Wednesday, May 30, 2012

TUMALIZIE SIKU HII HUKO WILAYA MPYA YA NYASA KWA MLO HUU!!!

Ndugu msomaji wa mtandao huu umesikia kuwa hivi sasa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kaanzisha wilaya mpya ya Nyasa sasa ufikapo wilaya hiyo chakula kikuu ni ugali wa Mhogo na Samaki kama unavyo ona hapo juu samaki alioko juu ya ugali anaitwa Mbufu
picha na maelezo hapa.
------------------------------------------------------------------------------------------------------Baada ya kusoma hapoa yaani jioni hii nimetamani kweli mlo huu. Huu ndio mlo ulionifanya niwe na afya hii niliyonayo leo. Mbufu ni samaki mtamu sana mwaka 2007 nilipokuwa Mbambab bay nilimla ila mwaka jana nilipokuwa Matema beach nilimkosa. Nikaona nisitamani tu ngoja niichukue picha hii ili iwe karibu nami. 
JIONI NJEMA KWA WOTE...

4 comments:

Mija Shija Sayi said...

Hivi ni vigezo gani hutumika kuunda wilaya au mkoa?

Asante kwa msosi Yasinta.

batamwa said...

huo msosi ni babkubwa hasa mpaka njaa inauma sasa!!!

Ester Ulaya said...

kila nikiangalia njaa yauma, mtamu kwa macho, je kwa kula live?

Da'Mija huwa wanaangalia wingi wa watu na maendeleo hivi ni vigezo vichache nivifahamuvyo

ray njau said...

Hakika huu ni ukarimu maridhawa!