Abiudi naupenda "Tenda Miujiza usiache mungu mwaka huu upite bila kutenda Muujiza"Dada Yasinta Mungu ametenda muujiza

Mwanasosholojia said...

Ni jambo la kumshukuru Mungu na kuzidi kumwombea mdogo wetu

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Mungu pekee ANAWEZA! Ushukuriwe ee Mungu wa Yakobo kwa kuwa ilikupendeza kuifanya hiyo operation kwa mikono ya binadamu!

Tunamuombea Dada Asifiwe apate nafuu mapema na kurejea katika shughuli zake za masomo!

Amina!

EDNA said...

Hakuna lisilowezekana kwa yeyote aaminiye,Hongera sana Asifiwe Mungu ashukuliwe.

Lulu said...

Jamani tuwe tunawapa watoto majina mazuri kwani huwa yanaweza kusaidia au Kuharibu. "Asifiwe" ni jina tamu hata mbele za Mungu na ndio maana Mungu aliye mkuu ametenda miujiza ili sifa na utukufu wake vijidhihirishe na SIFA apewe yeye. Yasinta na Ngonyani family kwa ujumla endeleeni kumsifu Mungu kwa kushusha sifa zake kwenye familia yenu!!

mnkadebe said...

Amina na amina tena Dada Yasinta. Tumshukuru Mungu kwavile "hapa hatuna mji wa kudumu, bali tunautafuta ule mji ujao".
"Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele,awape ninyi kila kitu chema, ili mpate kutimiza mapenzi yake akifanya ndani yenu lile linalopendeza machoni pake, kwa njia ya Yesu Kristo; yeye apewe utukufu milele na milele". Waebrania 13:20-21

John Mwaipopo said...

wakati nataka kuchangia jana mtandao ukaleta kwikwi lakini hisia nilizokuwa nazo jana zi ngali hali. usomapo post hii ya uponyaji hakika unapatwa na simanzi na faraja. mie ni mwepesi wa machozi, jana yalinilengalenga sana wakati nikiisoma hii post mstari mpaka mwingine.

basi yatosha kumshukuru mungu mponyaji mkuu kupitia mikono ya madaktari na manesi na wengine wote walioshiriki kwa njia moja ama nyingine kumponya dada mdogo asifiwe.

asifiwe ni jasiri. nadhani nisingalikuwa na ujasiri kama aliokuwa nao yeye katika mazingira yale ya wagonjwa waliomtangulia kupoteza maisha. hongera.

kama nwanko kanu basi asifiwe atakuwa na mafanikio mbeleni. nyota njema huonekana mapena na hii ya asifiwe kaileta mungu mwenyewe. sasa amepata uhai wa kumuwezesha kushiriki vema darasani na hatimaye pengine naye aje kuwa daktari. hongereni familia ya mzee ngonyani.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Eti Mungu wa YAKOBO!!!!! wa Chacha je?? anarushamawe??

mimi nafurahia matatizo kama haya. ni kwa ugonjwa huo kuna madaktari wamepata umaarufu, ajira na malipo.

yasinta kapata cha kutundika bloguni kushika hsia za wachangiaji wote na kila mtu anatamani kuwa mkubwa a.k.a ndugu wa mgonjwa wakati wengine wanamnyemelea, urafikiumejengwa nk

kwa hiyo ugonjwa kama huu na uendelee kuwepo, kuja na kutukamata tu upendavyo.

Chib said...

Kusanya mawazo ya woooote hapo juu, basi na mimi nimeyasema yoooote

Chib said...

Kusanya mawazo ya woooote hapo juu, basi na mimi nimeyasema yoooote

Unknown said...

Sasa mimi niseme niji.
Labda niseme tu kuwa jina la mwenye enzi mungu lihimidiwe ......aaamen,

Unknown said...

Samahani hapo juu nilitaka kusema.
"Sasa mimi niseme nini?"

Simon Kitururu said...

Naona yote yameshasemwa!

Poleni sana na na namtakia Asifiwe kila lakheri!

Anonymous said...

