Tuesday, May 8, 2012

UNAPOJIKUTA UNATAMANI NYUMBANI BASI SI VIBAYA KUANGALIA PICHA ZA NYUMBANI:-SONGEA YETU!!

 Kwa wale wote waliofika Songea Mjini mnajua hapa ni wapi. Au niseme tu hapa ni Songea mjini
Na hapa ni soko kuu la Songea.
Picha hizi zimenikumbusha sana Songea nimepatwa na HAMU ya kuwa Songea hakika nyumbani ni nyumbani. Picha ni picha lakini ni kumbukumbu moja nzuri sana. KARIBUNI SONGEA!! 

10 comments:

Mtani said...

Yasinta,

Hiyo picha ya juu ni sehemu gani hapo? Maana unasema mjini wakati mjini ni kubwa sana. Hata watu Lizaboni nao wako Mjini, hata Matarawe nao wako mjini na huku mitaa ya Posta, Magereza na Hospitali ya Mkoa wote wako mjini.

Hii ni Songea mpya, sio ile ya miaka ile zama za ma-bus ya Kwacha na KAURU. Hongereni watani zangu wangoni kwa kwa maendeleo ya mji wa Songea.

Yasinta nitafutie picha ya Uwanja wa Maji Maji, nilicheza HALAIKI kwenye uwanja huo mbele ya Mzee Mwinyi na kampeni yake ya Fagio la Chuma!

Nitarudi tena "Songiya" (Dr. Remmy - RIP)

ISSACK CHE JIAH said...

Asante nitakwenda tena sangea siweszi kusema sirudi tena kwa mjomba kama kitndawili kisemavyo ,mimi najuwa wakati ule miaka na hiyo songea jengo kubwa au gorofa ilikuwa ni kwa tajiri mmoja anaitwa komba sijajua komba gani na mwingine tajiri alikuwa ana mabasi sijuwi anaitwa mtumwene na wale akina matimila ndiyo walikuwa mabosi wa pale songea,kwakweli najuwa songea nijuayo mimi ya mwaka 1980 si ya leo kwani hilo soko kuu lilikuwa na jengo dogo si sana ila nje kulizungukwa na vijibanda na upande wa mashariki klikuwa na duka la wale akina haider na hapa karibu na gorofa la komba kulikuwa na duka la viatu la BORA SHOES enzi hizo wao ndo wauzaji wa kuu wa viatu tanzania ukirudi nyumakidogo kwenye njia panda ya kwenda chuo cha wauguzi pale kulikuwepo na hoteli moja nadhani ilikuwa inaitwa NEW HAPPY sikumbuki vizuri hapo ndipo barabara kuu itokayo tunduru kupitia stendi ya mabasi ,
lizaboni safari kuelekea PERAMIHO,GEREZA KUU LA KILIMO KITAI SEMINARI LIKONDE SEKONDARI YA KIGONSERA,MJI MMOJA HOPO JUU LIPUMBA MBINGA HIYOOO NATAKA NIENDE HOSPITALI LITEMBO UKIMALIZA MILIMA YA UMATENGONI LEO SIENDI MBAMBABAY NAISHIA HAPO
Dada songea mji unanzia kule sonea sekondari si kwenye magorofa ya akina komba tuu na huku mpaka kule jeshini majengo kule ruvuma na njia ya dar kule wanajina lake kote mjini songea usisahau RUHUWIKO MOTE SONGEA MJINI
ASANTE
CHE JIAH

Yasinta Ngonyani said...

Haya ndugu zanguni picha hiyo ya kwanza kama unatoka Mahenge, unafika makumbusho ya majimaji na badaye kanisa la Angalikana na baada ya hapo unafika benki NBC kwa hiyo hapa unateremka kidogo tu kushoto ndio soko na kulia kuan duka la Abasia bookshop na ukiteremka kidogo na kupinda kulia utafika Msikiti wa mkoa.

ray njau said...

Dada huyo ameshaolewa huko kwa waswedi na kurudi Songea ni kuja kutembea.!!!!!!!!!!x3

John Mwaipopo said...

sasa hapo nyumba iko wapi na bomba liko wapi?

John Mwaipopo said...

... na jogoo mkubwa-mkubwa yuko wapi?

Yasinta Ngonyani said...

Ray! una mbwembwe ww..kwanini isiwe kuishi?
Kaka John Nyumba gani na baombo lipi? halafu jogoo mkubwa mkubwa sijui kama nimekupata hapa...naona ukapulya wangu hapa umekwama..

John Mwaipopo said...

"kwetu nyumbii-bombii halafu kuna jogoo mkumbwa mkubwa" hapo ndio kwetu.

je nimeeleweka sasa?

Yasinta Ngonyani said...

Oh! kumbi ulikuwa unamaanisha "nishikie gari nipandi nyengu" Nimekuelewa kaka John tupo pamoja..

batamwa said...

nyumbani ni nyumbani hatakama nipolini au sio?