Wednesday, May 16, 2012

Wanafunzi wanasomea vibanda vya nyasi!!

Ni ile JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO NA LEO NIMEONA TUTEMBELEE WILAYANI NAMTUMBO.ELIMU NIMEIPATA HABARI HII  Albano Midelo Haya KARIBUNI.  Wanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi
 SelousWilayani Namtumbo wakiwa darasani.

WANAFUNZI wa shule tatu za msingi zaidi ya 500 katika kata ya Rwinga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wanasomea kwenye madarasa yaliojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi.
Uchunguzi uliofanywa katika shule tatu kati ya saba zilizopo kwenye kata hiyo ambayo ipo mjini Namtumbo umebaini kuwa katika shule ya msingi Rwinga wanafunzi 296 wanasomea kwenye vibanda vya miti vilivyoezekwa kwa nyasi.
.
Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo Onesmo Mbawala alisema idadi kubwa ya wanafunzi katika shule hiyo wanasomea katika vibanda vya nyasi kutokana na shule hiyo kuwa na upungufu wa vyumba 12 vya kusomea ambapo vyumba vilivyopo ni vinne tu na kwamba shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1975 ina jumla ya wanafunzi 592.
Katika shule ya msingi Selous jumla ya wanafunzi 108 wa madarasa ya tano na sita wanasoma kwenye vibanda vya nyasi hali ambayo walimu wanasema inachangia kushusha taaluma kwa wanafunzi.
Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo Sheweji Simba alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 ina jumla ya wanafunzi 477 huku ikiwa na vyumba vinne tu vya madarasa kati ya mahitaji ya vyumba nane hali ambayo imesababisha baadhi ya wanafunzi kusomea kwenye vibanda vya nyasi .
Katika shule ya msingi Mkapa ambayo imepewa jina la aliyewahi kuwa kiongozi mkuu wa nchi Rais mstaafu Benjamin Mkapa pia kuna wanafunzi wanaosomea kwenye vibanda viwili vya nyasi kwa kuwa shule hiyo ina vyumba vinne tu kati ya mahitaji ya vyumba nane.
Mkuu wa shule hiyo Hans Mwailima alisema shule hiyo yenye wanafunzi 306 madarasa matatu yanasomea katika chumba kimoja ambapo kuanzia darasa la tatu hadi la sita wanasomea kwenye vibanda vya nyasi kwa zamu .
“Unajua wanafunzi wana tabia ya kutaniana hivyo endapo darasa moja wakisoma kwenye vibanda vya nyasi kila siku wenzao wanawatania hivyo kukata tamaa na wengine kuwa watoro hivyo tumeamua wote wawe wanasoma kwenye vibanda vya nyasi kwa zamu ili kujenga mvuto wa mazingira ya kusomea’’,alisema.

Wanafunzi wa shule ya msingi Mkapa Wilayani
Namtumbo wakiwa darasani na mwalimu wao.

Mratibu elimu kata ya Rwinga Thomas Komba amekiri shule tatu kati ya saba katika kata yake ambazo ni Rwinga,Mkapa na Selous wanafunzi kusomea katika vibanda vilivyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi na kusisitiza kuwa shule za Minazini,Kidagulo,Migelegele na Mandepwende ndizo shule pekee katika kata hiyo ambazo hazina vyumba vya madarasa vilivyoezekwa kwa nyasi.

“Shule zangu tatu za Rwinga,Mkapa na Selous katika kata yangu zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa hali ni mbaya tunafanya jitihada za kuhamasisha jamii ili waweze kujitolea kufyatua tofali kuzichoma kwa kushirikiana na serikali ili kupata vyumba zaidi na kumaliza kero hii ya aibu’’,alisisitiza.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Kasimu Ntara alidai kuwa kuwa kuwepo kwa madarasa yaliojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi katika wilaya hiyo kunatokana na kuanzishwa shule nyingi za msingi .
“Mpango wa uboreshaji wa elimu ya msingi MEM nchini ulisababisha kuanzishwa kwa shule nyingi hivyo baada ya kuondoka kwa MMEM serikali imeshindwa kumudu ujenzi wa vyumba vya madarasa jitihada zinaendelea kufanyika kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa’’,alisisitiza.

