Sunday, May 6, 2012

JUMAPILI :- LEO TUANGALIA NENO UZINZI!!

Uzinzi ni kinyume cha mpango wa Mungu kuhusu mapendo ya kibinadamu na ndoa. Kwa sababu hiyo, Uzinzi ulikatazwa kabisa katika Taifa la mungu. Kutoka 20:14,17 inaeleza amri ya Mungu
Usizini;
Usitamani mke wa mwenzako.
JUMAPILI NJEMA KWA KILA ATAKAYEPITA HAPA:-)

5 comments:

Rachel siwa Isaac said...

Asante sana dada kwa neno,Mungu akubariki wewe na familia na woooote.J'2 iwe njema pia.

Yasinta Ngonyani said...

Rachel nakuambia leo ni siku ya kupumzika na kusali tu. Na halafu kuna kajua basi ndo raha kweli..Naamini Jumapili yako pia ipo safi:-)

emu-three said...

Pia kwa Waislamu imekatazwa, sio kuifanya tu, hairuhusiwi hata kuikaribia zinaa— Qur'an, Sura 17 (Al-Isra), ayat 32.

ray njau said...

EPUKA MAMBO YANAYOMCHUKIZA YEHOVA MUNGU.

Uuaji.—Kutoka 20:13; 21:22, 23.
Ukosefu wa maadili.—Mambo ya Walawi 20:10, 13, 15, 16; Waroma 1:24, 26, 27, 32; 1 Wakorintho 6:9, 10.
Kuwasiliana na pepo.—Kumbukumbu la Torati 18:9-13; 1 Wakorintho 10:21, 22; Wagalatia 5:20, 21.
Kuabudu sanamu.—1 Wakorintho 10:14.
Ulevi.—1 Wakorintho 5:11.
Kuiba.—Mambo ya Walawi 6:2, 4; Waefeso 4:28.
Kusema uwongo.—Methali 6:16, 19; Wakolosai 3:9; Ufunuo 22:15.
Pupa.—1 Wakorintho 5:11.
Jeuri.—Zaburi 11:5; Methali 22:24, 25; Malaki 2:16; Wagalatia 5:20.
Maneno yasiyofaa.—Mambo ya Walawi 19:16; Waefeso 5:4; Wakolosai 3:8.
Kuitumia damu isivyofaa.—Mwanzo 9:4; Matendo 15:20, 28, 29.
Kukataa kuiandalia familia.—1 Timotheo 5:8.
Kushiriki katika vita au katika mizozo ya kisiasa ya ulimwengu huu.—Isaya 2:4; Yohana 6:15; 17:16.
Kuvuta sigara au kutumia dawa za kulevya.—Marko 15:23; 2 Wakorintho 7:1.

Salehe Msanda said...

uongeze na usitamani mume wa mwenzio au?