Saturday, May 12, 2012

RUDI NYUMBANI AFRIKA/TUSISAHAU TULIKOTOKA!!Mmmhh nimepata hamu kweli kweli hapa ya kula vyakula hivi  mpaka naanza kufikiria kuwa ...naacha  bwana  labda ntasema siku nyingine. Je? nawe umepata hamu kidogo? ngoja Baba gaston amalizi na RUDI NYUMBANI AFRIKA!!!!
JUMAMOZI NJEMA. NYUMBANI NI NYUMBANI TUSISAHAU TULIKOTOKA.!!!!

14 comments:

Mija Shija Sayi said...

Yaani balaa tupu.... Aisee waafrika tunajua kupika.. Nimevitamani kweli vyakula hivi Yasinta.

ray njau said...

Mwanamke mapishi dada zangu!!
-------------------------------
Methali 31:10-31

1 Maneno ya Lemueli mfalme, ujumbe mzito ambao mama yake alimwambia ili kumrekebisha:

2 Niseme nini, ewe mwanangu, niseme nini, ewe mwana wa tumbo langu, niseme nini, ewe mwana wa nadhiri zangu?

3 Usiwape wanawake nguvu zako za uhai, wala njia zako kwa kitu ambacho hufanya wafalme wafutiliwe mbali.

4 Haifai wafalme, ewe Lemueli, haifai wafalme kunywa divai wala maofisa wakuu kuuliza: “Kileo kiko wapi?” 5 ili mtu asinywe na kusahau jambo lililoagizwa na kupotosha haki ya yeyote wa wana wa mateso. 6 Mpeni kileo mtu yeyote anayekaribia kuangamia na kuwapa divai watu wenye uchungu katika nafsi. 7 Acheni mtu anywe na kuusahau umaskini wake, na mtu asiikumbuke taabu yake tena.

8 Fungua kinywa chako kwa ajili ya mtu asiyeweza kusema, ili kutetea watu wote wanaopitilia mbali. 9 Fungua kinywa chako, hukumu kwa uadilifu na kutetea mtu mwenye kuteseka na maskini.

10 Mke mwenye uwezo, ni nani anayeweza kumpata? Thamani yake inapita sana ile ya marijani.

11 Moyo wa mume wake umemtegemea, wala hakuna faida inayokosekana.

12 Amemthawabisha mume wake kwa mema, wala si kwa mabaya, siku zote za maisha yake.

13 Ametafuta sufu na kitani, naye hufanya kazi yoyote inayopendeza mikono yake.

14 Amekuwa kama meli za mfanyabiashara. Huleta chakula chake kutoka mbali.

15 Tena huamka kabla usiku haujaisha, na kuwapa watu wa nyumbani mwake chakula na kuwapa vijana wake wa kike fungu lao lililoamriwa.

16 Amefikiria shamba, akalinunua; amepanda shamba la mizabibu kutokana na matunda ya mikono yake.

17 Amejifunga nguvu viunoni, naye ameitia nguvu mikono yake.

18 Ametambua kwamba biashara yake ni nzuri; taa yake haizimiki usiku.

19 Amenyoosha mikono yake kushika kijiti cha kusokotea uzi, nayo mikono yake mwenyewe imeshika gurudumu la kusokota nyuzi.

20 Amewanyooshea mkono wenye kuteseka, na mikono yake amemkunjulia maskini.

21 Hana wasiwasi juu ya watu wa nyumbani mwake kwa sababu ya theluji, kwa maana watu wote wa nyumbani mwake wamevaa mavazi mawili.

22 Amejitengenezea matandiko yenye mapambo. Mavazi yake ni ya kitani na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau.

23 Mume wake ni mtu anayejulikana malangoni, anapoketi pamoja na wanaume wazee wa nchi.

24 Hata ametengeneza mavazi ya ndani na kuyauza, nao wafanya-biashara amewapa mishipi.

25 Nguvu na fahari ndiyo mavazi yake, naye anaucheka wakati ujao.

26 Hufungua kinywa chake kwa hekima, na sheria ya fadhili zenye upendo ziko katika ulimi wake.

27 Anaangalia shughuli za nyumba yake, wala hali mkate wa uvivu.

28 Wanawe wamesimama na kumtangaza kuwa mwenye furaha, mume wake husimama, naye humsifu.

29 Kuna binti wengi ambao wameonyesha uwezo, lakini wewe—wewe umewapita hao wote.

30 Uvutio unaweza kudanganya, nayo sura yenye kupendeza inaweza kuwa ubatili; lakini mwanamke anayemwogopa Yehova ndiye anayejiletea sifa.

31 Mpeni baadhi ya matunda ya mikono yake, nazo kazi zake na zimsifu malangoni.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

ugali, maharagwe na mboga za majani jameni.....udeleli umenijaa kumudomo!

Mija Shija Sayi said...

Pastor wangu Ray Njau unanifurahisha sana..

Sifa zote zimrudie yeye..

ray njau said...

@Mija
=============
KIELELEZO KWA WAKE

10 Familia ni kama shirika, na ili lifanye kazi vizuri, linahitaji kuwa na kichwa. Hata Yesu anajitiisha kwa Yule aliye Kichwa chake. “Kichwa cha Kristo ni Mungu” kama vile “kichwa cha mwanamke ni mwanamume.” (1 Wakorintho 11:3) Kujitiisha kwa Yesu chini ya ukichwa wa Mungu ni mfano mzuri kwa kuwa sote tuna kichwa ambaye tunapaswa kujitiisha kwake.

11 Wanaume wasio wakamilifu hufanya makosa na mara nyingi wao hupungukiwa katika jukumu lao la kuwa vichwa vya familia. Kwa hiyo, mke anapaswa kufanya nini? Hapaswi kudharau mambo ambayo mume wake anafanya au kujaribu kumnyang’anya ukichwa. Mke anapaswa kukumbuka kwamba roho ya utulivu na upole ina thamani kubwa machoni pa Mungu. (1 Petro 3:4) Akiwa na roho hiyo, itakuwa rahisi kwake kuonyesha utii wa kimungu hata katika hali ngumu. Isitoshe, Biblia inasema: “Mke anapaswa kumheshimu sana mume wake.” (Waefeso 5:33) Lakini vipi akikataa kujitiisha chini ya Kristo akiwa Kichwa chake? Biblia inawasihi wake hivi: “Jitiisheni kwa waume zenu wenyewe, ili, ikiwa wowote si watiifu kwa lile neno, wavutwe bila neno kupitia mwenendo wa wake zao, kwa sababu wamekwisha kushuhudia kwa macho mwenendo wenu ulio safi kiadili pamoja na heshima kubwa.”—1 Petro 3:1, 2.

Sara aliwawekea wake mfano gani mzuri?
Sara akizungumza na Abrahamu

12 Mume awe ni mwamini au la, mke hatakuwa akimvunjia heshima ikiwa ataeleza maoni yake kwa njia ya busara hata kama yanatofautiana na ya mume. Huenda maoni yake yakawa sawa, na yanaweza kufaidi familia nzima ikiwa mume atamsikiliza. Ingawa Abrahamu hakukubaliana na mke wake Sara alipopendekeza jinsi ya kutatua tatizo fulani la familia, Mungu alimwambia: “Sikiliza sauti yake.” (Mwanzo 21:9-12) Bila shaka, mume anapofanya uamuzi ambao haupingani na sheria ya Mungu, mke wake anapaswa kuonyesha anajitiisha kwake kwa kuunga mkono uamuzi huo.—Matendo 5:29; Waefeso 5:24.

13 Mke anaweza kutimiza jukumu lake kwa kutunza familia. Kwa mfano, Biblia inaonyesha kwamba wanawake ambao wameolewa wanapaswa ‘kuwapenda waume zao, kuwapenda watoto wao, kuwa na utimamu wa akili, safi kiadili, wafanyakazi nyumbani, wema, wakijitiisha kwa waume zao wenyewe.’ (Tito 2:4, 5) Mke ambaye pia ni mama anayefanya hivyo, atapendwa na kuheshimiwa daima na familia yake. (Methali 31:10, 28) Lakini kwa kuwa ndoa ni muungano wa watu wasio wakamilifu, huenda hali fulani wasizoweza kuvumilia zikawafanya watengane au kutalikiana. Biblia inaruhusu kutengana hali fulani zinapotokea. Hata hivyo, kutengana hakupaswi kuchukuliwa kivivi hivi tu, kwa kuwa Biblia inashauri: “Mke hapaswi kuondoka kwa mume wake; . . . na mume hapaswi kumwacha mke wake.” (1 Wakorintho 7:10, 11) Msingi pekee wa Kimaandiko wa talaka ni uasherati.—Mathayo 19:9.

sam mbogo said...

turudi nyumbani.asante kwa ushauri.ukiyangalia maisha,ni kama safari ambayo kwa hakika unapita njia mbalimbali zenye mengi majaribu,furaha na hata huzuni/huthuni.ukiambiwa leo hii dada yasinta uchole ramani au njia yamaisha yako uliyopitia mpaka sasa ulipo, nakuambiwa uielezee hiyo safari kulingana na mchoro wako hakika itakuwa ni fundisho,funzo,ufahamu mkubwa katika maisha yako.pia katika kujaribu kukumbuka kila njia uliyo pita utajikuta sehemu nyingine unajishangaa umepitaje na hatimaye kuwa hapo ulipo sasa.kusafiri ni maarifa au nikupata maarifa irimradi tu safari yako hukukurupuka,hukukimbia,hukuchoswa ukimsikili mwana muziki baba Gasto ,bila kumsahau marehemu Remi ongala uamuzi wa kurudi nyumbani bado uko mikononi mwako binafsi ,pia usisahau maisha ndo hayo unayo ishi sasa hapo ulipo utajikuta siku zina yoyoma ukifikiria bado kuna maisha mengine ukirudi Tanzania/Afrika.kaka s

Rachel siwa Isaac said...

Mamama weeee dadake unauaa njaaa uwiii!!asante kwa tam tam hizi,Narudi nyumbani eeehhhh!!!

Ester Ulaya said...

CHAKULA CHA KIAFRICA KIATAMU SANA, YAANI HIZI PICHA MIE MATE KUNIJAA

Mtani said...

@Da Mija,

Usiseme waafrika, sema wa-Tanzania. Vyakula vingi vya ki-Tanzania huwa ni vitamu sana na wanajua kutumia viungo vingi na hivyo kuifanya ladha ya chakula iwe nzuri zaidi na pia chakula huvutia kwa macho.

Nimeishajaribu kula vya nchi zifuatazo kwenye nchi zao, sikuvipenda hata kidogo. Nikianzia kwa majirani zetu wa Kenya (wali huwa hauna ladha kabisaaaa labda Mombasa ambako sijawahifika). Rwanda na Uganda, hakuna kitu.

Kusini mwa Tanzania, Malawi ni zero, niliishia kushindia chips. Zimbabwe na Namibia sikuona mfano wa kupigiwa. Nilifurahia nyama choma yao tu, lakini vyakula vingine ni noma.

Nigeria na Ghana, huko kwa kweli hata kuelezea ni ngumu. Nigeria wanaweka pilipili utadhani ni mashindano. Akina mimi ukianza kula chakula chao lazima uwe na glass ya maji pembeni ili kupooza ukali wa pilipili kichaa.

Inawezekana ni kiwi cha macho, kwamba ninafagilia vyakula vya nyumbani ama kwa kuwa vimenikuza au nimevizowea. Kwa wengine ladha ya chakula inaweza kuwa uchachu wa viungo na wengine ukali pilipili. Lakini dada/mama zetu wa ki-Tanzania wanajua ku-balance vipimo kiasi kwamba ukipewa chakula utafurahia.

Big up to all Tanzanian Women na hasa wanaojua kupika ... ninawafagilia!

Yasinta Ngonyani said...

Kusema kweli chakula ulichokuli/kilichokukuza huwezi kukisahau hata siku moja. Na wala huwezi kusema nimesahau upikaji wake sidhani. Mtani hapo umesema ni lazima uwe na glasi ya maji kwa kuzimua ukali wa pilipili..hapao umekosea ni kwamba kama pilipili ni kali ukinywa maji ndio inazidi dawa yake ni kula tonge ya ugali, wali au kama una mkate iala si maji.

Mtani said...

@Yasinta
Asante kwa huo utaalam wa kupambana na pilipili. Agiza basi dagaa wa Ziwa Nyasa na unga wa muhogo, nime-miss sana.

Yasinta Ngonyani said...

Hakuna taabu ni kujulishana tu Mtani..kuhusu ugali/unga wa muhogo na dagaa Nyasa wala usikonde sitaki wa kuagiza nakwenda mwenyewe na ntakugawia.

Penina Simon said...

Umenitamanisha sjui nile kipi leo? maanake vyote naona vitamu sana tu

nyahbingi worrior. said...

Inapendeza sana.