Monday, May 7, 2012

TUIANZE JUMATATU HII KIHIVI:- KAPULYA AKIWA NDANI YA SUTI KWA MARA YA KWANZAKATIKA MAISHA YAKE!!!

Vipi mbona umenuna mama au hupendi ?
Ah! wewe nawe haya ngoja basi nitabasamu kidogo:-)
Kama wasemavyo watu MTU UNAISHI MARA MOJA basi jana jioni nikaona kwanini nisijaribu kuvaa suti na kuina naonekana vipi ndani ya suti.  Hakika ilikuwa kichekesho kwelikweli kama uonavyo katika picha ilikuwa mara ya kwanza na mara ya mwisho...Au? HAYA JUMATATU NJEMA JAMANI.

34 comments:

Mija Shija Sayi said...

Yaani kwanza nilitaka kusema mbona mtakatifu Kitururu leo kawa mfupi?..kumbe ni kapulya

Suti imekupendeza ila sema umepozi kibaba zaidi..

Una vituko wewe!!!!

Mija Shija Sayi said...

Yaani kwanza nilitaka kusema mbona mtakatifu Kitururu leo kawa mfupi?..kumbe ni kapulya

Suti imekupendeza ila sema umepozi kibaba zaidi..

Una vituko wewe!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Mija ww si wa kwanza ni wengi wameniuliza kama Mtakatifu nami ni pacha au ni ndugu? Mwenzangu nikaona sitaki kufa bila kujaribu kuvaa suti ila naona si vazi langu...

chib said...

Angalia tu hiyo suti isikuvae badala ya wewe kuivaa ... LOL

ISSACK CHE JIAH said...

hongera dada kwa kuwa kila kitu kina mwanzo na mwisho wake sasa unatakiwa uvae suti kila basidai yako ndo watu watakuzoea kuna watu huvaa suti wakipata kipa imara na kule kwetu tunavaa suti wakati tuna toka jando tu kwa vijana wa kiume na wadada huvaa gauni lile la asili
Che Jiah

Yasinta Ngonyani said...

kaka Chib! hii suti nilianzima ili kfanya majaribia kama inakuwaje kuvaa suti?

Kaka wangu Che Jiah! Sidhani kama nitavaa tena nimekwisha jaribu mara moja inatosha na nitabaki kwenye magauni na sketi ndiko nifaako:-)

Anonymous said...

Ha ha haaa nimechekajeee, Kapulya kwani suti hiyo ya kike au ya kiume? Nijibu kwanza halafu ndo ntachangia

Anonymous said...

Da Mija kwani mtakatifu mrefu??

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina hiyo suti ni ya mr. niliazima tu si unaona imenivaa kama kaka Chib alivyosema:-)

Usiye na jina wa 12.49...ni kweli swali nzuri kwa Mija kwani Simon mrefu? mimi nadhani tunalingana tu kwa urefu au ufupi.

batamwa said...

kweli suti wala haikufai ndio maana unasema ni mara yakwanza na ya mwisho yaani umekuwa mwanamme kabisa ingekuwa sio kukuzoea kukuona kwnye bulog basi ningefikiri ni kakayo huyo.

Mija Shija Sayi said...

Anony wa 12:49...daah! swali zuri sana, ila kwangu mimi nimwonavyo kwenye picha akiwa na watu niwafahamu ambao siwezi kusema ni wafupi, huwa naona wamelingana. Ila kuanzia sasa itabidi niwe makini kumwangalia asijekuwa anapandaga vistuli.

Yasinta kabla hujafikia uamuzi wa kuacha kuvaa suti kabisa, jaribu suti za kike zinazokufiti kulingana na shepu lako. Hata hivyo suti za sketi je nazo umezipiga chini?

ISSACK CHE JIAH said...

kWA MAONI YA WATU UNATAKIWA UVAE AU UWENDE DUKANI KAPIME SUTI YAKO SIZE YAKO HAPO NDIPO UTUONYESHE JINSI UTAKAVYO PENDEZA MIMI NAAMINI WOTE WALIOKUPONGEZA NA KUKUCHEKA WATABADILISHA TU MADA JARIBU TENA KWENDA DUKANI KISHA MIMI NITAAKUWA MTU WA KWANZA KUKUPONGEZA LEO NASEMA ACHA KUAZIMA SUTI YA SHEMEJI YETU KANUNUE YAKO KISHA WEKA KIBARAZANI
KWAHERI
CHE JIAH

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sipati picha ukitaka kupumua unafanyaje

Rachel siwa Isaac said...

