Monday, August 15, 2011

KUMBE INAWEZEKAN​A EH!!!!!

MWANAMKE mkazi wa kijiji chaIkandamoyo, wilayani hapa, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuziadimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.
Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katikaJimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo,imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miakasaba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa zakawaida.
Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mumemkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.

Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, zililifikia gazeti hili nakufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii,wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezoya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewemkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwampakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.
Wakiwa kijijini hapo mume wake aliendelea kufanya kazi ya ukulima wakati yeyemama (Veronica), pamoja na kilimo hujihusisha na upishi na uuzaji wa pombe yakienyeji ya iitwayo kayoga.

Mwanamke huyo ambaye amesema ana watoto wanne, Alfred (20), binti mwenye miaka16 (ambaye ameolewa) na wengine wawili wa kiume, mmoja akisoma darasa la sitana mdogo ana miaka saba, amesema hana shida na waume wake.

Ingawa wanandoa hao walizungumza kwa hadhari, majirani walikiri kuwa mwanamkehuyo anaishi na wanaume hao wawili kwa amani na kwamba mwanamke huyo ndiye mwenyesauti na si waume zake.

“Si siri tena sasa, tumeshawazoea, kwani wanaishi kwa amani ila yule mume mdogoanaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini anashinda kwamume mkubwa, ambapo inajulikana kijijini hapa kuwa ni nyumba kubwa. “Basi paleni mambo yote, kula na kunywa, mama huyu amewapangia zamu wanaume hao kamaafanyavyo mume mwenye wake wengi. Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona yaFirauni,” alisema mkazi mmoja kwa masharti ya jina lake kutoandikwa gazetini.Ilielezwa, kwamba wanaume hao wana akili timamu na hawatumii kilevi cha pombekama ilivyo kwa mke wao.
Hata hivyo, mume mkubwa anapewa sifa za upole tofauti na mume mdogo anayetajwakuwa mkorofi kiasi cha mara kadhaa kumchapa makofi mkewe anapomuudhi.

Majirani wanadai kwamba Mama Kaela na mumewe Paulo, walipofika kijijini hapo,walipokewa na kuishi maisha ya kawaida, lakini baadaye mama huyo alianza kuwana uhusiano wa kimapenzi na Arcado, ambaye naye alilazimika kuachana na mkewewa ndoa anayefahamika kijijini hapo kwa jina la Mama Pere.

Ilielezwa na mashuhuda hao kwamba mume mkubwa alipobaini uhusiano huo, alikujajuu, lakini mwanamke huyo inadaiwa alimweleza mumewe huyo, atake asitake lazimawataishi wawili, vinginevyo ataachana naye, ndipo mume mkubwa alipokubalikuishi na mume mwenza.
Katika maisha ya kawaida katika familia hiyo, inaelezwa kwamba katika baadhi yasiku ikitokea kuwa mama huyo amechoka kupika, mume mdogo huchukua jukumu lakupika na kumwandalia chakula na maji ya kuoga mume mkubwa.

“Lakini mara nyingi kwa mfano, ikiwa ni zamu ya mama huyo kulala kwa mumewemkubwa, basi humfulia nguo zake kisha anakwenda kwa mumewe mdogo nako anamfulianguo.

“Ndivyo wanavyoishi, nasi sasa tumewazoea ila yule mama ni mkali na ana sautipale kwake kwa wanaume wale ila tunaona kama ana wivu sana kwa huyu mdogoambaye naye pia ana wivu kwa mkewe huyo, labda anahofia kuwa mama huyo anawezakuongeza mwanamume mwingine,” anasema mmoja wa majirani hao.

Hakuna mazuri yasiyokuwa na machungu, japo familia hiyo inaelezwa kuwa naamani, mtoto wao mdogo nusura avuruge uhusiano wa wanandoa hao, baada yakuibuka mzozo wakati wa maandalizi ya ubatizo wake.

Kwa sababu anazojua mama, ingawa inafahamika kuwa wote ni watoto wa mumemkubwa, mke huyo katika hati za ubatizo aliandikisha ubini wa mtoto huyo kuwani Mlele (akimaanisha kuwa mtoto wa mume mdogo), lakini mume mkubwa aliwekapingamizi kanisani akidai yeye ndiye baba halali wa mtoto huyo.

