Huu ni ujumbe ndani ujumbe ndani ya wikiendi maridhawa.Hii zawadi ya wikiendi kwa wadau wa kibarazani na hitimisho dhahiri la upendo katika mchakato wa maisha na mafanikio. ----------------------------------- Wimbo wa Sulemani 8:1-14
1 “Laiti ungekuwa kama ndugu yangu, ukinyonya maziwa ya mama yangu! Ningekukuta nje, ningekubusu. Watu hawangenidharau mimi. 2 Ningekuongoza, ningekuleta ndani ya nyumba ya mama yangu, aliyekuwa akinifundisha. Ningekupa kinywaji cha divai iliyotiwa vikolezo, maji safi ya makomamanga. 3 Mkono wake wa kushoto ungekuwa chini ya kichwa changu; nao mkono wake wa kuume ungenikumbatia.
4 “Nimewaapisha ninyi, enyi binti za Yerusalemu kwamba msijaribu kuamsha au kuwasha upendo ndani yangu mpaka wenyewe utake.”
5 “Mwanamke huyu ni nani, anayepanda kutoka nyikani, akimwegemea mpenzi wake?”
“Chini ya mtofaa nilikuamsha. Hapo mama yako alikuwa na uchungu wa kukuzaa. Hapo yeye aliyekuwa akikuzaa alipata uchungu.
6 “Nitie kama muhuri juu ya moyo wako, kama muhuri juu ya mkono wako; kwa maana upendo una nguvu kama kifo, msisitizo juu ya kujitoa kikamili ni wenye kudai kama Kaburi. Miwako yake ni miwako ya moto, mwali wa moto wa Yah. 7 Maji mengi hayawezi kuuzima upendo, wala mito haiwezi kuufagilia mbali. Kama mtu angetoa vitu vyote vyenye thamani vya nyumba yake kwa ajili ya upendo, hakika watu wangevidharau.”
8 “Tunaye dada mdogo ambaye hana maziwa yoyote. Tutamfanyia nini dada yetu siku atakapochumbiwa?”
9 “Kama akiwa ukuta, tutajenga juu yake mnara wa fedha; lakini akiwa mlango, tutamzuia kwa ubao wa mwerezi.”
10 “Mimi ni ukuta, na maziwa yangu ni kama minara. Basi nimekuwa machoni pake yeye kama msichana anayepata amani.
11 “Kulikuwa na shamba la mizabibu ambalo Sulemani alikuwa nalo katika Baal-hamoni. Aliwapa watunzaji hilo shamba la mizabibu. Kila mmoja alikuwa akileta vipande elfu moja vya fedha kwa ajili ya matunda yake.
12 “Shamba langu mwenyewe la mizabibu liko chini ya mamlaka yangu. Nawe, Ee Sulemani una elfu na wale wanaotunza matunda yake wana mia mbili.”
13 “Enyi mnaokaa katika bustani, hao wenzi wanasikiliza kwa makini sauti zenu. Acheni niisikie.”
14 “Kimbia, mpenzi wangu, ujifanye kama swala au kama mtoto wa paa juu ya milima ya manukato.”
8 comments:
Asante sana Kapulya, nakupenda pia, asante kwa ujumbe, ijumaa njema na kwako
Huu ni ujumbe ndani ujumbe ndani ya wikiendi maridhawa.Hii zawadi ya wikiendi kwa wadau wa kibarazani na hitimisho dhahiri la upendo katika mchakato wa maisha na mafanikio.
-----------------------------------
Wimbo wa Sulemani 8:1-14
1 “Laiti ungekuwa kama ndugu yangu, ukinyonya maziwa ya mama yangu! Ningekukuta nje, ningekubusu. Watu hawangenidharau mimi. 2 Ningekuongoza, ningekuleta ndani ya nyumba ya mama yangu, aliyekuwa akinifundisha. Ningekupa kinywaji cha divai iliyotiwa vikolezo, maji safi ya makomamanga. 3 Mkono wake wa kushoto ungekuwa chini ya kichwa changu; nao mkono wake wa kuume ungenikumbatia.
4 “Nimewaapisha ninyi, enyi binti za Yerusalemu kwamba msijaribu kuamsha au kuwasha upendo ndani yangu mpaka wenyewe utake.”
5 “Mwanamke huyu ni nani, anayepanda kutoka nyikani, akimwegemea mpenzi wake?”
“Chini ya mtofaa nilikuamsha. Hapo mama yako alikuwa na uchungu wa kukuzaa. Hapo yeye aliyekuwa akikuzaa alipata uchungu.
6 “Nitie kama muhuri juu ya moyo wako, kama muhuri juu ya mkono wako; kwa maana upendo una nguvu kama kifo, msisitizo juu ya kujitoa kikamili ni wenye kudai kama Kaburi. Miwako yake ni miwako ya moto, mwali wa moto wa Yah. 7 Maji mengi hayawezi kuuzima upendo, wala mito haiwezi kuufagilia mbali. Kama mtu angetoa vitu vyote vyenye thamani vya nyumba yake kwa ajili ya upendo, hakika watu wangevidharau.”
8 “Tunaye dada mdogo ambaye hana maziwa yoyote. Tutamfanyia nini dada yetu siku atakapochumbiwa?”
9 “Kama akiwa ukuta, tutajenga juu yake mnara wa fedha; lakini akiwa mlango, tutamzuia kwa ubao wa mwerezi.”
10 “Mimi ni ukuta, na maziwa yangu ni kama minara. Basi nimekuwa machoni pake yeye kama msichana anayepata amani.
11 “Kulikuwa na shamba la mizabibu ambalo Sulemani alikuwa nalo katika Baal-hamoni. Aliwapa watunzaji hilo shamba la mizabibu. Kila mmoja alikuwa akileta vipande elfu moja vya fedha kwa ajili ya matunda yake.
12 “Shamba langu mwenyewe la mizabibu liko chini ya mamlaka yangu. Nawe, Ee Sulemani una elfu na wale wanaotunza matunda yake wana mia mbili.”
13 “Enyi mnaokaa katika bustani, hao wenzi wanasikiliza kwa makini sauti zenu. Acheni niisikie.”
14 “Kimbia, mpenzi wangu, ujifanye kama swala au kama mtoto wa paa juu ya milima ya manukato.”
nawewe pia ubarikiwe sana tunakupenda sana
Si uongo Yasinta...Ijumaa njema.
Ijumaa njema kwa wadau wote wa kibarazani.
Thanx for nice massage of the day.
Have anice day
Upendo daima kwa wote na kumbukeni sisi sote ni ndugu kwa vile ni watoto wa baba mmoja.
Maisha na mafanikio ni mchakato endelevu unaohanikizwa na upendo.
Post a Comment