Tuesday, March 16, 2010

WALIANZA WANAWAKE NA SASA NI WANAUME!

Je? na huyu naye ni mchina au?

Kuna simulizi nyingi sana ninazipata kutoka huko nyumbani Tanzania ambazo huwa zinanishangaza sana. Awali ilikuwa ni wanawake ndio waliokuwa waathirika lakini sasa hivi na wanaume nao inasemekana wameingia katika mkumbo huo mpaka najiuliza, sababau ni nini hasa. Je ni uelewa mdogo au ndio athari za utandawazi zinawaathiri ndugu zangu?

Kuna wanawake wengi wamekuwa ni wahanga wa madawa ya Kichina ya kuongeza makalio, kiasi kwamba wengine wamepoteza maisha. Ni jambo la kushangaza kidogo kuona kwamba serikali yetu imeshindwa kusimamia na kudhibiti uingizwaji wa haya madawa ya kichina yenye athari lukuki kwa binadamu mpaka pale zinapotokea athari za wazi.

Haya, sasa mambo yamegeuka, wanaume nao wameingia kwenye mkumbo huo. Hivi karibuni kuna habari zimesambaa huko nyumbani kuwa kuna mwanaume mmoja amejikuta akiwa na maumbile ya sehemu zake za siri makubwa kupita kiasi, inasemekana hata mkewe amemkimbia. Kisa, alitumia dawa za kichina za kukuza maumbili ya wanaume.

Habari zaidi zinadai kuwa mkewe alikuwa anatoka nje ya ndoa sana na baada ya mume huyo kumuuliza mkewe sababu ta kutoka nje ya ndoa ndio akajibiwa kuwa ana maumbile madogo na ndio maana akaona akatafute dawa za kichina ili akuze maumbile yake kumridhisha mkewe. Lakini kinyume na matarajio yake, maumbile yake yakawa makubwa kupindukia, hata mkewe akamkimbia.

Kuna wakati niliwahi kuandika juu ya wanaume kununua dawa za kuongeza nguvu za kiume maarufu kama mkuyati, kama ukitaka kujikumbusha bofya hapa. Nakumbuka nilipata upinzani mkubwa kutoka kwa wanaume, lakini naamini kwa hili watakubaliana na mimi.

Kwangu mimi wale wanawake wenzangu wanaokimbilia dawa za kichina ili kuongeza makalio yao na wale wanaume wanaotumia dawa za kuongeza nguvu za kiume maarufu kama mkuyati na dawa za kichina ili kuongeza maumbile yao nawaona kama watu wasiojiamini.

Mara nyingi tunapozungumziwa matatizo katika ufanyaji wa tendo la ndoa huwa tunafikiria matatizo ya ufanyaji kazi wa viungo vyetu tunavyotumia katika kutekeleza tendo hilo. Kwa kawaida tendo la ndoa halina kanuni moja, yaani sio jambo ambalo kila mtu anaweza kulifanya kwa kufuata kanuni moja na akaridhika, inategemea kwa kiasi kikubwa kuwa mhusika analichukuliaje tendo hilo ukilinganisha na kile alichojifunza juu ya tendo hilo tangu utotoni.

Kuna wengine wanalifurahia kutegemeana na mkao wakati wa tendo hilo, wengine watasema wanalifurahia zaidi pale walifanyapo na mtu wampendaye kwa dhati, ili mradi kila mtu atakwambia sababu ya kulifurahia tendo hilo, lakini je, vipi kuhusiana na ukubwa wa maumbile ya wanaume, yanayo nafasi kubwa kiasi gani katika kuwafurahisha wenzi wao katika tendo?
Katika hilo kuna kiwango kikubwa sana cha dhana kuhusiana na ukubwa wa maumbile ya wanaume na tendo la ndoa. Dhana hii imekuzwa kwa kiasi kikubwa sana na wanaume wasiojiamini kiasi kwamba imepewa nafasi na jamii na kuonekana kama jambo la msingi sana wakati hakuna uhusiano wowote kati ya ukubwa wa maumbile na ufanisi katika tendo la ndoa. Hata baadhi ya wanawake nao wameingia katika mtego huo na kuona kama hilo ni jambo la msingi wakati swala hilo halina kanuni.

Vipi kuhusiana na swala la hamu ya tendo la ndoa nalo? Kuna dhana imejengeka kuwa wanaume ndio wenye uchu mkubwa wa kufanya tendo la ndoa ukilinganisha na wanawake, dhana ambayo ina ukweli kwa kiasi fulani ingawa sio mara zote.