Hii imekaa vema sana, yaani kuomba na kushukuru baada ya kupata kile ulichoomba. Nami naungana nanyi kumshukuru Mungu kwa wema wake kwa mdogo wako Asifiwe. kama jina lake linavyojieleza yatupasa kumsifu kwa matendo yake makuu aliyoyafanya. Nimefurahi kuona pie umewakumbuka madaktari, hasa Dr. Mushi, natumaini huyo Mushi unayemzungumzia hapa atakuwa ni Mrs. Mushi maana wapo wawili pale Peramiho, mtu na mkewe, hivyo natumaini atakuwa ni Dr. Mrs. Mushi maana mumewe ni daktari wa meno. Ninaweza kuandika kurasa kibao kumwelezea huyu Dr. Mushi (Mrs). ni mtu mwema, anajali wagonjwa na ni mchapakazi kwelikweli. naweza kuandika zaidi lakini wacha niishie hapo ili nipate muda wa kufanya kile mabosi wangu wanahitaji nifanye.

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii kwa kuwashukuruni wote kwa maoni yenu mazuri ya kutia moyo. Na pia nimeongea na Asifiwe jana anaendelea vizuri kabisa. Ni kweli ni jambo la kumshukuru Mungu kwa muujiza huu.Ahsanteni sana.

Anonymous said...

with caution, but our study of one patient with vitamin C deficiency and with H pylori eradicated does lend some supporting evidence. H pylori infection is now recognised as http://buyviagraonlineauviagra-au.com#3,9839E+27 buy viagra online all the Doctor's masks had been stripped away, leaving him with no more armour than the truth. She shivered. '' It's very hard for me to http://buyviagra100mgcostviagraonline.co.uk#1,88389E+68573 viagra 967 Cortisol (hydrocortisone), the stress hormone, and cortisone basically works against insulin

Anonymous said...

Great Taste No Pain is created by Sherry Brescia, a health researcher cheap lumigan Let's explore how amino acid supplements can work for your benefit
When it comes to the way you feel and emotions, don't look for external solutions because that will lead to thinks lick smoking addiction and alcohol addiction cheap cymbalta These people have conquered their depression and they have great advice to share with you!
It will help relieve some of the inflammation Viagra for women pills It is good to shower on a regular basis to cleanse the skin especially around the anus
She practically invented this look! She sported her usual ethereal glow at the Golden Globes again this year generic iressa Hence, Thypro answers all your queries and helps you maintain a sound body and mind
I hope you found these general anxiety treatments useful Asacol Keep a strict check on your diet

Anonymous said...

Остренькое! [url=http://aftertube.net.ua/tags/%E7%E0%ED%E8%EC%E0%E5%F2%F1%FF/]занимается[/url] Посмотри про то как [url=http://aftertube.net.ua/tags/%ED%E0%E1%EB%FE%E4%E0%F2%FC/]наблюдать[/url]
со слабыми нервами вход воспрещен!

Anonymous said...

It assists in developing websites which is established as well as stretched an organization’s products, corporate identity, and grabs business clients online across the world. unblockwebs. In this particular issue, the middle class has been found to be assertive in fighting for better health than other classes. facebook unbloker

Anonymous said...

To answer you crisply, yes there are few fish oil side effects viagra Allow the feelings to spread and deepen Depression is extremely common cialis uk There are also many other foods like fast food, processed foods, refined sugars, milk and poultry which are also toxic and will cause body odor when they are emitted from the body

Anonymous said...

Esophagus is nothing but a structure similar to a tube which is hollow in the centre and enables free movement of food and liquid through it. windows os for mac. Quantum ensures supreme quality and highest level of durability in each of its products. vpn network ubc

Anonymous said...

Essential oil candles emit a fragrance of specially selected oils, which when put into the air; offer a healing factor as the vapors are inhaled. ata raid ethernet video high

Anonymous said...

Log in everything you do, and take lots of photos for your science fair project and display. feisty server. However, there is also room given to students who might be somewhere near the answer. red hat advanced server 3

Anonymous said...

Pretty! This has been an extremely wonderful post.
Thanks for providing these details.
Feel free to surf my blog Diet That Works

Anonymous said...

Concluding Remaгks In determinаtion, it сan be ѕaid that tantric mаsѕage thеrapy cаn
safеlу bе interpreted by you testament haνe the pleasure to meet with
our hot аngelѕ. Αs pr�tіcas de tantгic
massagе variam de severe buгnѕ is demanding and challenging unԁertaking.



My blog post - website