Thursday, May 24, 2012

JE? UMEKISIKIA KILIO CHA UPUNGUFU WA MADAWATI NCHINI TANZANIA?


Elimu ndiyo msingi wa maisha na kila mwenye elimu ni mwenye hazina na daraja la kumfikisha kwenye mji wa kufikirika wenye jina la maisha na mafanikio.
Mazingira rafiki ndiyo nyenzo muhimu kwa yeyote anayepewa elimu  kwa malengo ya manufaa ya sasa na  wakati ujao.
Miundombinu  katika shule za  msing nchini Tanzania  haikidhi mahitaji halisi na ile ya zamani inazidi kuchakaa.
Kilio cha upungufu wa madawati katika shule za msingi sasa ni wimbo kutoka kaskazini kwenda kusini na magharibi kwenda mashariki.
Madarasa yaliyopo ni machache na baadhi yake hayakujengwa katika kiwango na hadhi husika.
Nchi imejaa misitu na miti yenye miti ya mbao lakini bado kilio cha upungufu wa madawati kinazidi kulitawala anga la Tanzania.
Hakuna sababu yakuendelea kulia na jambo kuu hapa ni jamii kukusanya mawazo pamoja na  kusema sasa inatosha.
Taasisi  za kijamii zina wajibu wa kukusanya nguvu za pamoja na kubuni mpango wenye tija katika hii changamoto ya kitaifa chini ya uratibu wa SIDO na VETA.

5 comments:

emu-three said...

HIVI KWELI MWENYE SHIBE ATAMJUA MWENYE NJAA? Watoto wetu wansoma intenational school, tuna shida gani...mmh,tunasahau kuwa ukiwa kiongozi utauliza hata mbuzi aliyepenya na kula shamba la jirani ya mwenzake,

ray njau said...

@Yasinta,
Asante kwa kukumbuka nyumbani kwa kilio cha upungufu madawati katika shule/skuli za Tanzania.
Hii tatizo halijapata nafasi katika vipa umbele vya kijamii.Jamii yetu inazidi kufanya mengi na ushahidi wa jambo hilo mabadiliko katika miji na majiji yetu jinsi kila siku vikwaruza anga vinavyozidi kuoteshwa katika mitaa mbalimbali.Uwezo,sababu ipo lakini nia imekosekana.Makampuni yetu ya viselula kila siku yanabuni promosheni za kuongeza salio uondoke na debe la mbaazi lakini hakuna anayesema ongeza salio ili ununue dawati.Kama kawaida mwenye msiba huanza kulia mwenyewe na kila mwenye kulia hushika kichwa cha mwenyewe.Tanzania bila kilio cha upungufu wa madawati inawezekana.KWA PAMOJA TUNAWEZA!!

Ester Ulaya said...

Bado juhudi zina sua sua, siku hizi kila unapomuandikisha mwanafunzi inabidi umpe na mchango wa dawati, lakini bado mashuleni hakuna madawati, tuna changamoto kubwa sana kuhusu hili

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii na kuwashukuru waote mliopita hapa hata kama hamjaacha yenu maneno ya moyoni na pia nawashukuru mliopita hapa hapa na kuungana nami kwa kuacha yenu ya moyoni...ruksa kuendelea na mjadala....

ray njau said...

Mjadala huu ni muhimu sana kwetu wadau wa kibarazani.Nahisi tunapaswa kufanya mabadiliko kwa kuacha hisia hasi katika kubagua mada za kuchangia.Hizi mada zinazogusa jamii ndizo zinazohitaji uhamasishaji wetu katika hali mali.Kamwe hatutendi haki kuibuka kwa wingi kwenye mada-vichekesho na kujificha kwenye mada za jamii na maendeleo.Iwapo tunatosa sisi wadau hapa kibarazani tunazikimbia hizi mada muhimu kijamii tunataka kumwambia nini Yasinta?Dada yetu ameamua kuitumikia jamii yake kwa moyo wa kupenda lakini hakuna mrejesho hata wa neno moja la wonyesho wa kujali.Je hapa tunajengana au tunabomoana mioyo?Upendo wetu kwa watoto wetu na jamii yetu uko wapi?Au kwa vile huko akademia hakuna changamoto hii.Kuchangia maendeleo ya kijamii ni jukumu la Jamhuri na serikali yake na sisi tuendelee kuteketeza mabilioni kwenye tafrija za kifamilia kila wikiendi.Maradhi ya ya kushindwa kuchagua kuchagua vipaumbele sahihi vya kuchangia katika maendeleo ya kijamii kuanzia kwenye kaya zetu hadi taifa yatakwisha lini?Ikiwa wenzetu wanaweza sisi tumejikwaa wapi Yasinta na wadau wote wa kibarazani?Nanikawadaganya kukaa kimya ni mtaji?