Kwa mujibu wa mwanamke huyo, yeye na Arcado ni waumini wa madhehebu ya Katolikiwakati Paulo ni Mpentekoste. Madai ya mzozo wa uhalali wa `ubaba’ wa mtotohuyo, yalithibitishwa na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, akiwamo mwalimu wadini wa Kigango cha Kanisa Katoliki Uruira, Mashaka Abel. Walisema miaka sitailiyopita, mtoto huyo akiwa na umri wa mwaka mmoja, alifanyiwa taratibu zaubatizo, lakini ilishindikana, kutokana na wanaume hao, kila mmoja kudai ndiyebaba mzazi wa mtoto.

“Lilikuwa jambo la kustaajabisha sana, kwani familia hiyo ilifanya maandaliziyote ya sherehe ya ubatizo wa mtoto huyo, lakini siku hiyo kanisani wakati huoilikuwa ni kigango cha Katumba ambacho sasa ni Uruira, sakata lilianzia palePadri alipomwuliza mama wa mtoto huyo ubini wa mtoto naye akasema ni Mlele.

“Hapo ndipo mume mkubwa alipopinga na kudai kuwa mtoto yule si wa Arcado baliwake na yeye ndiye baba halali. Padri hakuamini, aliuliza tena na tena namajibu yakawa ni yale yale, ndipo ubatizo ukashindikana,” alisema KatekistaAbel.

Kazi ya kutafuta undani wa ndoa hiyo haikuwa rahisi kutokana na mazingira yawoga na usiri uliokusudiwa kubaki, ambapo awali mama alisema kwamba mume wakeni Paulo pekee japo siku ambayo mwandishi wa habari hizi alifika kijijini hapona baadaye nyumbani kwa wanandoa hao na kumkuta mume mdogo (Arcado akimsaidiamkewe kukoroga pombe. Awali katika utambulisho, walidai kuwa ni mtu na mdogowake na kusita kuzungumzia maisha yao ya kifamilia.
Mke wao ambaye alionekana wazi kuwa ni msemaji mkuu alifoka na kuja juu, akidaikuwa hayuko tayari kuzungumzia uhusiano wake na wanaume hao wawili, ingawaalikiri kuwa wanaishi pamoja.
"Kwa hiyo umefunga safari yote hii kutoka huko ulikotoka ili uje kwangumie Veronica … nasema sitaki kabisa mtu kuja hapa na kutaka kunivurugiampangilio wa maisha yangu, kwanza nani alikueleza hayo, wambea wakubwa haoyanawahusu nini watu hao?” alihoji.

“Mie mume wangu ni huyu Paulo basi … sasa leo umeniachia vurugu ndani ya nyumbanitapigwa na huyo mume wangu Paulo, kwani mmenishikisha ugoni?” alifoka MamaKaela. Hata hivyo, mume mkubwa alidai kuwa hatamwadhibu mkewe huyo na kwambawataendelea kuishi pamoja na mdogo wake Arcado kwa amani. Hata hivyo, akinamama wengi kijijini hapo wanalaani kitendo cha mama huyo kuishi na wanaumewawili ambapo waliomba uongozi wa Kanisa uingilie kati, ili mama huyo aweze kufungandoa na mume mmoja.
Lakini kwa upande mwingine, baadhi walimpongeza mwanamke huyo wakidai kuwakitendo hicho ni cha kijasiri kwa mwanamke, kumudu kuishi na wanaume wawili nakuwa na mamlaka juu yao.

Ndugu wa Arcado wao wanalaani kitendo cha ndugu yao kuolewa na mama huyo,wakidai kuwa walishamshauri na kumuahidi kuwa endapo ataachana na mama huyowatamwozesha mwanamke mwingine, lakini yeye Arcado, amedai kuwa yuko tayarikufa, lakini si kuachana na mama huyo, kwani ndiye ubavu wake wa maisha.

