Wednesday, August 17, 2011

JUMATANO YA MARUDIO/KUMBUKUMBU..LEO NI KUMBUKUMBU YA MAMA YETU ALANA NGONYANI MIAKA SABA SASA HATUNAYE KIMWILI!!!

NI MIAKA SABA LEO TANGU UTUACHE MAMA
Hapo ni mama Alana ni huyo aliyekaa na mimi
nikimsuka mwaka 1997 kijijini Mahumbato Mbinga!!!


Ndugu zanguni leo ni ile siku ya JUMATANO ambayo ni:- kipengele cha marudio ya mada/makala, picha na matukio mbalimbali. Na leo imeangukia kuwa ni jumatano ambayo mama yetu Alana Ngonyani alituacha. Kwa hiyo nimeona iwe siku ya marudio ya mada hii au niseme kumbukumbu.
------------------------------------------------------------------------------------
Nimeamka leo nikiwa na majonzi mengi kwani hii tarehe huwa inanikumbusha sana mama. Kwani ndio ilikuwa pia JUMATANO ya tarehe 17/8/2004, ambayo alituacha kwa hiyo leo ni miaka 7. Nina mengi ya kuongea nawe mama, kuna wakati huwa nadhani upo nasi na nachukua simu na nataka kuongea nawe, nataka kuisikia sauti yako, kicheko chako pia kukuomba ushauri/mawazo. Na mwisho nabaki nikitoa machozi. Mweeh!!!.

Halafu natamani kweli kukusimulia jinsi wajukuu wako wanavyoendelea pia makuzi yao. Wao pia wanakukumbuka sana. Unakumbuka mara ya mwisho mwaka 2001, uliwapa zawadi Camilla ukamnunulia gauni na Erik shati na kaputula, bado wanavitunza mpaka leo. Na wanaviabudu mno.
Najua unanisikia huko uliko, sisi wote tunakukumbuka sana mama Ustarehe kwa Amani. SISI TULIKUPENDA LAKINI MWENYEZI MUNGU ANAKUPENDA ZAIDI. AMINA.

8 comments:

Anonymous said...

HAPA NAPENDA KUTOA POLE NA KUOMBA UDUMISHAJI WA MOYO WA UVUMILIVU KWA FAMILIA YA ALANA NGONYANI.
-----------------------------------INAKUWAJE MTU ANAPOKUFA
Moto huenda wapi unapozimika?
5 Yehova, Muumba wa ubongo anajua kinachotukia tunapokufa. Anajua ukweli na katika Neno lake, Biblia, anaeleza hali ya wafu. Biblia inafundisha hivi waziwazi: Mtu anapokufa, hayupo tena. Kifo ni kinyume cha uhai. Wafu hawaoni, hawasikii wala kufikiri. Hakuna sehemu yoyote ya mwili wetu inayoendelea kuishi baada ya mwili kufa. Hatuna nafsi au roho isiyoweza kufa.*

6 Baada ya Sulemani kutaja kwamba walio hai wanajua kwamba watakufa, aliandika hivi: “Lakini wafu, hawajui lolote kamwe.” Kisha akafafanua kweli hiyo ya msingi kwa kusema kwamba wafu hawawezi kupenda wala kuchukia na kwamba “hakuna kazi, wala utungaji wala ujuzi wala hekima katika Kaburi.” (Mhubiri 9:5, 6, 10) Maisha yetu ni kama moto. Unapozimika, hauendi popote. Haupo tena.