TUKUTANE TENA JUMATANO IJAYO KWA JINGINE LA ZAMANI!!

14 comments:

Ester Ulaya said...

yaani hawa ndo wabunge,mawaziri, walimu, masurveyor nk. wajao, ukweli mazingira kama haya automatically lazima watoto wafeli,mh

emu-three said...

Lazima watafeli Ester, nakubalina na wewe,halafu ndio wakitoa matangazo ya matokea wananadisha kuwa shule iliofaulisha vyema ni....
Hivi kweli kuna haja ya kulinganisha ufaulu,....mnalinganishaje na hali kama hii, haiji katika mizani...
Sawa mwenye nacho atapata zaidi , lakini tukumbuke huenda hapo kungelitokea majiniasi,...wanasayansi wakubwa, lakini wanazimwa kiaina,...na nini hatima yake,mtaoana siku zijazo.
Sasa zipo shule za kata...nachelea kusema kuwa hizo ni bora ziitwe shule za `walalahoi...'TEMBELEENI MZIONE NA ONENI MATOKEO YAKE YA MITIHANI NA KWENYE MATOKEO ZINALINGWANISHWA NA INTANESHINO SKULI, ZA WENYE NAZO.hiyo sio haki kabisa,linganisheni kutokana na madaraja, za juu chini na kati...maana hata makzini siku hizi mishahara ndio hivyi hivyo, kuna wakuja ,mwenzangu na mimi na tx...mpo hapo

Yasinta Ngonyani said...

Este, na emu3! nakubaliana nanyi kabisa hapo hakuna kusoma kabisa kwa sababu gani mtu unaposoma unahitaji utulivu yaani sehemu iliyo kimya nk. Sasa hapo kweli kuna utulivyo hapo kweli? akipita mtu wote wanachungulia au sijui mdudu..Yaani baada ya miaka 50 ya huru hali bado ileile kwa kweli inaumiza sana.
Hivi hisi shule za kata, kwanini zimeanzishwa kama shule za msingi hali ndio hii..Sio kwanza kuwa na msingi na ndipo watoto wanaweza kwenda kusoma huko katani? Au hii ni kama sifa tu kila kata ina shule ya sekondari? Lakini kama hakuna msingi je nani atasoma katika hizo shule za kata?..naacha na wengine waseme kwanza....

ngaizaskids said...

Du nimekumbuka chekechea yangu chini ya mti mwe siku moja joka huko juu likawa linatuchungulia tunavyoteseka tulikiMbiaje sasa, Tanzania nchi yenye mlima mrefu, maziwa yatoayo samaki na kulisha majuu, mbuga za wanyama n.k Leo hii tunaona hivi mh! Kweli Tanzania italiwa na wenye meno na wanaimaliza haswa!

Mungu ibariki Tanzania

Yasinta Ngonyani said...

Ndiyo hapo sasa ngaizaskids! Nchi yenye Amani na Upendo na hivyo pia ulivyotaja hapo juu. Lakini hatuwezi kujinufanisha wengine wanakuja na kuchukua kila kitu na sisi tunabaki palepale miaka nenda rudi...Halafu jambo moja mimi linishangazalo ni kwamba hizi shule za kata kama kule kwetu Songea/peramiho wazazi wanahitaji kuchanga kila kitu hadi dawati au sijui kiti na meza kwa mtoto. na ada juu yake. Sasa hii ni nini? Cha kuchangaza sasa mtoto alishafeli kwa vile hali kama hiyo kwenye picha si hali ya mtoto kuweza kuituliza akili yake katika masomo. aahh nina mengi sana ya kuandika ila wengine nao wapeta ruhusa...

ray njau said...

Hapa lawama ni kwetu sote kwa kudumisha utamaduni wa kuwekeza kwenye mambo yasiyo na tija kijamii.
Suala la madawati siyo suala la kutuumiza kichwa hapa Tanzania kutokana na wingi wa mbao.Kilichopo ni sisi wanajamii tuamue kupitia uwajibikaji wa pamoja.Nilijaribu kuomba mtandao mmoja wa simu uanzishe promosheni ya ongeza salio uchangie dawati chini ya uratibu wa VETA na SIDO lakini hadi leo ni kigugumizi kitupu.Tukiamua tutaweza na tukinyamaza tutashindwa.

