Sunday, May 27, 2012

LEO NI SIKU YA AKIMNA MAMA (MORS DAG)


Hapa Sweden leo ni siku ya akina mama duniani. Nasi leo tumeamua kumpongeza mama yetu mpendwa ktk blog yake ni sisi Camilla na Erik. Tunampenda sana mama yetu hasa akiwa na hasira, huwa tunapata kila kitu tutakachotaka.( kwa niaba ya mama)

Ok, basi nami nimepata nafasi ya kusema machache ni kwamba. Najua sehemu nyingine siku hii imeshapita ila hapa Sweden ni leo. nami napenda kuwapa pongezi akina mama wote duniani bila kumsaau mama yangu. NAWAPENDA AKINA MAMA WOTE DUNIANI.NA TUTAFIKA TU.

6 comments:

sam mbogo said...

Hongera mama C&E. kaka s.

Mija Shija Sayi said...

Hongereni sana kina mama wa Sweden, hongera Yasinta kwa kuwa mama mwema.

Kila la heri kina mama woote..

ray njau said...

@Erik&Camilla Klaesson:
Napenda kuchukua fursa hii kuwapongezeni sana kutokana na uamuzi wenu wa kuonyesha ushujaa wa kumpongeza mama yenu akiwa hai.Naamini kuwa maneno yenu machache ni yenye thamani sana moyo mwake na atayahifadhi kwa muda wote wa maisha yake.Kumbukeni kuwa watoto hawana uwezo wa kulipa wazazi wao gharama halisi za malezi na wala hakuna mzazi mwenye nia ya kumdai mtoto gharama hizo lakini ni jukumu la watoto kutambua kuwa wana deni kubwa sana mbele ya wazazi wao.Siku zote wazazi wanataka watoto waonyeshe hisia mwenzi zenye fadhili-upendo na wonyesho halisi wa KUJALI.Hata umpe mzazi wako dola 100,000,000,000,000.00 hatakuwa na thamani yoyote kwake iwapo hutaonyesha kuwa unamjali.Erik &Camilla nawatakieni afya njema,baraka tele,utendaji maridhawa na ufanisi bila nukta.
-----------------------------------

MFANO KWA WATOTO
---------------------

17 Je, watoto wanaweza kujifunza kutoka kwa Yesu? Ndiyo, wanaweza! Kupitia mfano wake, Yesu alionyesha jinsi watoto wanavyopaswa kuwatii wazazi wao. Alisema: “Kama vile Baba alivyonifundisha, ndivyo ninavyosema.” Akaongezea: “Sikuzote mimi hufanya mambo yanayompendeza.” (Yohana 8:28, 29) Yesu alimtii Baba yake wa mbinguni, na Biblia inawaambia watoto wawatii wazazi wao. (Waefeso 6:1-3) Ingawa Yesu alikuwa mtoto mkamilifu, aliwatii wazazi wake, Yusufu na Maria, ambao hawakuwa wakamilifu. Hapana shaka kwamba hilo lilichangia furaha ya kila mmoja katika familia ya Yesu!—Luka 2:4, 5, 51, 52.

18 Je, watoto wanaweza kutambua njia wanazoweza kumwiga Yesu zaidi na kuwafurahisha wazazi wao? Ni kweli kwamba nyakati nyingine watoto huona ni vigumu kuwatii wazazi wao, hata hivyo, Mungu anataka watoto watii. (Methali 1:8; 6:20) Yesu alimtii Baba yake wa mbinguni sikuzote, hata hali zilipokuwa ngumu. Pindi moja, Mungu alipomtaka Yesu afanye jambo gumu sana, Yesu alisema: “Niondolee kikombe hiki [au takwa fulani].” Hata hivyo, Yesu alifanya mapenzi ya Mungu kwa sababu alitambua kwamba Baba yake anajua mwendo bora wa kufuata. (Luka 22:42) Kwa kujifunza kutii, watoto watawafurahisha wazazi wao na Baba yao wa mbinguni.#—Methali 23:22-25.
19 Ibilisi alimshawishi Yesu, na tunaweza kuwa na hakika kwamba atawashawishi watoto pia wafanye mambo mabaya. (Mathayo 4:1-10) Shetani Ibilisi hutumia mikazo ya marafiki ambayo inaweza kuwa mikali sana. Basi ni muhimu sana watoto wasishirikiane na wale wanaotenda mabaya. (1 Wakorintho 15:33) Dina, binti ya Yakobo alishirikiana na watu ambao hawakuwa wakimwabudu Yehova, na kufanya hivyo kulimletea matatizo makubwa. (Mwanzo 34:1, 2) Hebu wazia jinsi familia inavyoweza kuumia mmoja wao akihusika katika mwenendo mpotovu kingono!—Methali 17:21, 25.
---------------------------------
@Yasinta;
Hongera sana kwa siku ya mama kwa kuwa ni kama mama?Kila mtu hulia mola wangu au mama yangu!Mama ni dhahabu isiyo thamani?
Hongera sana kwa kuendelea kutimiza wajibu wako wa mama mwenye upendo kwa familia yake.
-------------------------------
Zaburi 127:1-5

Wimbo wa Mipando. Wa Sulemani.

1 Yehova mwenyewe asipoijenga nyumba,

Ni bure kwamba wajenzi wake wameifanyia kazi ngumu.

Yehova mwenyewe asipolilinda jiji,

Ni bure kwamba mlinzi ameendelea kukaa macho.

2 Ni kazi ya bure kwamba ninyi mnaamka mapema,

Kwamba mnakaa mpaka kuchelewa,

Kwamba mnakula chakula kwa maumivu.

Hivi ndivyo anavyompa hata mpendwa wake usingizi.

3 Tazama! Wana ni urithi kutoka kwa Yehova;

Uzao wa tumbo ni thawabu.

4 Kama mishale mkononi mwa mwanamume mwenye nguvu,

Ndivyo walivyo wana wa ujanani.

5 Mwenye furaha ni mwanamume ambaye amelijaza podo lake na hao.

Hawataona aibu,

Kwa maana wataongea na adui langoni.
---------------------------------
Mama wa familia ni mwalimu,daktari,

ray njau said...

Mama wa familia ni daktari,mwalimu,hakimu,na mtekelezaji wa majukumu ya kifamilia.
HONGERENI SANA AKINA MAMA NA MUNGU AWABARIKI KATIKA MAJUKUMU YENU YA KILA SIKU!

Interestedtips said...

they love their beloved mama, safi sana

Rachel Siwa said...

Hakuna kuchelewa,Hongereni wa mama woote Mungu azidi kuwabariki/kutubariki na kuwasimamia/kutusimamia katika malezi ya Watoto,Hongera sana Shemeji baba Erik kwa kumfanya Kadala kuwa mama,Pia kina Eriki kwa kumpata mama huyu!!!!!