Jamani mwehh hata mimi nilimuazia Kitururu kabla sijaangalia picha vyema,kwani wiki hii kule Fc amemwaga mapicha meengi ya suti.

Da'Yasinta Suti inakupendeza sana tuu, kwani ukinunua/kushona ya kike hakika utazidi kupendeza zaidi.

Pia naona lile ombi ulioombwa la kuvaa Pensi/Kaptula limewadia au?

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

umetoka bombi ile mbayaaa! kama vile prezenta wa Tv!!!!

Jumatatu yangu imeanza vema pia...kumbe na mie nitaanza kuvaa suti maana naona chama cha wasovaa suti kinaanza kupotelewa na wanachama teh teh teh

Ester Ulaya said...

hahahahaha Da'Mija kama upo mawazoni mwangu, nimecheka mie leo, nikasema nikitulia ndo niandike, Mdogo wake kituru huyu jamani,

Yasinta unavituko sana, leo nimeongeza maisha mara tatu, uliwaza nini lakini? kesho usivae ya kuazima kanunue size yako dukani ndo tutajua uendelee kuvaa au lal

Ester Ulaya said...

hahahahaha Da'Mija kama upo mawazoni mwangu, nimecheka mie leo, nikasema nikitulia ndo niandike, Mdogo wake kituru huyu jamani,

Yasinta unavituko sana, leo nimeongeza maisha mara tatu, uliwaza nini lakini? kesho usivae ya kuazima kanunue size yako dukani ndo tutajua uendelee kuvaa au lal

Mija Shija Sayi said...

@Ester Ulaya...laiti ungejua umri wa Kitururu usingethubutu kusema mdogo wake Kitururu huyu..hahahaha.. Ngoja Kitururu anisikie..

Yasinta Ngonyani said...

Mweeh! kaaaazi kwelikweli yaani nimecheka mpaka basi Ester yaani umenifurahisha kweli MDOGO WAKE KITURURU...hujui kama mimi ni bibi kizee? haya bwana maana hii nayo ni moja ya sifa...Jamani mwenzenu nilikuwa tu najaribu kuvaa suti...

Ester Ulaya said...

jamani mimi mwanichekesha sana bandugu, ujue huo ufupi si ndio nikadefine fasta mdogo wake, anisamehe bure Simon, Yasinta ungevaa Viatu virefu hakika hii definition isingekuwepo, Vazi limenifurahisha sana

Yasinta Ngonyani said...

Ester wala si uonge ni kweli katika picha hii nimeonekana mfupi kuliko kawaida ni kwamba jana katika familia tulikuwa na kamchezo ka kuigiza ndo nikapigwa hiyo picha ...Hata rafiki yangu mmoja kaniambia pia kama ni dadake Kitururu? Sijui yeye mwenyewe yupo wapi? Maana kakaa kimyaaa...

Penina Simon said...

Wala sio kichekesho umependezeamo sana tu,

ray njau said...

Dada huyo anameremeta na ameshaolewa kwa waswedi na mahari imeshatolewa huko kwetu Ruhuwiko Songea!!!!!!!!!!x3.

Simon Kitururu said...

DUH!:-)

Simon Kitururu said...

Mie nimependa lakini Da Yasinta huo mtoko wako!

Yasinta Ngonyani said...

Sasa upo nasi watu wengi walifikiri ni wewe..Mtoko upi tena jamani...??

Simon Kitururu said...

MTOKO wakisutisuti!@Kadala Yasinta!

Yasinta Ngonyani said...

Niliona nami nijaribu maana mtu unaishi mara moja tu lakini nimeona nimetoka kivyake nimekuwa wewe:-) Si umesoma maoni yote wasomaji wameona ni kama vile wewe au mdogo wako:-)

Simon Kitururu said...

Yasinta nimuulize Baba nini? Isijekuwa siye ndugu!:-) Natania!

Yasinta Ngonyani said...

Muulize labda dadako...LOL kama ni hivyo nami nakutania ila kweli kiduchu kwa mbali tumefanana katika hiyo suti:-)

Ester Ulaya said...

hahahhaha msiwaulize wazazi jamani, nyie endeleeni kuwa ndugu tu

Salehe Msanda said...

Umependeza;

Kila la kheri,ila nadahani enzi za utoto uliwahi kuvaa suti na si kweli kuwa ni mara yako ya kwanza.

KBI said...

Hata mm nilifikiri kwanza Kitururu yani kopi left kabisa Yasinta kisuti bomba hicho kwako.

ray njau said...

Dada Yasinta hakika kwa suti umependeza.Hongera sana binti Nangonyani mama wa Afrika.