Thursday, May 3, 2012

EBU ANGALIA HAPA KAAAZI KWELIKWELI MAISHA HAYA JAMANI!!!


Habari/simulizi kama hii niliwahi kusikia wakati ule naishi Madaba/Matetereka kuwa akina mama walikuwa wakienda kilabuni walikuwa wakiwanywesha watoto pia. Kisa walikuwa wanataka watoto wasiwasumbue, maana wakipata pombe basi wanalala...duh! kweli tembeo uone!!! NAWATAKIENI WOTE JIONI NJEMA INGAWA KWANGU YAMEIBUKA MASWALI KIBAO KICHWANI BAADA YA KUONA HII HABARI. !!!

5 comments:

ray njau said...

Maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua.
=====================================
Mlee mvulana kulingana na njia inayomfaa; hata atakapozeeka hatageuka kando na kuiacha._Methali 22:6
================================

Anonymous said...

Dada Yasinta,kwanza mtandao wangu unanizingua sijatizama hiyo video natumia maelezo yako kukueleza visaa viwili kuhusu pombe na watoto, mtanisamehe kama ntaenda nje ya mada.
Kaka yangu alibahatika kupata kabinti ka mjini wakapata ujauzito na akazaliwa mtoto wa kiume mzuri mno, Ubungo DSM, wifi yangu na kaka hawakuwa wazai wale tulowategema bado beach wao, party wao, disco wao night club wao...mtoto anaachwa na msichana ili asisumbue wanampa kizibo kimoja cha konyagi mtoto analala fofofo...kuna siku mpaka wamerudi wamelala wameamka mtoto kalala tu mpaka wakampeleka hospitali kumbe walipoondoka akaamka na msichana wa kazi akamwongeza tena... Huyo mtoto sasa hivi yuko form four uwezo wake darasani wa kawaida ila anakunywa pombe huyo kama komba na halewi ng'oo na kaka hana la kusema.
Kisa cha pili ni cha rafiki yangu wa kiume (just a friend), yeye alikuwa anaishi na baba ake huko mbali na mama yao kikazi... baba akiacha chupa zake za whisky mtoto anamimina anakunywa anaongeza vimaji kidogo baba asigundue, akaishi hivyo akaja kuoa mwaka wa 12 sasa hajaapata mtoto katika pitapita kwa wataalamu akaambiwa mbegu zake haziwezi kutungisha mimba na sababu mojawapo alioambiwwa ni pombe....

Mtani said...

Mambo ya togwa hayo ... wenyeji wa mikoa ya Iringa na Njombe huwa wanasema Ulanzi mtoto hawezi kulewa, kwa hiyo nyakati za msimu wa kilimo watoto hupewa ulanzi ili walale na hivyo kuwapa fursa mama zao wafanye kazi za kilimo.

Kosa lao ni kwamba huwa hawajiulizi kwanini mtoto akipewa ulanzi huwa analala fofofo? Kulewa kupo kwa aina nyingi. Sasa kwa kuwa mnywaji ni mtoto huwezi jua kama amelewa maana haongei au hatembei ili uone kama anapepesuka au kusema ovyo. Kulala fofofo ni dalili mojawapo ya kulewa pombe na ndio maana walevi wengi watu wazima wakizidiwa na pombe wanaweza kulala popote.

Ndio mambo ya mila yenyewe

Yasinta Ngonyani said...

Ray! Ni kweli usemacho na asente kwa neno hilo.
Usiye na jina! ni habari ya kusikitisha wakati mwingine hawa wasichana wa kazi wanaharibu sana maisha ya wanetu. Na hicho kisa cha pili pole sana na yeye kama ndo kweli pombe zimesababisha. Ahsante sana kwa visa hivi vya kufundisha.

Mtani! Togwa ni togwa na mtoto unaweza kumpa ila si mtoto wa mwaka mmoja . Ulanzi ni pambe mtani inalewesha ingawa sijawahi kunywa ila najua. Nafikiri akina mama wengi wanachotaka wakiwa klabuni kuwa wasisumbuliwe na watoto ili wao wapte starehe adhali zake wao hawajali kabisa. Kinashotakiwa hapa ni kuwahamasishatu.

cytotec said...

obat telat bulan i think your blog very informative obat penggugur thanks for sharing obat cytotec