9 Kwa nini basi wanadamu hufa? Ili kupata jibu, lazima tuzingatie kilichotukia kulipokuwa na mwanamume na mwanamke mmoja tu duniani. Biblia inaeleza: “Yehova Mungu akachipusha katika nchi kila mti wenye kutamanika kwa macho ya mtu na ulio mwema kwa ajili ya chakula.” (Mwanzo 2:9) Hata hivyo, alikatazwa kufanya jambo moja. Yehova alimwambia Adamu hivi: “Matunda ya kila mti wa bustani unaweza kula mpaka ushibe. Lakini kuhusu matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula, utakufa hakika.” (Mwanzo 2:16, 17)
13 Yehova hakuwa na sababu ya kuwaacha Adamu na Hawa wasiomtii waendelee kuishi milele. Walikufa kama Yehova alivyokuwa amesema. Adamu na Hawa wakakoma kuwapo. Hawakuendelea kuishi mahali pengine wakiwa viumbe wa roho. Tunajua hivyo kwa sababu ya yale ambayo Yehova alimwambia Adamu baada ya kuzungumza naye kuhusu uasi wake. Mungu alisema: ‘Utarudi katika udongo, kwa kuwa ulitolewa katika huo. Kwa maana wewe ni mavumbi nawe utarudi mavumbini.’ (Mwanzo 3:19) Mungu alimuumba Adamu kutokana na mavumbi ya nchi. (Mwanzo 2:7) Kabla ya kuumbwa, Adamu hakuwapo. Kwa hiyo, Yehova aliposema kwamba Adamu angerudi mavumbini, alimaanisha kwamba Adamu hangekuwapo tena. Adamu hangekuwa na uhai kama vile mavumbi yaliyotumiwa kumuumba yasivyo na uhai.
KUNA FAIDA KUJUA UKWELI KUHUSU KIFO
15 Mambo ambayo Biblia inafundisha kuhusu hali ya wafu yanafariji. Kama ambavyo tumeona, wafu hawahisi maumivu wala uchungu. Hatuna sababu ya kuwaogopa wafu kwani hawawezi kutuumiza. Hawahitaji msaada wetu wala hawawezi kutusaidia. Hatuwezi kuzungumza nao.
19 Kujua ukweli kuhusu wafu hukulinda usidanganywe na uwongo wa dini. Pia hukusaidia kuelewa mafundisho mengine ya Biblia. Kwa mfano, unapojua kwamba watu wanapokufa hawaendi katika makao ya roho, ahadi ya uzima wa milele katika paradiso duniani inakuwa na maana zaidi kwako.
MAMBO AMBAYO BIBLIA INAFUNDISHA
Wafu hawaoni, hawasikii wala kufikiri.—Mhubiri 9:5.
Wafu wanapumzika; hawateseki.—Yohana 11:11.
Tunakufa kwa sababu tulirithi dhambi kutoka kwa Adamu.—Waroma 5:12.
------------------------------
R.Njau
Dar es salaam.

John Mwaipopo said...

hakika kama ulivyosema mwenyewe, hamko naye kimwili tu. mungu akuzidishieni moyo wa uvumilivu na ustahimilivu

Simon Kitururu said...

R.I.P Mama Alana NGONYANI!

emu-three said...

Mungu amlaze mahala pema peponi.

Rachel Siwa said...

Poleni sana wapendwa,Mungu awape uvumulivu.

Salehe Msanda said...

Pole sana Hyasinta ndio maisha, Mungu akufariji na akuimarishe Kiroho,

penina Simon said...

Mungu azidi kukutia nguvu kwa changamoto unazokabiliana nazo,
Pia nakushukuru kwa kuja kututembelea ingawa hatukutiana jicho lkn nimefarijika kupata habari kuwa ulikuwa bongo, pia nimependezewa sana na kwa unavyojiweka,
eg, pamoja na kuwa umekaa sana huko ulaya lakini pia bado unakumbuka nyumbani na ukija huku unajirahisisha kama vile bado unaishi huku, unakula vyakula vya asili, huoni taabu kujichanganya na mazingira uliyoyaacha miaka mingi wala kuyaonea kinyaa. Mungu akuzidishie huo moyo. Binafsi umenigusa sana the way you are. ingekuwa mwingine na hivyo umeolewa na mzungu yaani ingekuwa akija huku inakuwa ni shughuli( Au kwa msemo mwingine pangekuwa hapatoshi( au tungekuwa tunamkoma))

Nikutakie Maisha na shughuli njema pamoja na familia yako.

Salehe Msanda said...

Tumuombee huko aliko
na atuandalie makazi mema maana nasi tuko nyuma yake

Kazi njema