Monday, March 29, 2010

Nani wa kwanza kujulishwa mtoto anapozaliwa??

Nimewahi kusuluhisha ugomvi uliotishia ndoa ya mtu mmoja.

Mkewe alipojifungua mtoto wao wa kwanza aliwaambia kwanza rafiki zake (mashosti au mashoga zake) wote na mmoja wao ndiye aliyemwambia kwa msg mume kuwa kapata mtoto na jinsia ya mtoto. Mume akiwa haamini kama mkewe anaweza kujifungua bila kumjulisha alianza kwa kubisha na baadaye alipokwenda kumtazama alipokuwa amepumzishwa alimkuta kweli mkewe kajifungua na alipokagua simu yake alijiridhisha kuwa amejifungua zaidi ya masaa mawili yaliyopita na muda wote huo tayari alikuwa kishawajulisha mashosti wake wote bila kumkumbuka mumewe, mume alidai mkewe kamdhalilisha sana na hampendi tena.

Kwa mujibu wa maelezo yao hawakuwa na ugomvi wowote na wakati wote mama alipokuwa kwenye chumba cha kujifungulia mume alikuwa nje katika maeneo ya hospitali anahangaika huko na huko kuweka mambo sawa mama amaliza shughuli salama.

mnaonaje waungwana, nani anapaswa kuwa wa kwanza kujulishwa?

Mada hii nimeichukua kutoka JAMII FUROM, nami nimevutiwa nayo nikaona sio vibaya kuiweka hapa na tujadili kwa pamoja

9 comments:

John Mwaipopo said...

nadhani mama alijua kuwa mumewe hakua baba wa kibaolojia wa mtoto. nadhani pia mashosti walijua baba halisi ni nani. nadhani jamaa alikuwa na haki ya kufura kwa kutojuliswha kwanza.

ngoja kamala na mtakatifu kitururu nao waseme.

watila said...

duh kumbe yanawezekana mambo haya
sikufikiria mwaipopo kwani nani ilompeleka huyo mzazi hospitali si huyo baba watoto

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wa kwanza kujulishwa ndiye wa kwanza.



kuna vitu vingine kuvijua waweza jikwaa, hasa ukiambiwa na mhusika, kwa hiyo ni bora usikiasikie then uje gundua ukiwa umetuliza ujinga wako



lakini inafuatana na kipaumbele


kwa nini mlipata mtoto ili mashost wawakome au wafurahie??? wajulisheni tu


baba si atajua tu! kwani si alimpeleke hosp ili azae? si alishajua au???

Anonymous said...

Mbona story yenyewe inajicontradict? Kama baba alikuwa kweli hospitali nje ya labour room, manesi wangelikuwa wakwanza kumjulisha asingesubiri kuletewa sms na mashoga ambao wakati mkewe anajifungua wako mtaani yeye yuko nje ya hapo.

Wewe umeshawahi jifungua unafahamu hali ya mzazi inavyokuwa imediately baada ya kujifungua, na ni muda gani unatumika kumsafisha, kumweka sawa na hata kumrudisha chumbani/wodini kutoka labour room, inaweza chukua kati ya nusu saa mpaka saa nzima watu wengine kumuona, kwa hiyo mashosti walikuja hospitali baada ya saa nzima wakijua kuna mtoto wakati yeye aliyekuwa nje akisubiri mtoto azaliwe asijue?

Kuna mawili, ama ni hadithi ya kutunga/kufikirika ili kustarehesha baraza au imetokea kweli lakini mume was nowhere close to his wife au hata hospitali, pengine alikuwa kwa kimada na simu kazima hajui kinachoendelea mpaka kuja kuambiwa na mashoga. Sasa hiyo anatumia kama kujihami kuficha madhambi yake.

Swali kwa huyo mume na marafiki zake, siku hizi hata TZ wanaume wanaruhusiwa labour room, not necessary kushuhudia tendo la uzazi lakini hata before or immediately after birth, where was this man wakati mkewe anajifungua? Na kama alikuwa hospitali kumpa support mkewe kipindi hicho kigumu, kwanini akose taarifa ya uzazi wakati yeye ni next of kin?

Bi Mkora

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Kwako Bi Mkora: Natumai hujambo. Napenda hata hivo kuhitilafiana nawe kidogo kwa kukuambia kuwa:

Kuna baadhi ya wamama wanapokuwa wajawazito huwa wanawachukia waume wao na hata wanapojifungua bado huwa na hasira juu ya waume wao.

Kuna wengine wanapojifungua hujiapiza kuwa 'sitaki kuliona hilo janaume tena na sitazaa tena!'