Je na wale wanawake wenye uchu wa tendo la ndoa kuliko wenzi wao inakuwaje? Hapa ni vigumu swala hili kuwekwa wazi sana na wahusika kutokana na kile tulichojifunza. Jamii imetufundisha kuwa wanawake ni wa kungoja tu waombwe tendo na sio vinginevyo. Pale mwanamke napokuwa hajaridhika na tendo la ndoa na mwanaume kuonekana kukosa hamu ya kuendelea, ujumbe unakwenda kichwani kwa mwanamke ni kujiona kama vile mumewe hampendi au amepata mwanamke mwingine nje ya ndoa au wakati mwingine hujihisi kupoteza ule uzuri wake uliomfanya mumewe ampende.

Je na ukubwa wa makalio ya wanawake nao unayo nafasi kubwa kiasi gani katika kuwavutia wanaume linapokuja swala la kufanya tendo la ndoa? Hii nayo ni dhana ambayo imepewa nafasi kubwa na wanaume na kuonekana kama vile ni jambo la msingi sana, wakati yale ni maumbile ya kawaida tu ambayo hayana uhusiano wowote na ufanisi katika tendo la ndoa. Lakini kutokana na ushabiki tu wa wanaume, hasa baada ya hii mitindo ya mavazi iliyoingia ambayo huacha maumbile ya wanawake wavaao mavazi hayo nusu uchi, na ndio maana swala hilo limepewa nafasi.

Bado tunayo safari ndefu sana katika kufikia muafaka juu ya swala hili, je ukubwa wa maumbile ya wanaume na ukubwa wa makalio ya wanawake unayo nafasi kiasi gani katika kulifurahia tendo la ndoa?

Tutafakari kwa pamoja……………………..

15 comments:

chib said...

Hii balaa sasa. Mambo ya kumkosoa Mungu hayo!!!

Master Taji said...

Dada,
nikiandika sana nitaandika yaliyo ndani ya matendo yangu binafsi na bado sijawa na status yet ya kujiweka hadharani nikafaidika...
However, huyo dad kwenye picha hajaathiriwa na dawa za kichina, yupo natural kabisa na sijui ulimpata vipi...Cherokee?
Kwani hilo ndilo jina lake.
Anyway, mbona umesahau kifua?

Bennet said...

Mara nyingi tumekuwa haturidhiki na jinsi mungu alivyotuumba, tunaona kama alikosea au fulani kampendelea zaidi wakati si kweli, mambo ya urembo mara nyingi huchangiwa na wenza mfano mkorogo kama huupendi mwana mke wako hawezi kuupaka na kama unapenda makalio makubwa lazima wa kwako atumie dawa za kichina. Kwa upande mwingine nao pia kama Mamaa anatoka nje sababu kifaa chako ni kidogo lazima utatafuta dawa ya kukiongeza kiwe kikubwa
Mwisho tunahitaji ubunifu zaidi kwenye majambos ili uweze kumridhiha mwenzio kutoka nje sio dawa wala kuubadilisha mwili sio njia ya kumaliza tatizo lenu

Anonymous said...

Kama mwanaume anatakia nini kukuza matako anashida gani wasenge wenyewe hukuti wanamatako makubwa au kukuza, lakini hatuwalaumu wachina bali sisi wa tz ndio wapumbavu kila kinacholetwa tunatumia wachina wamepata pa kujaribia kila aina ya madawa tumekuwa kama wanyama wa kujaribiwa lakini kwa ridhaa yetu na ujinga tulionao, tunachekwa sana na watu wengine.

Mija Shija Sayi said...

Hivi kumbe ni kweli hizi dawa za wachina zipo, mimi nilikuwa nadhani ni uvumi tu.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Aksante kungwi.....binti na vijana wangu wakiwa tayari ku-oa/olewa ntakuita uje uwafunde manake nadhani hizi chiken pat, sendof, brazaz pat hazina maana...lol

kiukweli hii haina maana kwa kuwa aweza kuwa na ndog/fupi na bado mama/dada aka-enjoy kwa kituo

na kuhusu makalio na wengine kuongeza ukubwa wa titi ni ujinga wa wote kwa kuwa jamii imewatengeneza hivo.

kazi ipo kabisa ya kuelimisha...

Koero Mkundi said...

Kule Arusha kuna wamasai wanatembeza hizi dawa za kuongeza nguvu za kiume katika vilabu vya pombe na zinanunuliwa sana, dawa za kuongeza nguvu za kiume zina soko kubwa sana siku hizi, na wasiwasi wangu ni kule kutokuwa na uhakika na athari za dawa hizi, Je zimefanyiwa utafiti wa kutosha kama hazina athari kwa wanaume maana jinsi wanavyozifakamia inatisha!!

Utakuta mmasai anatembea na chupa kubwa la maji ya uhai la lita tano limejaa mizizi ndani iliyochanganywa na maji ambayo hata hivyo sina uhakika kama imechemshwa au ni safi na salama lakini wanaume wanaibugia midawa hiyo utadhani soda.

sasa sijui wanaume wa siku hizi wamechoka kiasi cha kupoteza ufanisi katika tendo la ndoa au ni kitu gani hasa kimewapata.

