Nipo juu ya mlima Kilimanjaro!!Majira ya baridi kali , ni mwezi huu wa tatu na hapa ilikuwa jumamosi iliyopita
Hapa baridi inaanza ni mwezi wa nane mwaka 2009 (autumntime) Höst. Ni majira ya kupukutika kwa majani.
Hapa ni 2009 mwezi wa nne-tano (Springtime) Majira ya kuchipua.
Na hapa ni mwaka 2008 (Summertime) Majira ya joto hapa tupo mji wa Karlstad nje ya tangi kubwa la maji.
NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MWISHO MZURI WA JUMA HILI , MUWE NA WAKATI MZURI NA AFYA NJEMA !!!!!
13 comments:
Nafikiri Chacha au Kamala wakikuletea picha za misimu tofauti ya Bongo.... maana barabara zote hubomoka wakati wa mvua, kikija kiangazi ni vumbi na uhaba wa maji, kipupwe ndo usiseme hakuna amani tu.
Wikend njema nawe
Picha zinatekenya kweli mvutio machoni mwangu!:-(
Mdada wewe Mrembo kweli !
Namna hii kwanini Yasinta usipende chai?
Kama hali hyo ingekuwa ni haa bongo, watu wangeshaijaza dunia kwa kuzaana......
kama kule kwa wagema ulanzi ndio ingekuwa balaaa....
@damija, unaongelea chai ipi anayoipenda ili ikiingia baridi iishe?? ya jikoni au?
Chib: picha zipo mwenyewe anaweza asiamini.
Yasinta: hilo jaketi na suruali umevivaa ama vimekuvaa?
Sijui kama mimi ningeweza kusavaivu hiyo mineno. Nakumbuka mwaka 2005 nilitua Boston na yakanikuta ya kunikuta ya HILO baridi ikabidi nikimbilie San Fransisco nikae huko ktk kipindi choote cha miezi 3 nilopanga kuwa huko.
Pamoja na kubomoka barabara lakini bado napenda hali ya hewa ya hapa...lol
Nawe Poa tunakutakia kila la kheri katika mwisho huu wa wiki.
PamoJah Dada Jasinta
nauliza, kwani baridi na joto bora nini? mimi napenda baridi kuliko ugali ndo mana siwezi ishi Dar niko Arusha.
Yasinta wale watoto ni wa kwako? mbona kama wazungu vile?
GOODLUCK ARUSHA
nasisi huku kibaridi ndio kinaishia na tarehe 4th april tutakuwa na sikukuu ya mauwa, hivyo tutakuwa na holiday ya kuangalia mauwa nafikiri kipindi hicho sakura pia itakuwa imechipua
Mumie hili baridi heri liishe....laumiza mimi!
Dada Yasinta,umemsikia Simon (Kitururu).Kaniacha sina mbavu.Je hao kwenye picha nne ni wanao?Mmependeza sana.
Goodluck: Una vitimbi weye! ati watoto wazungu!
Si yawezekana baba yao akawa mzungu?
Ahsanteni wote kwa kutochoka kuitembelea blog hii ya MAISHA NA MAFANIKIO na pia kwa maoni yenu. UPENDO DAIMA
Na kaka evarist ndio hao ni wanangu.
Post a Comment