Showing posts with label kilimo. Show all posts
Showing posts with label kilimo. Show all posts

Monday, May 26, 2014

KUULIZA SI UJINGA...NAMI LEO NINA WALI KWENU....KILIMO CHA UFUTA....KAPULYA MDADISI!!!

 Kama mjuavyo na udadisi wangu...nimejaribu kuatika UFUTA na umeota sasa swali niendelee vipi  ili kupata ufuta?
Hili si shamba langu. Ila naota kama lingekuwa langu . Kwa hiyo ndugu zangu naombeni msaada wenu ili nifanikishe ...Kaka Bennet msaaaadaaaaaa...

Thursday, September 26, 2013

NIMELAZIMIKA KUVUNA NYANYA ZANGU KWA AJILI YA BARIDI KUWAHI MAPEMA KULIKO MATARAJIO YANGU....

 Hizi ni nyanya zangu ambazo zilikuwa bado kuiva kama mnavyoona ...nimeamka leo asubuhi  nimeshikwa na butwaa nyasi zote zilikuwa nyeupe theruji  kabisa kitu ambacho zikutarajia kwa haraka hivi. Kwa hiyo imenibidi kuzivuna kabla hazijaharibika sana na kuzihifadhi. Vipi SIJUI kwa kweli..Je nikizihifadhi kwenye boxi zitaiva? Maana hapa ni nusu ya tulizokula....
Hahahaaa:-)  na nikaamua nivune tu na vitunguu vilivyobakia ...mkulima wa ajabu anaanza kula kabla hajavuna na sasa vimebaki sita (6) tu....KARIBUNI KUNISAIDIA KULA NYANYA HIZO!!!

Thursday, August 1, 2013

UTAMU WA KULIMA BUSTANI NI SASA: VIAZI VYA KULIMA KWA MIKONO YANGU MWENYEWE LEO TWALA....MLO WA JANA JIONI

 Hivi ni vile viazi angalia hapa na jana jioni ndiyo ikafikia muda wa kuangalia kama vyaweza kuliwa na matokeo yako yakawa kweli vyaweza kwa hiyo jana jioni tumekula viazi vya kulima Nangonyani.......kama
....uonavyo kwenye sahani hapa ni viazi , broccoli, nyanya kidogo, limao na samaki aina ya salmon(kiswahili ) nisaidieni ......kilikuwa kitamu mno....nawashauri wote mlio  na nafasi ya kulima bustani kulima viazi mviringo....NAWATAKIENI ALHAMIS NJEMA NA MWANZO MWEMA WA MWEZI AGOSTI:-)

Friday, September 21, 2012

TANGAZO:-NUFAIKA NA KILIMO ANZA SASA!!!

WEWE NI MKULIMA STADI? …… HUJACHELEWA ……. ANZA SASA ….
Fesh Farms (T) sasa wanasaidia uwekezaji katika kilimo cha miti ya
nguzo, karatasi na mbao. Wanauza mashamba yenye miti (ardhi pamoja na
miti); maeneo ya Mufindi-Iringa (kilomita 75 kutoka Iringa mjini). Bei
ni tsh 600,000 hadi 1,000,000 kwa ekari. Umri wa miti ni miaka 1 hadi
5. Unaweza kununua ekari kuanzia moja na kuendelea. Fresh Farms (T)
wana magari yatakayokupeleka na kukurudisha mashambani ikiwa unataka
kuyaona, kujifunza ama kununua.
Pia tunauza mashamba tupu (ardhi tupu) kwa 100,000 hadi 200,000 tu kwa
ekMashamba yote yana "documents" za umiliki na Fresh Farms (T)
itaendelea kukusaidia kutunza mashamba uliyonunua, hadi kuvuna miti
kwa gharama na utaratibu nafuu kabisa.
NB: Muda wa kuvuna miti ya mbao tangu kupandwa ni kuanzia miaka sita,
miti ya nguzo inavunwa baada ya miaka 4-5 tangu kupandwa. Miti
iliyokomaa kwa ekari moja unaweza kuvuna mbao hadi za shilingi 12M.
Wasiliana nasi kwa anuani zifuatazo
Fresh Farms (T)-Albert Sanga (Director) 0766 742414/0719 127 901
e-mail; stepwiseexpert@googlemail.com
Markus Mpangala (Advertising Officer)- 0764936655
e-mail: mwanazuoni27@gmail.com

Monday, August 6, 2012

TUANZE JUMATATU HII KIHIVI:- KILIMO....UKIITUMIA MIKONO YAKO KAMA INAVYOTAKIWA :-MATOKEO YAKE NDIYO HAYA...UTAKUWA MLO WA MCHANA WA LEO MBOGA/MAJANI YA MABOGA!!!

MBOGA YA MABOGA KWENYE UNGO...
Ni furaha ilioje kuweza kula chakula ulichopande mwenyewe, hapa ni majani ya maboga na ndiyo yatakuwa mlo wa mchana wa leo:-) Napenda kuwakaribisheni wote karibuni tujumuike..Si mnajua kulima analiama mmoja lakini walaji ni wengi.... Ndiyo nimeanza  kuitengeneza....

Monday, March 9, 2009

SHAMBA LANGU LA MAHINDI NA MIGOMBA RUHUWIKO SONGEA

Wote nadhani mnajua kuwa si muda mrefu nimerudi toka nyumbani TZ. Pia ule msimu nilikuwa kule ulikuwa ni msimo wa kilimo kwa huyo nami sikuwa nyuma nimelima shamba la mahindi kama muonanyo.