Thursday, May 10, 2012

TUSISAHAU METHALI ZETU/BAADHI NI IMANI ZA USHIRIKINA (SUPERSTITIONS)!!

1.Kuku wakionekana kama wananongónezana basi patafika wageni ghafla.
2. Kuweka mikono kichwani bure tu, kunaleta kifo cha mzee wake mtu.
3. mtu akiinuka akaona nguo imeganda matakoni basi inaonyesha kuwa mtu huyo ana tabia ya kusema uwongo.
4. Mwanamke hali ndizi pacha(hasa mwenye mimba) kwa kuchelea kuzaa watoto pacha..
5. Ukiona mwasho juu ya kiganja cha mkono wa kilia utapokea fedha.
6. Kiganja cha mkono wa kushoto kikikuwasha ni alama ya kutumia fedha.
7. Ukijikwaa mguu wa kulia pana heri inakungoja huko uendako.
8. Ukijikwaa mguu wa kushoto utafikwa na maafa huko uendako.
UKIWA NA METHELI NAWE UNAWEZA KUONGEZEA NA NDIYO KUJIFUNZA MENGI!!!

9 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Hizi nadhani si methali bali hekaya za wahenga....

nimeipenda hiyo namba 4 na nitaipinga sana kwani napenda watoto mapacha :)

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Chaha naomba unipe tafouti ya Metheli, Hekaya, kitendawili, nahau na misemo? Hahaha eti unapenda watoto mapacha:-)

Joseph U said...

dah kwakweli waafrika utamaduni wetu ni babkubwa''''wazungu hawana uchawi kama huu

Ester Ulaya said...

1.ukiona buibui anakutambalia utapata zawadi au hela
2.ukiona buibui anashuka mlongoni kutokea juu ujue utapata wageni
3.ukiona jicho lincheza kuna kitu utakiona usichokitegemea
4.ulimi ukiwcheza utalia au utaongea sana hasa ktk mabishano
5.ukiona nyoka wanajamiina ujua msiba wa ndugu akuhusuye utatokea.
Ngoja nipumue nitaendelea baadae

Yasinta Ngonyani said...

Joseph U! mbona hata wazungu wanazo hizo nimeshawahi kusikia 1. Usiweke fungua mezani ni bahati mbaya
2. usiruke ngazi utapata mikosi ..ngoja nipumzike nitaendelea..

Ester! Ya kwanza, pili, nne na tano hizo kwangu ni ngeni. Ahsante kwa kujumuika mnami yaani kwa kutokuwa mchoyo:-)

Ester Ulaya said...

nendeleza pale
6.kama tumekaa kwa kunyoosha miguu ukituruka tunakuwa wafupi
7.ukiwashwa sana miguu kule kwa kukanyaga utasafiri.
8.ukiota kuna sherehe eti msiba utatokea, duh
9.ukijing'ata gafla kuna mtu anakuongelea either ndugu yako
......

Yasinta hiyo ya buibui na kuwashwa mikono naweza kuconfess nimeifuatilia sana ni kweli, mfano tokea jana mkono wa kushoto umewasha sana, can u imagine kuna mtu nilikuwa namdai over a year now leo kanipigia kaniletea hadi nikabaki hoi na nilikuwa nimegive up, zipo zina apply

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

da Yasinta...labda nimwalike Mwl. Matondo atupe busara zake maana umetaja vingi sana teh teh teh.

Ndiyo napenda mapacha!

Rachel siwa Isaac said...

Teh tehteh kaka Chacha tunasubiri Mapacha!

Na kujikwaa wajikwae wakubwa lakini watoto wakijikwaa makonzi/kukalipiwa hutembei vizuri,huangalii chini!!!

Asanteni kwa shule hii Waungwana.

obat vimax said...

vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg