Tuesday, March 2, 2010

Je? ulijua kuwa mwanamke wa kwanza ambaye amekuwa mke wa marais kwa nchi mbili ni Grace Machel?!!!

Grace Machel mwanamke wa kwanza,
kuolewa na marais wa nchi mbili.

Grace Machel alikuwa amefunga ndoa na Samora Machel (1933 -1986) , ambaye alikuwa rais wa Mozambique kati ya mwaka 1975-1986. Alifariki kwa ajali ya ndege tarehe 19 Octoba 1986.

Tarehe 18 Julai 1998 Grrace alifunga ndoa tena na Nelson Mandela ambaya wakati ule alikuwa rais wa Afrika ya kusini. Kwa mtindo huu, Grace amekuwa mwanamke wa kwanza ambaye ameolewa na marais wa nchi mbili.

13 comments:

Fadhy Mtanga said...

Rekodi ya kipekee. First lady wa nchi mbili tofauti. Tena moja Afrika ya Kireno (tena jirani zako hao mtani) na nyingine Afrika iliyoendelea. Huyu mama anajua kuchagua kweli. Nataka kusema yupo makini na machaguo yake. Waume wake siyo tu walikuwa marais, bali ni marais with potency.

Majaliwa said...

Ni kweli dada!Inanikumbusha ule mwimbo tuliokua tunaimba enzi za Mwalimu (wa Kapteni John Komba nadhani): "Samora angejue kama....."

John Mwaipopo said...

iko kwenye guiness book of records siku nyingi. ila anajua kuvizia mapresident.

winnie mandela ndie aliyemkaribisha 'mwizi' wake huyo kwenye familia ya mandela. samora machel alipolipuliwa kwenye ndege mpakani mwa afrika ya kusini, winnie mandela ndie alikuwa kimbelembele kumpigia simu graca na kumwambia na nanukuu 'waliomuua mumeo ndio waliomfunga mume wangu jela.' mwisho wa kunukuu. katika hali hiyo graca akawa 'family friend' hata mandela alipoachiwa huru miaka mi-4 baadae,12/2/1990 graca akawa family friend. slowly slowly mzee akaanza kuvutiwa na graca. yalipotokea ya kutokea graca akawa hamad kibindoni ....

Mija Shija Sayi said...

@MWAIPOPO je hii ndo inakamilisha ule msemo usemao KIKULACHO KI NGUONI MWAKO?

Walianza mbali, kwanza baba wa ubatizo mwishowe mume kabisa.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

walikuwa wakimuibia jamaa labda walishiriki kummaliza ili wachukue mzigo jumla.

mumyhery said...

mhu jamani!!!

chib said...

Madiba sasa ni mzee sana, sasa sijui amekwisha mdekshia nani tena, labda Robbie Mugabe sasa

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Tuseme naye ni Mwanamke wa Shoka au? Da Mija unasemaje?

Mija Shija Sayi said...

Ndo hivyo tena Masangu.

Majaliwa said...

@Chib,nahisi Mwai Kibaki manake mzee huyu wengi wanamhisi anakabinti/nyumba ndogo mahali fulani(http://news.bbc.co.uk/2/hi/7922093.stm).

Majaliwa said...

@Chib,nahisi Mwai Kibaki manake mzee huyu wengi wanamhisi anadezaini hiyo(http://news.bbc.co.uk/2/hi/7922093.stm).

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Hilo nalo NENO

Yasinta Ngonyani said...

Natamni ningekuwa kama Grace. Lol Ama kweli huyu ni mwanamke wa shoka