Monday, August 22, 2011

MWANABLOG YASINTA NGONYANI/KAPULYA ALIVYOKUTANA NA KAKA SAMWELI MBOGO/KAKA S!!!




Picha ya pamoja ,Yasinta/kapulya, kaka S na binti yake Yasinta dada Camilla hapa ni Rwaha (mbuyuni)



Mama Maisha na Mafanikio a.k.a Kapulya akiwa na kaka S

Kweli wahenga walisema milima haikutani bali wanadamu hukutana... Nimetoka zangu Ruhuwiko/Songea mida ya mchana mchana hivi . Giza likaingia na kituo cha kwanza kikawa Njombe..Asubuhi yake safari ikaendelea , kufika Iringa tukapumzika na kupata soda moja na bila kusahau kuchimba dawa. Mara Mnyasa nikaona Samaki nikashindwa kuvumilia nikanunua samaki wawili...Safari ikaendelea mpaka kufika Rwaaha na hapo ikawa ni muda wa kupata chochote/chakula cha mchana. Basi mnyasa huyu na binti yake wakakaa na kuanza kuwatafuna wale samaki huku wakitelemshia maji..wakati wengine waliamua kula sambusa.

Sasa ngoja nikuambia nilichotaka kusema ni kwamba wakati nakula samaki hao...mara akaja kijana/kaka mmoja. Akasimama mbele yangu nami nikawa nakereke, na nikajiuliza huyu kijana/kaka anataka nini? au anataka samaki wangu nini? kwanini anasogea sana nilipokaa na nilivyo mwoga nikaanza kuogopa. Lakini kaka huyu akawa ananisemesha utazani anaifahamu au kama vile tumeonana miaka mingiiiii iliyopita. Kila nikimtazama sipati kabisa picha yake. EEeeh, nikaona hapa kaaazi kwelikweli nikawa najiuliza ananifanananisha au?...Baadaye akajieleza kuwa yeye ni msomaji, mchangiaji na mtembeleaji mzuri sana wa Maisha na Mafanikio... Hata hivyo nikawa sipati kabisa picha yake...unajua kwa nini? yeye hana picha ndio maana sikumjua maana sikuwahi kuiona picha yake. Hakika hapo ndio niliposema kweli unaweza kujuana na mtu bila kuijua sura yake, kweli MILIMA HAIKUTANI BALI WANADAMU HUKUTANA. Na pia kusafiri kwa usafiri wako ni kuzuri unaona mengi na unakutana na usiokutana nao. Ahsante!!

8 comments:

Anonymous said...

Haya ndiyo maisha na mafanikio yake na siku hazingandi lakini zinayeyu na siku isiyo na jina Ray atakutana na Kapulya.

Anonymous said...

"SIKU HAZINGANDI LAKINI ZINAYEYUKA"

Anonymous said...

Katika,kupitia pitia hizi blog, niliwahi kupata mawazo ama kufikiri iposiku nitakutana Da Yasinta. sijuwi nikwanini. maeneo ambayo yalikuwa yakitokea katika kufikiri huko, ni katika viwanja vya ndege,hasa Uholanzi.nimekuwa nikipata picha hiyo kwa muda mrefu.nahatimaye bila kutarajia nimeweza kukutana na dada huyu . kama alivyo sema jinsi nilivyo anza kumhoji na ndivyo nimekuwa nafikiri,niajabu sana hii kitu imetokea.kwakweli safari yangu pia sikuwa nimepanga kupitia mbeya,mpaka tunafika morogoro ,kwa gari ambayo nilipewa msaada,kwa kawaida huwa tunapita Dodoma halafu ndo Tabora-Mpanda.Lakini baadaye walio nipa lifti wakasema tuna pita ya mbeya.sikupinga wala nini, japo niliona sasa shughuli za Tabora zitakuwa zimekufa,ikabidi nijipange kwakuwa hatahivyo safari yangu ilikuwa inaishia Mpanda. kumbe mambo yote hayo ni huyu binti wa kingoni ananivuta tu mpaka tukaonana.sikuamini macho,nilijisika rahaa sana ,kumkuta mdadamwenyewe mchangamfu hilo lilinipa faraja zaidi,kwani angekuwa mwingine jinsi nilivyo mvaa,(nashemejiyuko pembeni) ninge shushuliwa,lakini kwa Da Yasinta,alikuwa poa tu, kweli wewe ni 'Kapulya'.haya nisiseme sana ila nimefurahi kuku ona. KaKa S

Rachel Siwa said...

Inapendeza sana,kweli safari ilikuwa nzuri naya furaha.

Mija Shija Sayi said...

Heeeee!! Kaka Sam, jamani nimefurahi sana tu kuiona picha yako na Yasinta, aisee milima haikutani..

Vipi kwani umerudi?

@Yasinta..Jamani mwenzetu uliinjoi likizo hii..

Anonymous said...

Da mija, nimerudi nduguyangu.Bongo safi tu nijinsi unavyo taka wewe mwenyewe kula likizoyako.lakini ukienda mikoani(nyumabani kabisa) unafaidisana hakuna mikimikiki kama dar .Tuwasiliane basi.
Kaka S.

emu-three said...

Kwa vile ilikuwa safari yenye mambo mengii ya kifamilia, lakini ulipofik hapa bongo, ungelikutana na wanablog wengi ambao wapo hapa Dar, lakini wakati mwingine ikiwezekana! Ni wazo tu

Anonymous said...

Nikwelikabisa unayo sema ,emu-three,natamani sana kuonana nao hao wana blog,nimuhimu sana.safari nyingine tukijaaliwa, mwakani nitafanya hivyo.unajuwa inapendeza sana mnapo onana usokwa uso. nitalifanyia kazi wazo lako

Kaka S.