Wednesday, March 17, 2010

Utamaduni katika baadhi ya nchi Duniani!!!!

Kwetu bila mshenga mke hupati





Asia:

Vijana hukaa na wazazi hadi anapofikia wakati wa kuoa na akisha oa au kuolewa huchagua mzazi mmoja na kuishi kwake kwa muda fulani ndipo huanza maisha.


Australia:

Mabinti huwaomba vijana wa kiume kwenda nao “outing” kwa ajili kuombwa uchumba na analipa gharama zote kama vile chakula na vinywaji.


Columbia:

Kama msichana unatoka naye kwenda kuongea kwa mara ya kwanza kawaida huambatana na rafiki yake mmoja wa kike unawajibika kuwalipia gharama zote.

Finland:

Vijana wa kiume na kike huenda kwa kundi moja kama 30 hivi lengo likiwa ni kutafuta wachumba (matching).

Latin America:
Kaka au dada yeyote atakaye muomba mwenzake kutoka naye kwa ajili ya mazungumzo ya faragha (uchumba) anawajibika kulipa gharama zote za vinywaji na chakula.

Japan:
Siku Valentine wanwake huwapa zawadi wanaume na baada ya mwezi kuna white day ambayo wanaume nao hutoa zawadi kwa wapenzi wao wa kike.

India Kaskazini:
Hakuna uchumba hadi wazazi wamkubali msichana ambaye unataka kumuoa kama wewe ni kijana wa kiume, wazazi wakikataa umeumia na kama wakikubali unaruhusiwa full speed kuoa.

Je, sehemu unayoishi wewe tamaduni za kuoana zipoje?
Au hakuna kanuni na taratibu rasmi?
Je, njia mnazotumia zinasaidia vipi kuhakikisha wachumba wanafahamiana na kujuana ili kuwa na maisha ya ndoa yenye mshikamano na si migongano

Habari hii nimeipata kutoka kwa kaka Mbilinyi :-http://mbilinyi.blogspot.com/

7 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Dada Yasinta - huna hata haja ya kwenda mbali namna hii. Hata ukiangalia katika makabila yetu ya Tanzania tofauti zilizopo kuhusu tamaduni za ndoa utashangaa. Hili ni jambo ambalo nataka ulizungumzie kwa kirefu sana katika kitabu chako.

Nitaendelea pembeni.....

Anonymous said...

Naona hujaelezea Bongo au mambo yanajulikana wazi sana, tumekua kushinda hata wazungu tunazaa kwanza kisha harusi baadae au hata saa nyingine hamna harusi tunaishi milele, makubwa haya madogo yana nafuu.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Jamani nasikia kuna kabila hapa Tz ambapo kijana akitaka kuoa lazima baba AMUONJE mkazamwana wake kama yuko fit kwa ajili ya kijana wake! sijui ni kweli ama ni uvumi tu?

Kweli mila zipo!

Da Yasinta unifanyie mpango huko Australia ama?

Anonymous said...

Anony March 17, 2010 1:48 AM: Unazungumza kwa utafiti au? Nijuavyo mimi wazungu ndio wanaongoza kuzaa bila ndoa. Wenyewe wanaamini zaidi katika kuishi as partership.. rather than marriage. Wana sababu zao za msingi kukataa ndoa.

Simon Kitururu said...

Nahisi Hii habari imeandikwa kwa kifumi mno.

Kwa mfano ASIA ni kubwa kweli na kila aina ya vikorokoro vya mila utavikuta. Kwa mfano hii aliyoandika mwandishi inaweza ikawa ni asilimia ndogo tu ya watu ambao huifuata.

Na hiyo ya FINLAND miye binafsi sijawahi kuishuhudia ingawa naweza kudai nawajua Wafini Nje ndani.


Nachojaribu kusema ni kwamba ukitaja NCHI au eneo, kumbuka kuna watu wa aina nyingi wenye mila na desturi tofautitofauti kwa hiyo kuna MILA unaweza kufikiri ni ya Wahindi kumbe uwaitao wapo tu INDIA lakini ni WAYAHUDI na wafanyacho hapo INDIA hakina tofauti na Israel.

Au jiulize unafikiri UTAMADUNI wa WATANZANIA ni UPI ukifikiria WAMASAI na WAZARAMO wote ni WATANZANIA?

watila said...

ya babu chacha ni kali
tamaduni za hapa ninapoishi hakuna kutoka na msichana kabla ya ndoa siku ya harusi ndio unachukua kwa jumla kuna tamaduni nyengine huko india mke ndiye anayetowa tunasema mahari kijana unampa mahari na mtoto wako wa kike akaishi nae milele ukiwa na watoto sita wa kike ndo wahindi hujipiga kitanzi kwa hivo wao bado mpaka leo wanaamini mtoto wa kike ni zogo katika nyumba

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii na kuwashukuruni wote mliochangia mada hii na wote waliosoma tu bila kuchangia nimejifunza na naendelea kujifunza kupitia maoni yenu. Ahsanteni.