Sunday, August 14, 2011

JUMAPILI YA LEO:- IMANI IMEKWISHA/ KWENYE KIFO HAMNA KUJUANA, UNAMKANA HATA MUUMBA WAKO!

Nimeamka nikaona ngoja nifunguo kopo langu na kusoma barua pepe na mara nakutana na ujumbe huu kwa vile sina tabia ya kuwanyima ninyi ndugu zangu chochote nimeona niweke hapa ili wote tupate kuelimika. ujumbe wenyewe ni hivi....Karibuni.

Jamaa mmoja alikwenda msikitini na panga mkononi na kuwauliza waumini: "Nani muislamu kati yenu?"
Watu kimyaa! Akauliza tena kimyaa!! Akamfuata mmoja akamchukua akaenda nae nyumbani kwake akampa mbuzi wake amchinjie.

Kabla ya kumchuna akarudi tena msiktini na kisu chenye damu na kuwauliza tena waumin: "Ni nani muislamu?" wote kimya kwa woga.
Kwa mshangao akawauliza kwa SAUTI kubwa: "Yaani nyie mpo ndani ya msikiti halafu hamumjui Muislamu?"

......Ghafla wote huku wakitetemeka wakasema IMAMU wetu ndie muislamu.


IMAMU kusikia anatajwa akalalamika: "Jamani....jamani! yaani kuwaswalisha siku mbili tu ndo nshakuwa Mwisilamu? Muogopeni Mungu!!"

Kumbe yule jamaa lengo lake lilikuwa kuchinjiwa na kuchuniwa mbuzi wake!

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!!


5 comments:

Mija Shija Sayi said...

Duuh!!..Nimecheka sana, ila ni fundisho kubwa kwetu sote..

Christian Sikapundwa said...

Ama kweli kifo kinaogopwa sana,wale ni waislamu kweli hofu yao ni lile panga halafu tena kisu chenye damu,maana walijua kuwa yule aliye mchukuaalimchinja na kisu kile na pale alifika kuwaonyesha alivyo kuwa mkatili.

Yumkini wangalijua kuwa wanatakiwa kuchinja mbuzi na kumchuna wasinge sita kusema kuwa wao ni waislamu.Tunashukuru kwa kali uliyotuletea leo.

Anonymous said...

namimi ni kaswali langu hapa hivi ni kwanini nia waislam tu wanaruhusiwa kuchinja?

emu-three said...

Hicho kichekesho kuna hoja nje ya pazia, na huenda nia kubwa ni kuzua mjadala wa kiimani(kwanini kuchinja)....au huenda ilikuwa changamoto ya kupima imani za watu. Kwa wenye imani ya dini wanajua vipi hali kama hiyo ikitokee kifanyike nini...inaitwa `dharura'...ikiisha unatubu ...
Dini haina ugumu yakhe, haihitaji mtu kuumia, ila kwa wale wenye kuijua na kuiamnini!

Anonymous said...

Sio waislamu tu wanaoruhusiwa kuchinja, hata wayahudi na manasara (kama bado wapo) nao wanaruhusiwa kuchinja kwa kufuata masharti yaliyowekwa kuhusu kuchinja.

Sharti la kwanza kuchinja huko kuwe ni lazima kwa ajili ya muumba wako sio kuchinja kwa ajili ya mizimu na mauza uza mengine ndio maana wakati wa kuchinja unatakiwa ulitamke jina la Mungu, na sio mitume au viumbe wake alowaumba.

Pili kuchinja huko lazima kufuate taratibu inayopelekea mnyama aliyechinjwa kutoa damu yote nje ili damu isibaki kwa mnyama ikaleta madhara kwa mlaji. Yaani damu yote inatakiwa iwe drained wakati wa kuchinja.

Uchinjaji uwe wa haraka sana kwa kisu kikali ili kusiwe na mateso kwa mnyama.

Wengine wataongezea hayo ni baadhi tu ya masharti ya uchinjaji. Na nyama ilichinjwa na myahudi huitwa kosher meat na muislamu anaweza kuila hiyo. Ya manasara hawa kwa sasa sidhani wapo kama wapo ni wachache na wa siku hizi akitaka kuchinja atataja jina la Mungu yupi? Ndio maana waislamu hawali nyama ilichinjwa na manasara wa sasa kwa sababu haitimizi masharti ya uchinjaji.