Sunday, March 28, 2010

Sala kabla kula chakula + Jumapili njema kwa wote!!

Kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu, Utubarikie Mungu wetu sisi na chakula chetu tupate nguvu ya kukutumikia vema Amina. NAWATAKIENI WOTE AMANI KATIKA JUMAPILI HII YA MATAWI NA YA 13 PIA YA MWISHO YA MWEZI HUU MACHI NA WOTE MNAPENDWA!!


15 comments:

Born 2 Suffer said...

Yani umenitamanisha mate yananitoka hapa chakula cha nyumbani hicho.

Fadhy Mtanga said...

Ahsante sana.

Bora umenikumbusha, wacha niende sokoni fasta nami mchana nile ugali samaki.

EDNA said...

Duuuuu,huo ugali na samaki umenifanya mate yanidondoke,Jumapili njema kwako pia.

Mwanasosholojia said...

Mmh,da Yasinta, sijala ugali siku nyingi!Natamani!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

niko wazaliwapo samaki japo sio mshiriki wa kitoweo hiki

acha ubaguzi Yasinta juu yawatu wa jumapili na matawi, kuna tuusiokuwa na siku maishani yaani siku zote kwetu ni sawa na zinalingana

malkiory said...

Yasinta, tueleze kama kweli uliandaa mwenyewe au ni picha uliyopiga siku uliyoenda kule Songea kwa likizo. Hapo ughaibuni unga mweupe kama huu upo kweli?

Mzee wa Changamoto said...

Mmmmmhhhhh!!!!
Ni dhambi kutamani na naamini KUTAMANISHA PIA.
Sasa jumapili hii watuambia tusali huku ukitutamanisha na li-nguna kwa samaki. Sijui tusipo-concentrate kwenye sala sababu ya taswira hiyo, dhambi zitabebwa na nani?

Mama ntilie wanajua kupika jamani, nakumbuka nilivyompeleka Yasinta kwa Mama Tatu aka-oda huo ugali na kupiga picha. Nilidhani uliipoteza. Kumbe liitunza?
Duh

PASSION4FASHION.TZ said...

Mmmm! Yasinta umenitamanisha ugali na samaki sijala siku nyingi sana,kwanini lakini?unatutamanisha vitu wengine sio rahisi kuvipata.

Jumapili njema na kwako pia.

Mija Shija Sayi said...

Yasinta..

Baraka Chibiriti said...

Safi sana hii, kabla ya kula lazima kusali, katika maadili ya kikristu.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Okey, hapo sawa!

John Mwaipopo said...

katika sala zoote naipenda hii maana ni fupi. tofauti na zile za wengine mpaka wanaanza kuombea mkulima, mvunaji, mpishi. wanaombea amani kisha chakula.

Unknown said...

Hebu nifundisheni sala nyingine ya kuombea chakula isiwe hiyo hapo juu

Anonymous said...

Hahhhahhaah

Anonymous said...

Usisahau kununua mabenda uteremshe nayo