Wednesday, May 2, 2012

KISWAHILI CHETU NA MATUMIZI YA HERUFI!!!!

NIMEIPENDA HII NIMEONA TUENDELE NA HII JUMATANO  YA MARUDIO KIHIVI.....KARIBUNI!!!!

Usahihi ni: Hapauzwi. Utatapeliwa.
Lipo tatizo kubwa kwa baadhi ya watu wa makabila fulani nchini Tanzania kuhusiana na matumizi ya herufi, 'R' na 'L' au 'H' na 'U' katika matamshi na hata kwenye maandishi. Pia, wapo wale ambao hushindwa kutofautisha kati ya herufi 'S' na 'Z' au 'P' na 'B' ama 'V' na 'F' na 'DH' na 'Z' na kadhalika.

Ingawaje kwa maneno mengine huwa si rahisi kupoteza maana kusudiwa, makosa hayo bado huweza kuleta maana tofauti kabisa na iliyokusudiwa, hasa kwa mgeni au mwanafunzi wa lugha ya Kiswahili.

Kwa mfano, neno 'ukiri' ni tofauti na neno 'ukili' au 'karamu' na 'kalamu'. Vile vile 'kazi' ni tofauti na 'kasi' kama ilivyo 'vuma' ikawa tofauti na 'fuma'. Kadhalika, 'barua' ni tofauti na 'parua' ama 'dhana' na 'zana'.

Matumizi yasiyo sahihi ya maneno hayo humlazimisha msomaji kujua maudhui ya habari kwanza ili kuweza kupata maana kusudiwa. Hii si vyema kwa wageni wanaojifunza lugha tunayojisifia kwayo kuwa ni asili yetu.
Chanzo toka wavuti.
OH! NIMEKUMBUKA  PIA BAADHI YA MAJINA YA MIJI KAMA VILI LILONDO WENGI WANASEMA RIRONDO, PIA RUHUWIKO  WENGI WANASEMA LUHUWIKO NK.

9 comments:

batamwa said...

ndio yasinta nikweli watu wengi wanayakosea hayo maneno aidha kwasababu ya ulimi wa mama au wengine kwakutokuwa makini kama sasahivyo ilivyo kusikiliza radio hizi zilizoanzishwa ndio ziko mstari wa mbele kuharibu lugha.mfano:nyimbo hii badala ya wimbohuu,mapungufu badala ya upungufu,jumbe nyingi badala ya ujumbe mwingi namengine na mengine hivyo inabidi tujirekebishe ilikusudi lugha yetu ipendeze

Ester Ulaya said...

karibu inakuwa kalibu, kuna baadhi ya maneno yanatamkwa kiutata kabisa

ray njau said...

Shikamoo mwalimu Yasinta.
Wengi wetu Kiswahili ni lugha ya pili tukiwa na athari za lugha zetu za [mama] awali.Mimi hapa naweza kuandika nchi lakini nitasoama 'nji' hii.Jambo kuu hapa ni kila mdau kutambua udhaifu wake na kuzingatia usanifu wa lugha wakati wa kuandika.
------------------------------------
"Media nyingi zimeendelea kutumia neno kupelekea badala ya kusababisha."
-----------------------------------

Yasinta Ngonyani said...

swali la kizushi! je inamaana walimu wetu wa kiswahili hawana elimu ya kutosha ya kiswahili? Maana mtu hata kama una lugha mbili yaani lugha zetu za asili ukifundishwa unaweza kumudu. Kwa kweli hii mara nyingi nimewaza ni kama kuharibu lugha sasa. Au wengine wanadfanya makusudi "KUIGA" wageni?
utasikia mtu anasema "wewe acha fanya hifi" badala ya "wewe acha kufanya hivi" lugha inapotea au nisemi inaibiwa sijui?

Anonymous said...

Yasinta,

Kwenye lugha kuna makosa ya aina mbili, matamshi na uandishi. Mara nyingi walimu wengi hutia mkazo kwenye uandishi kwa kuwa wanajua athari za lugha ya asili ni ngumu kuzirekebisha. Ni sawa na ndugu zetu Nigeria BRODA anamaanisha BROTHER. Unaweza kumkuta ni Prof. wa Language lakini anatamka BRODA.

Sasa hivi limekuja wimbi jipya la makosa ya uandishi. Ukiwa yahoo messenger, unashangaa msg inaingia "HUPO?" akimaanisha kuuliza "upo?" Na huyo anayeandika hivyo amemaliza F6 au ana degree kabisa. Hilo ndio linaloniogopesha. Ukweli unabaki kuwa kiwango cha elimu kinazidi kushuka siku hadi siku, ama walimu ni wachache au walimu hawafundishi ipasavyo.

Ukiona hata kiswahili inakuwa mgogoro, maana yake ni kwamba hata wakisema kitumike kufundisha kuanzia chekechea mpaka PhD, bado tutaendelea kuwa na matatizo na tena makubwa sana.

ISSACK CHE JIAH said...

Du dada hiyo unawataka ndugu zako wale wanyamwezi uwakasirishe maana hao ndiyo hawajuwi kutamka vizuri utagombana na mbogo haya bwana wee
lakini Rachel humwambii kitu kwa wasukuma na wanyamwezi mi nimeshakula mahari ya ng'ombe
kwaheri
CHE Jiah

ray njau said...

KARIBUNI NYOTE katika tovuti rasmi ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA). Baraza la Kiswahili la Taifa liliundwa chini ya sheria namba 27 ya Bunge ya mwaka 1967. Kimsingi, BAKITA ndiyo inayofanya kazi ya kuratibu na kusimamia shughuli zote za kukuza, kuendeleza na kueneza Kiswahili nchini. » Soma zaidi...
BAKITA kuwa taasisi yenye nguvu kisheria, kifedha na inayotambulika kitaifa na kimataifa katika kuratibu, kusimamia na kukuza maendeleo ya lugha ya kiswahili. Kukubalika kwa matumizi ya Kiswahili katika Umoja wa Afrika (UA) na mafanikio ambayo lugha hii inayapata, vinatupa tumaini na imani kwamba kile tunachokiamini na ambacho tumekuwa tunakiamini siku zote kuwa Kiswahili kitakubalika duniani kote sasa taratibu kinaelekea kuwa kweli na kwa hakika zaidi.
Kukuza, kustawisha na kuhimiza matumizi ya Kiswahili fasaha ndani na nje ya nchi kwa ushirikiano na wadau wengine.
Viunganishi Vingine

Wizara ya HVUM
TATAKI
BASATA
BAMVITA
MCT

Habari Mbalimbali

Maonyesho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara:-
DSM
Butiama
Matukio katika picha

Matangazo

Hakimiliki © 2012, BAKITA. Haki zote zimehifadhiwa

Mbele said...

Lakini namshukuru huyu jamaa kwa kututahadharisha, tusije tukaingizwa mjini.

obat vimax said...

vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg