Wednesday, March 10, 2010

Wakati leo ni siku ya mayatima, hebu sikilizeni story ya rafiki yangu huyu!!!

Hakuna asiyehitaji upendo
sikieni story ya rafiki yangu huyu.. Kila tarehe 10 march huadhimisha siku ya watoto wa mitaani kwani miaka kadhaa iliyopita tarehe na mwezi kama huo aliingia rasmi mitaani kama mtoto aishiye kwenye mazingira magumu hadi miujiza ilipotokea akakombolewa baada ya kusota huko mitaani zaidi ya miaka miwili. Baadhi ya shida alizopata akiwa huko mitaa ni pamoja na

1. Kunusurika kuuwawa na watu wenye hasira akidhaniwa mwizi, baada ya kukurupushwa usiku kwenye vilabu vya pombe za kienyeji alikokuwa amelala, aliokolewa na msamaria mwema aliyekuwa akimfahamu
2. Kulala kwenye vilabu vya pombe za kienyeji, stand za mabasi na madarajani hata wakati wa masika
3. Kulimishwa mashambani, madukani na migodini kwa ujira wa ugali, nk.

Anasema katika maisha yake amewahi kujaribu kujinyonga mara mbili ……anaongeza kuwa hajawahi kuona mtu akimpenda kwa dhati maishani mwake………….. hata wanawake alianza kuwapata baada ya kupata kazi na hivyo kuwa na pesa za kuwahonga.

Ilitokea miujza, akatokea mtu akamuingiza shule na kumtunza kwa miezi sita tu kabla hajasema mzigo wa kulea umemuelemea na kumfukuza nyumbani……..lakini kamwe hamsahau mtu huyo, kwani kwake ana hadhi ya malaika wa Mungu …………….. kuna maelezo marefu hapo yanafuatia lakini sasa tuko naye chuo kimoja huku nje ya nchi, yeye akichukua PhD,………….

Amenisimulia haya baada ya kumkuta amepamba chumba chake kwa maua na akisikiliza nyimbo za gospel kwa wiki nzima mfululizo (kumbuka tarehe 10 march ni jumatano ijayo), ndivyo anavyoadhimisha siku hii kwa mwaka huu,………… kweli story yake inasikitisha sana……… machozi yamenitoka leo…………

je, tumfariji namna gani huyu ndugu?...............

HII NIMEIDESA JAMII FORUM nami nimeona sio vibaya nikiweka hapa Maisha na Mafanikio tuweze kujadili/kujifunza kwa pamoja!!!!.

9 comments:

Koero Mkundi said...

Hii stori inasikitisha sana na inaonyesha pande mbili za wanaadamu.
Sisi hatujui litakalotutokea kesho wala litakalowatokea watoto wetu kesho ni vyema tukawafanyia wengine vile ambavyo tungependa tutendewe.

Hivi ni watu wangapi wenye uwezo lakini wameshindwa hata kuchukua mtoto yatima au wa mtaani na kuishi naye kama mwanaye?

Tunahitaji kubadilika kwa hili, kwani hili ni jukumu letu sote.

Kilichonifurahisha katika stori hii, ni kuona kuwa pamoja na kupata misukosuko ya maisha lakini kijana huyu aliamini kuwa anaweza, na hakika ameweza.

Hakika kwangu mimi huu ni kama muujiza.

Sisulu said...

KILA MTU anahitaji upendo binafsi nimependa hii sentensi mimi binafsi nina babu yangu aliyepoozakwa upande wa kulia wa mwili wake na kwa maaana hii hawezi kuzungumza umri wake ni mkubwa na siku za hivi karibui amekuwa akitenda kama mtoto.kitu nilichogundua babu yangu huyu anahitaji sana upendo.mayatima wanahitaji upendo.NI HAKIKA

Mija Shija Sayi said...

Hata tumfariji kwa kiasi gani haitasaidia kwa sasa. Ataona ninafarijiwa sasa kwa vile nina kitu, kitu kimoja kinachoweza kumfariji labda ni kuwasaidia wale walio miitaani sasa hivi, kuhakikisha watapata maisha wanayo stahili.

Mtizamo wangu.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Pamoja na matatizo yoooooooooote, bado tuna uwezo wa kuwa kile tulichoandikiwa.

Hongera kijana.

Yasinta Ngonyani said...

Hapa nakunukuu Da Koero "Hivi ni watu wangapi wenye uwezo lakini wameshindwa hata kuchukua mtoto yatima au wa mtaani na kuishi naye kama mwanaye?

Tunahitaji kubadilika kwa hili, kwani hili ni jukumu letu sote." Mwisho wa kunukuu:- Kwanza kabisa hao watu wenye uwezo ni wabinfsi ndio maana hawafanyi hilo pia hawana upendo. Na kuhusu kubadilika ni lazima mmoja aanza la sivyo hakuna ule mfano wa kuiga. si unajua tabia zetu za kuoga. Pendekezo langu kwa nini serikali isijenga shule na nyumba ya kutunzia watoto hao? na pia kuwa na walimu/walezi?

MARKUS MPANGALA said...

yatima, wanatoka wapi?

watila said...

hayo ndo maisha na mafanikio kweli kaka mpangala anauliza wanatoka wapi hawa yatima sijuwi nani ataweza kumsaidia ndugu yetu nani ni yatima ?

chib said...

Hujafa, hujaumbika....

Simon Kitururu said...

Siku hizi mambo yote ujanja ni kwenye kalenda kuyatafutia siku.:-(

Matatizo na siku za maadhimisho !
Siku ya Mayatima.
Siku ya Ukimwi
Siku ya WEUSI
Siku ya Wasenge

Siku ya akina MAMA
Siku ya Malaria.....nk


Unaweza mpaka ukafikiri haya matatizo hayako mwaka mzima. Na usipo anagalia matatizo ya YATIMA kesho huyafikirii sana kwa kuwa nayo ni siku ya UKOMA au tu VALENTINE kwa hiyo inabidi ulazimike kumjali mpenzi naye asije kukuona humjali na kuanza kukunyima chakula cha usiku na kuzidisha kukununia bila sababu.


CHAKUJIULIZA:
Hivi kuna uhakika hizi Siku za MATATIZO bado zinalipa kama nia ni kujulisha UMMA kuhusu matatizo ya wahusika hasa zilivyo nyingi na zizidivyo kwa uwingi siku hizi?


Hivi madhumuni ya kuwa na SIKU MAALUMU kwa ajili ya swala moja MAALUMU bado ni njia ililetayo ufanisi?



..Kirahisi utaguswa zaidi na kinachocheza zaidi na kikuumizacho roho.

Daima hakuna atakaye weza kufanya yote.

Daima maneno hayatoshi kushughulikia matatizo yahitajiyo vitendo.

Kuhusu NDUGU huyu ambaye kaongelewa katika topiki nahisi ahitajicho ni upendo tu na ni na dawa anayo yeye mwenyewe kwa kuwa ni mpaka ajisikie anapendwa yeye binafsi ndio anaweza kuondokana na kujisikia hapendwi. Nafahamu baadhi ya watu ni mpaka wawe na watoto wao wenyewe wajisikie wanapendwa bila masharti ndio hupona mikwaruzo iliyojengwa na kuwa MTOTO yatima.


Dawa ni UPENDO tu ,...
..... ila kwa bahati mbaya kila mmoja anastaili yake tofauti ya kusikilizia hii ndude iitwayo UPENDO.:-(

Kila mmoja atende awezavyo!