Mshana said...

Dah! Cmchezo kwakwel suala la elimu tz bado ni changamoto sugu. Mana kwa hali kama ile inamaana serikali haina taarifa ya shule kama ile? Kiukwel hakuna ambaye hili litamuingia akilini kwamba tanzania hii ya tatu kwa madini ya dhahab dunian na wilaya hyo ya namtumbo ndo ilomfaoya bush aspend siku nne tz kwasabab ya madin ya uranium yayopatkana kwa wingi wilayan namtumbo, inazo miongon mwa shule zake kama ile, watoto wanasomea kwenye vibanda kama vya kuhamia mchele kweli? Alaf muda huohuo inawabunge wanaotembelea gar ambazo gar moja lina garama ya kupata shule moja standard na vifaa vya kutosha. Kwakwel watanzania tunatakiwa kuwaangalia viongoz 2naowapadhamana ya kutuongoza.

Mija Shija Sayi said...

Ndiyo tunatakiwa turudi sasa tukafanye mabadiliko, maana mapungufu tunayoyaona sisi inawezekana kabisa wao hawayaoni...

Au Mtakatifu Kitururu unasemaje?

ray njau said...

Ndugu zangu,ndugu zangu,ndugu zangu nisikilizeni.Hapa tatizo siyo mtu kwa jina bali ni mfumo wetu usiotambua wala kutambua vipaumbele katika jamii.Hapa tuwekeze katika mabadiliko kuanzia ngazi ya kifamilia.Iwapo tumeamua kuwekeza katika sherehe na tafrija za kijamii na kusahau kuwa watoto wetu wanasomea kwenye vibanda vya nyasi bila walimu na madawati acha tukavune tulichopanda.

"KUPANGA NI KUCHAGUA NA KUCHAGUA NI KUPAMGA"."ZILONGWA MBALI ZITENDWA MBALI."ZILONGWAZO SIYO ZITENDWAZO".
==================================
MADA KUU HAPA NI:
TUFANYE NINI ILI TUPATE PESA KWA AJILI YA UNUNUZI WA MADAWATI YA KUTOSHELEZA MAHITAJI YA WANAFUNZI WOTE NCHINI TANZANIA?
=================================

Anonymous said...

Binafsi nimefundisha shule ambayo darasa ni full suit...tembe..udongo chini juu juu na madawati pia ni udongo ulioinuliwa zaidi, ndani ya darasa moja wanasoma madarasa mawili, la tatu wanageukia kule na la nne huku, walimu wawili mnaingia darasani kwa wakati mmoja...
Mabadiliko niliyoyafanya ni kwenda kusoma fasta ili niondoke kule na kweli niliondoka.
Tulikuwa tunasikia tu wakaguzi kwetu hawafiki...
Wanakijiji hawataki watoto wao waje shule kwahiyo vigumu kuwashawishi wachangie ujenzi wa madarasa, serikali ya kijiji hata haielewi unachowaambia serikali kuu ndo haina habari kama tupo...
Natamani kurudi leo baada ya miaka 14 nikaangalie kama kumebadilika au bado kuko vilevile au kuna mabadiliko.

Yasinta Ngonyani said...

Jamani! Hapa kila nikifikiri naona kama cha msingi hapa ni kuanza na paa na sio madawati kwa vile wakiwa na madawati je watakaa na jua pia mvuu iwapige? Halafu asiye na jina wa 11.38AM hilo la kuguuziana migongo katika darasa moja kwa nini msinge jenga ukuta na kuwa madarasa mawili? Ningekuwa mwanafunzi nadhani ningetoka kila siku sifuri maana walimu wawili kufundisha wakti mmoja ...

Ester Ulaya said...

sasa nikigombea ubunge nikajitahidi kuboresha haya nitapona?? nasikia uchungu jamani,Ngaiza poleni kwa nyoka kuning'inia

ngaizaskids said...

Asante my wii Gombea utupunguzie

Salehe Msanda said...

Hbr,
Hii ndo Tanzania yetu.
Tuna safari ndefu ya kufika katika maendeleo ya kweli