Kwa mantiki hiyo na sababu hizo hapo juu yawezekana ikawa sababu mojawapo ya hao mashosti kuwa wa kwanza kujulishwa juu ya ujio wa mtoto wakati BABA anahangaika hapo nje kama KUKU ANAYETAKA KUTAGA.....lol

Nawasilisha

Anonymous said...

Bwana Chacha Wambura sikubaliani na hizo sababu zako, kwani haziendani na hiyo meseji inavyojieleza, labda nimeisoma vibaya ama between the lines, lakini kuna maswali zaidi kuliko majibu.

Mimi kama mwanamke Mungu Muumba amenijaalia kuzaa, yaani lile tendo la kubeba mimba mpaka kujifungua. Na mwanamke akishajifungua tu, hormones zote zilizokuwepo wakati wa ujauzito zinaondoka muda huo huo mtoto anapotoka, kwa mfano wanawake wengine wanashindwa kutest au wanakuwa na hali fulani hivi ya kushindwa kunywa hata maji mpaka waweke kitu kingine, au wanakuwa na hasira, chuki na hali ambayo inatokana na ujauzito. Na yote hayo huondoka mara moja mtoto anapotoka tumboni.

Pili sio hiyo hali inayotokana na hormones tu, mzazi husahau hata ule uchungu alokuwa nao wakati wa kujifungua, na hakuna kitu kigumu na kinachouma kama uchungu wa uzazi lakini mtoto akishatoka tu mama anasahau uchungu wote na kuwa na furaha ya kuona mtoto wake. Hata kama alikuwa na chuki, kisirani na hasira na nani vyoote hivyo vinaondoka. Ndivyo maumbile alivyoumba Mungu muumba ama sivyo wanawake wangelizaaa mtoto mmoja mmoja tu na wasingerudia tena kuzaa mtoto wa pili au hata watatu. Hebu jiulize kwa uchungu ule mtu mzima anapiga kelele kama mwehu au mtoto mdogo (uchungu wa uzazi hauna mfano wake) inakuwaje wanawake wanarudia kuzaa tena na tena?

Ndio maana nasema hiyo hadithi haina mashiko zaidi ya kawaida ya mfumo tuliouzoea, mimi mpaka mtu anipe sababu ya huyo mume kutokuwepo karibu na mkewe, wakati mkewe alipokuwa kwenye death bed, maana uzazi una mawili mtu atoke salama yeye na mtoto au wote wafe au mama aondoke aache mtoto au mtoto afe mama apone. Sasa inakuwaje huyu baba asiwe hata nje ya hospitali kama huyu mama alikuwa hataki kumuona kama ulivyosema?

Mimi bado nasema huyu alikuwa kwa kimnada tu maana wanaume wengine kutwa mara tatu kama dawa za hospitali na wake zao wakiwa katika hali hiyo last semester tena karibu ya kujifungua mama anakuwa hawezi kufanya tendo la ndoa basi ndio anaishia huko kwenye spear tire, matokeo yake mtoto anazaliwa mwanaume hana habari.

Mwisho namalizia kwa kusema kuwa mwanaume yoyote yule ambaye hajui hata kama mtoto wake anazaliwa ni mzembe na hafai kuitwa baba.

Bi Mkora

Mija Shija Sayi said...

Hizi ndizo stori ambazo mimi husemaga ili kupata ukweli ni lazima wahusika halisi wawekwe kati, vinginevyo tutaishia kulumbana tu. Nimesoma maoni ya wote juu na yote naona yanawezekana.

Yasinta Ngonyani said...

hii ni ajabu kweli kwani kwa mimi najua mila zote ya kwamba hapo ni lazima mume afahamishwa kwanza. Pia ni kweli kwanini hakuwa katika kile chumba wakati wote tangu kazi inaanza mpaka inakwisha? Kwa mtindo huo asingehitaji taarifa kutoka kwa marafiki wa mkewe. Hivi ni kweli akina baba bado hawaruhusiwi kuingia katika chumba hicho?

Anonymous said...

Sijui lkn kwa upande wangu mimi sioni contradiction yoyote katika hii mada,kama ilivyotolewa inawezekana kabisa.
Inawezekana huyo Baba alikuwepo maeneo ya Hospital kama ilivyo'reportiwa akiweka mambo sawa,wakati wa zoezi lenyewe hasa(la mkewe kujifungua) akawa ametoka kidogo ksbb fulani hivyo kuwa mbali na maeneo yale,haijalishi ku'reportiwa kuwa alikuwepo Hospital ndo agande palepale kwenye benchi masaa yote 24 ya siku ile,hata voucher asiende kununua au kula asiende kula kwenye Mgahawa anaouamini yeye.
Sasa kwa kupokea ujumbe wa kujifungua kwa Mkewe kutoka kwa mashostito wa mke wake ndo haijakaa sawa,ndo yanaingia sasa mawazo ya Kaka Mwaipopo.