Tuesday, March 30, 2010

Robo mwaka inakatika...Tumesonga mbele ama nyuma???

Amani, Heshima na Upendo kwenu.



Kwanza namshukuru MUNGU kwa baraka ya uhai ambayo mimi nawe tunayo.
Pili nikupe pole kwa harakati za maisha ambazo sote twazipitia kufanikisha yale mema tupendayo.
Nafurahi kuwasiliana na kila mmoja wetu kuweza kuwaza changamoto zilizo mbele yetu kama JAMII YA WANA-BLOG wenye lengo la kuigusa jamii na kisha tujiulize kama tunasonga mbele ama nyuma katika harakati zetu. Nashukuru kwa blogs na tovuti mpya ambazo zinachipuka na kuendeleza nia njema ya kuigusa jamii. Kaka Luta Kamala aliwahi kuandika akijuliza KWANINI TUNA-BLOG? (http://kamalaluta.blogspot.com/2009/07/swali-kwa-wenye-blogu.html) na hata Kaka Chambi Chachage aliuliza kama uwepo wa blog zetu unakuza ama kufifisha tasnia nzima ya uandishi (http://udadisi.blogspot.com/2009/08/blogu-zinachochea-au-zinafifisha.html). Jibu halisi tunalo mioyoni mwetu kulingana na dhamira tulizonazo.
Lakini kwa ujumla, haijalishi ni sababu gani ilikufanya u-blog, mwisho wa safari sote tunajikuta na zao moja ambalo ni JAMII. Awekaye picha anataka kuionesha jamii alichokiona, ahabarishaye anataka kuihabarisha jamii. Yule aandikaye Utambuzi anataka jamii ijitambue. Anayeweka kumbukumbu ni sababu anataka jamii ije isome baadaye. Atangazaye biashara anataka jamii ijue ilipo huduma. Afunzaye mapishi, mitandao, mavwazi, mitindo nk, woote wanalenga katika kuielimisha jamii.
Kwa maana nyingine sote twaiandikia JAMII.
Lakini je, mwaka huu ambao unamaliza robo yake ya kwanza wiki hii unaonekana kuwa hatua gani kwetu? Tumeshuhudia KUTHAMINIKA KWA KAZI ZA BLOGGERS kwa aina mbalimbali.
Tuliona wenzetu wakitunukiwa vyeti vya kuthamini kazi zao, tumesikia wengine (kupitia utambulisho wa blog zao) wamepata nafasi ya kushiriki vipindi vya idhaa za kimataifa kufanya uchambuzi wa habari. Hivi juzi tumemuona Kaka Michuzi akishiriki Diaspora huko London kwa nafasi yake kama blogger. Hizi ni chachu kwetu kuwa kuna kuonekana mchango wa kile tufanyacho na pia kuna kukua kwa ueleweka wa kazi zetu.
Ninalowaza ni VIPI TUNAWEZA KUWEKA NGUVU NA JITIHADA ZETU PAMOJA KUWEZA KUITUMIKIA VEMA JAMII?
Mafanikio ya blogger mmoja mmoja yanaweza kudhihirisha kuwa TUNAWEZA na tunalostahili kufanya ni kushirikiana na kuwa makini katika kila jema tutendalo.

Tunapoianza robo ya pii ya mwaka 2010, tuangalie nyuma na kujiuliza, robo ya mwaka inakatika....Tumesonga mbele ama nyuma??
Na hii iwe CHANGAMOTO YETU sote

Baraka kwenu nyote

http://www.changamotoyetu.blogspot.com

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ninanukuu "Ninalowaza ni VIPI TUNAWEZA KUWEKA NGUVU NA JITIHADA ZETU PAMOJA KUWEZA KUITUMIKIA VEMA JAMII?
Mafanikio ya blogger mmoja mmoja yanaweza kudhihirisha kuwa TUNAWEZA na tunalostahili kufanya ni kushirikiana na kuwa makini katika kila jema tutendalo." mwisho wa kunukuu. Umoja ni nguvu na penye nia....Kwa hiyo TUTAWEZA TU. Upendo Daima!!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Yes We Can!

Koero Mkundi said...

Hii ni changamoto yetu wote.....

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

haya

Mija Shija Sayi said...

Mzee wa Changamoto, kila nikisoma waraka huu eti naona kama hujamaliza vile? sijui kwa nini?
Unaweza ukaendelea?