Inashangaza kidogo kuona kwamba dawa hizo zikipata umaarufu sana siku hizi tofauti na hapo mwanzo.

Hebu wanaume mtueleze hapa kulikoniiii........

Anonymous said...

Yansita mimi nakuomba unipe line nzuli yakupata hizi dawa zakukuza uume,duh mbona yakwangu inadidimia?pleazzzzzzzzz.

watila said...

unaona nilikwa mbia nimepigwa na mshangao sijuwi kama nitaweza kuchangia hapa waswahili wanasema (bumbuwazi) duhhhh

Mzee wa Changamoto said...

Mmhhhhhhhhhh
Binadamu wa sasa anapenda saana kile kiitwacho "extreme" katika kila kitu. Iwe kwenye mashindano wanajitahidi kuvunja rekodi hata kama kwa kufanya hivyo kunahatarisha maisha yao. Uliona kilichomsibu yule lugger wa Georgia katika Olimpiki? Walitengeneza track ambayp ingekuwa the fastest in the world. Baada ya kujaribu (licha ya kuwa aliwapigia wazazi akisema inatisha na alikuwa akiogopa) lakini medali na rekodi vikatangulizwa.
Ni haya haya yanayofanya hata kwenye miili na mapenzi.
Niliwahi andika kuhusu hili nilipotoa maoni kwa Kaka Matondo ambaye ameandika saana kuhusu MNYAMA-BINADAMU anayejifanya kuwa mwenye akili zaidi na kutenda ujinga zaidi. Moja ya makala ambazo zinadhihirisha kutoridhika kwa mwanadamu na ambayo nilitoa maoni kwake ni hii hapa (http://matondo.blogspot.com/2010/02/ati-hawa-wakizeeka-inakuwaje.html).
Na ni humo nilipokumbuka hadithi ya mwanamke aliyekwenda mahakamani kuomba talaka akimuomba jaji avunje ndoa yao kwa kuwa mumewe amekuwa akimlazimisha kufanya mapenzi akiwa amemfunga pingu na kamba. Yaani alikuwa akitaka MKEWE awe kama mateka wakati yeye anafanya naye mapenzi.
Nikajiuliza HIKI NI NINI?
Na mume akasema (bila aibu) kuwa amechoshwa na mtindo wa mapenzi anaopata toka kwa mkewe kila siku. Anahitaji "style" tofauti.
Kwa maana hiyo anapokataliwa mtindo huo wa kimateka anaamua kwenda kusaka "wa kulipia" mtaani.
Lakini swali ni kuwa kwanini watu wanapenda EXTREME mpaka kwenye ndoa.
Lakini watu wanasema kuhusu DAWA ZA KUONGEZA UUME NA kuongeza makalio lakini sijasoma asemaye namna ambavyo kinadada (baadhi) wamekuwa wakifanya mambo ya ajabu kwelikweli. Sijasoma kuhusu wadada wanaofanya mapenzi na wanyama na zaidi ya yote PUNDA. I MEAN PUNDA ambaye mimi nikiona "anampanda" jike (ambaye ameumbwa kuhimili jinsia ya pili ya punda wenzake) nasikia huruma lakini leo hii eti mwanadamu anataka kwenda that extreme.
KUNA MENGI YA KUSIKITISHA KUHUSU BINADAMU

Anonymous said...

Nimecheka kinoma hiyo picha na hasa mesji uliyoandika.Umefikiria nini kuandika hivyo? ila kweli kuna wanaume wameachika kisa hawawatoshelezi wake zao.Nafikiri hiyo ndo dawa.

PASSION4FASHION.TZ said...

Huyo dada nimaumbile yake,sio mchina kama alivyosema master T,za mchina ni balaa omba kusikia,Mija sio kama watu wanasema tu,ni kweli zipo na zinazidi kutesa watu,sisi binadamu ni watu wa ajabu sana,watu wanaona kabisa hizo dawa zina athali kubwa lakini wengi bado wanazitafuta kwa nguvu zote ili wazitumie.

Anonymous said...

ni upuuzi tu, wachina tunawasingizia tu. Mimi katika kuishi kwangu sijawahi kuona mchina mnene kupitiliza. sasa hao wanaotumia hizo dawa za mchina ni wao kimpango wao na tamaa zao.

@Koero, sio kwamba wanaume wa siku hizi hawana nguvu za kiume, ila pia inawezekana wanawake wa kisasa wanademand zaidi, maana kama walivyosema wachangiaji wengine kwamba kama katika pair mmoja hapendi, basi sidhani kama mwingine atahangaika kutafuta solution za kichina china.

Anonymous said...

Cherokee D'Ass - I love this woman. She is the BEST katika majambozzzz...

John Mwaipopo said...

yasinta kwarezima hii jamani...