“Sasa tumebaki tunamwangalia tu huyu ndugu yetu Arcado, tumemshauri, lakinimkaidi, hatusikilizi. Basi nasi hatuna la kufanya zaidi ya kumwangalia,“alisema mmoja wa ndugu wa karibu wa Arcado. Kwa upande wake, Mwenyekiti waKijiji hicho, Florence Katobasho, alikiri kuwa mwanamke huyo anaishi kinyumbana wanaume wawili na wanaishi kwa amani kwani hajawahi kufikishiwa malalamikoyoyote kuhusu wanandoa hao.

“Ni ukweli usiopingika, kwamba Mama Kaela anaishi na wanaume hao wawili …lakini kwa kuwa sijafikishiwa malalamiko yoyote kuhusu maisha ya wanandoa hao,mimi kama kiongozi hapa sina la kufanya na siwezi kuwafukuza, kwa kweliwanaishi kwa amani, mengine ni yao,” alisema Mwenyekiti wa Kijiji.
Source: Habarileo

11 comments:

emu-three said...

Aaah haya mambo mengine ni AKILI KICHWANI MWAKO, kwani swali kubwa ni kuwa ndoa ni imani , sasa wewe unafuata imani gani, je imani yako inakuruhusu kufanya hivyo? Maana mwisho wa siku sote tutarejea kwa huyo aliyetuumba, kama unamwamini , basii kuna `yakujibu' kama humwamini, utayakuta huko huko mbivu au mbichi!

Yasinta Ngonyani said...

Mtakatifu vp...mbona umeguna?

Simon Kitururu said...

@Yasinta: Nafikiria tu sijui na mimi nikubali kuwa mme mdogo sehemusehemu?:-(

Anonymous said...

Wanawake wengi wameolewa na wanaume zaidi ya mmoja. Wanafanya siri kubwa. Huyu ameweka bayana na anawamudu, tatizo likowapi? Nani kawaambia mwanamke hana haki ya kuolewa na wanaume wawili? Vvu na ukimwi watapima. Juma Nyumayo

PASSION4FASHION.TZ said...

Hii ndio tunasema haki sawa kwa wote,hapo hakuna cha ajabu ni kawaida tu kama wanaume wanaweza,sisi tushindwe tunani?

MARKUS MPANGALA said...

hii stori inaleta ladha na fikra kweli kweli, duh! hapo kuna kutosheka kweliiiiiiiiiii

Simon Kitururu said...

Markus Mpandala umeuliza bonge la swali! Kwa kuwa siye wengine huwa mpaka tushibe ,... kipengele huwa kina hitaji mapumziko , sasa kama naye huyo mwingine anahitaji ashibe na mlafi vilevile si kipengele kinaweza kugeuka kidonda?

Ndio,...
.... kushikana shikana na mabusu yana utamu wake ila wengine hayo husababisha tutake kubenjue firigisi!:-(

ray njau said...

KWA MSINGI WA MAADILI YA NDOA FAMILIA HALI HII NI TETE NA INAACHIA
JAMII MASWALI MENGI KULIKO MAJIBU!

Anonymous said...

Lakini ni sawa hioo ni haki ya binadamu kwa nini mwanaume tu awe na haki hata mimi dada yangu ana affair na wanaume awtatu kwa wkwti mmojanini ajabu na wote wajnajuana kama wanamninihii dada yangu

Anonymous said...

Hata mimi nina affair na mke wa kaka yangu na kaka anajua hilo IS JUST A SEX, kama yule mama hatosheki na kiu anaweza hata ongeza mme wa tatu. Kazi inakuja tuu wakati siku wote wanataka uroda ndio ajitayarishe na group sex . Hongera sana huyo mama tunahitaji watanzania waliokuwa shujaa bila kuficha nafsi zao

Anonymous said...

AMERICA KUNA WANAWAKE WASOMI WENGI WAMEOLEWA NA WAUME WAWILI. NDOA MOJA ANAIFANYA AMERICA NA NYINGINE NJE YA NCHI ILI ISIWE KWENYE RECORD. WANAZAA NA WAUME WOTE WAWILI. HII SIO MPYA.