Saturday, March 6, 2010

Habari mchecheto!!

Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi wa kitabibu, baadhi ya kuku wa kufugwa wanaoingia sokoni wamekuzwa kwa kutumia ‘utundu’ wenye hatari wa baadhi ya wafugaji wasio waaminifu kwa kulisha mifugo hiyo dawa za ARV ambazo huwafanya kuku hao kuonekana wakubwa na wanene kwa muda mfupi.

Uchunguzi huo unakwenda mbele zaidi na kubainisha kwamba, tabia za dawa hizo ambazo ni kujenga mwili na kuimarisha kinga ya magonjwa kwa mwathirika wa Virusi vya Ukimwi, ndiyo inayompata mlaji wa kuku hao.

Inadaiwa kuwa, kuku hao wanapokula chakula kilichochanganywa na dawa hizo, huweza kutumia siku kumi na mbili hadi kumi na nne kutoka kuwa vifaranga hadi utayari wa kuingizwa kwenye soko la walaji.

Ili kukamilisha uchunguzi huo, Amani lilituma machero wake maeneo ya Kibamba, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo ndipo kwenye viwanda vya kuzalisha kuku wa ‘sampuli’ hiyo.

Kwa mujibu wa kijana mmoja ‘profesheno’ wa kutunza kuku katika moja ya nyumba maarufu kwa uzalishaji maeneo hayo, ambaye hakutaka jina lake lichorwe kwenye ‘pepa’ hii, alikiri kuwepo kwa ishu hiyo, lakini alibainisha kuwa hajui bosi wake anapochukulia vidonge hivyo vya ARV’S.

MADHARA:
Kwa mujibu wa Daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbi ambaye aliomba hifadhi ya jina lake, mtu anayependa kula kuku waliokuzwa kwa kutumia ARV na yeye huanza kunenepa kupita kawaida, lakini uzito unaweza kuwa tofauti na unene ‘boya’.

Mtabibu huyo aliongeza kuwa, watoto wengi wanaozaliwa siku hizo ambao wazazi wao wamekuwa watumiaji wazuri wa kuku, hukua haraka kiasi kwamba, mtoto wa miaka 18 huonekana kama ana miaka 27.

Aidha, alidai kuwa, wengi ambao kuku hao wamekuwa chakula chao kikuu, hufika mahali wanakuwa ‘legelege’ katika utendaji wa kazi wa kila siku tofauti na zamani huku sehemu kubwa ya chakula hicho ikiangamiza ‘pati’ ya subira na uvumilivu na mlaji kuwa na hasira.

Dalili nyingine ni mtu kuhisi muda wake wa kuchoka unakuwa mfupi akilinganisha na zamani na wakati mwingine hali ya kuhisi kusinzia humtawala hata kama anafanya kazi.

Habari hii nimeidesa mtandaoni na nimeona si vibaya kama nikiiweka hapa ili wenzangu nanyi msome..........

5 comments:

Koero Mkundi said...

UUUUWIIIII TWAFAAA!!!!!
DUH!!!!
KAAAAAZI KWELI KWELI DADA YASINTA

watila said...

dahh haponi mtu hapa ndo naona hata hawa vijana humu ndani ya nyumba wanatabia za kuku wa kufuga kumbeee!!!!!

Shein Rangers Sports Club said...

Hayo nilikuwa nayasikia mtaani nikajua mambo ya wazushi wa jiji ila kwa mpango huu naona ipo haja ya vyombo husika kuchukua hatua stahili.

Faustine said...

Kwa bahati mbaya nchini Tanzania hatuna vyombo vya kusimamia afya za walaji. Vyakula vingi tunavyokula havina viwango, vimeisha muda wa matumizi au kutokuwa na usalama unaotakiwa.

Matumizi ya madawa ya binadamu kwenye mifugo yanaweza kuleta usugu (resistance)kwa binadamu.
Kwa kuwa binadamu atakuwa anapata dozi ndogo ndogo ya madawa haya, vimelea vya magonjwa vinajenga hali ya kuzoea madawa haya na kuyafanya dawa hizi kushindwa kutibu magonjwa yanayolengwa na madawa haya.

Zinahitajika juhudi za makusudi za kudhibiti hali kabla ya Taifa halijaingia katika gharama za kubadili matibabu kwa wagonjwa wa UKIMWI.

Mdau
Faustine
drfaustine.blogspot.com

Chacha o'Wambura said...

thanks God sili nyama. Yawezekana hata kwenye samaki ukayakuta hayo....:-(