Saturday, May 19, 2012

JUMAMOSI HII NIMEKUMBUKA MATETEREKA/MADABA HAKIKA ZILIPENDWA

Nimerudi nyuma na kufikiri sana na kila nikiangalia picha hii hapo ndio nionapo kweli watu tumetoka mbali Mwaka 1992 Wilima (Matetere) Madaba.
NAWATAKIENI WOTE JUMAMOSI NJEMA SANA...BINAFSI NAENDA KULIMA KABUSTANI KANGU .

15 comments:

ray njau said...

Mtoto ni mtoto kwa mama hakui,ni mtoto tu,mtoto ni mtoto hata awe kama Yasinta,ni mtoto tu.
Yasinta,libarikiwe titi ulilonyonya na mikono salama iliyokulea na kukuza salama na sasa ni mama wa familia katika ardhi ya waswedi.
------------------------------------
Mfunze mtoto namna ya kuishi vizuri, naye hatasahau njia hiyo hata uzeeni._Methali 22:6
----------------------------------

ngaizaskids said...

Mkanda wa kipepeo naukumbuka nilikuwa namuibia mamangu. Du 92 nilikuwa chekechea chini ya mti mh! Jmosi njema mamii

Ester Ulaya said...

huo mkanda jamani, ujue nimenunua wa kipepeo juzi, zilipendwa zinarudi upyaaa, 92 nilikua la nne, na nilipoteza babu yangu mwaka huo na ndo aliniandikisha shule kijijini kwetu, duh umenikumbusha mbaliiiiiiiiii, uwe na jumamosi njema mamie

Mtani said...

Reflections ...

Nikiona picha hii inanikumbusha mitaa ya Mahenge mpaka Kanisa la Biblia, ninamkumbuka Mchungaji wangu na Familia yake; ninaiona sura ya Marehemu Baba Askofu Komba (RIP); ninaiona sura Baba Askofu Mtega zama hizo akiwa Rector wa Peramiho Major Seminary, ninakumbuka vitu vingi sana!

Nikiona picha hii ninakumbuka Vilima vya Matongoro na Ruhira Seko, ninamuona kijana wa Box 2 akiwa ametoka mkanda nje akiwa amepulizia "utuli" perfume ya YOU (sijui bado zipo?) anawaka waka na mafuta ya Shanti, vumbi laini la Songea halina huruma nimemvaa vizuri miguuni!

Nikiona picha hii nakumbuka TAMSALA ninaiona sura ya ukali ya Mwalimu Pyuza, lakini alikuwa na nia njema kwa mabinti wale, maana kama asingekuwa mkali wengi wao wangemezwa na mamba!

Nikiona picha hii ninamkumbuka yule Mzee aliyeishi na Kadala wakati Kadala akisoma secretarial course. Ni mzee huyu huyu ndiye aliyemtafutia kazi iliyompeleka Wilima Sekondari. Ni mzee huyu huyu alifanya hata wengine tumfahamu Kadala.

Nikiona picha hii ninakumbuka post moja ya Kadala akielezea namna alivyoishi na familia ya Mzee huyo. Ninaona picha ya Mzee aliyekaa kwenye kiti akipata "togwa la kisasa?" au sijui "ugimbi wa kisasa?". Mungu ambariki sana huyu Mzee, maana bila yeye labda Kapyula angekuwa alipita njia nyingine na may be tungekutana nae katika mazingira tofauti na kwa njia tofauti.

Lakini yote ni maisha ... it feels good to refelct back; it gives you strength to remain focused!

Hongera rafiki mwema Kadala!

EDNA said...

Nawe pia,na mimi nimeanza kupanda bustanini kwangu,ngoja viote nitakurushia picha.

John Mwaipopo said...

Naam picha na muziki hukumbusha watu mambo ya kale kwa haraka sana. Ni vema picha hii uliiscan na kuitinza. Hakika ya kale dhahabu, dada mkuu.

Mtani said...

Dada Mkuu ... hili neno sijalisikia miaka mingi sana, mpaka nilishasahau kama bado lina exist. Asante Bwama Mwaipopo kunikumbusha!

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! ntafikisha ujumbe kwa wahusika. Ahsante sana....

ngaizaskids! kumbe wewe ni kamwizi.LOL huu nmkanda niliupenda sana ...

Ester! Pole kwa kukukumbusha huu mwaka ila nami nimekumbuka kweli huu mwaka tupo pamoja ndugu wangu.

Mtani! Ama kweli wewe ni mtani. Maana unaonekana unanifahamu kwelikweli duh! nimesoma na kuona kama vile tuliishi kijiji kimoja au tumewahi kuonana.kKusema kweli kama kweli hunifahamu basi itakuwa umenisoma kwelikweli...Sina la zaidi isipokuwa nasama AHSANTE SANA.
Edna! Ahsante...Bustani leo yaani mpaka muda huu nipo hoi na kamgongo kanauima si unajua tena uzee:-)
kaka John! ni kweli picha na mziki ni vitu muhimu sana kuhusu kumbukumbu..nasikitika sina picha ambayo nilikuwa kachiki kabisa...hiyo picha ningeipenda sana. Nimefanya kama ulivyosema naitunza sana hii picha..kama vile ulijua nilishakuwa dada mkuu nilipokuwa shule ya msingi...

Mtani! Kusahai neno kama hili kweli? Dada mkuu/kaka mkuu kilanja au sijui Kiranja...mambo ya shule bwana raha kweli:-)

Mija Shija Sayi said...

Mkanda umezua kumbukumbu... Mwaka 92, nilishaondoka Nganza sekondari... "Ester ulikuwa la nne???.. mamaaaaa!! Binafsi sikumbuki kama nimeshakuwa nao mkanda huu au nilikuwa naazima kwa wanafunzi wengine pale Nganza, ila ninachojua nimeshawahi kuuvaa mara nyingi tu...

Asante kwa kumbukumbu Dada Mkuu.

NN Mhango said...

Da Yacinta,
Hata kama hakukuwa na internet au maendeleo ya tekelinalokujia, those were golden days everybody misses badly. Si mara yangu ya kwanza kuona picha hii ambayo is of course iconic for you. Have a spiffy weekend.

Ester Ulaya said...

hahahahaah Da'Mija Nganzaa oyeeee, tulikuwa tunaishi Mwanza South Mwanza, nakumbuka nilendaga kusalimia ilikuwa Likizo, ndo tukakutana na masahiba hayo, kweli hii imezua kumbu kumbu duh

Rachel siwa Isaac said...

Nawe dada Kadala ulikuwa wamo kwenye Mitindo,Duuhh makanda wa kipepeo!!hahahahahaanachni hizo si Chipsi?/viatu vilikuwa moto kweli!!

ray njau said...

Ama kweli maisha ni safari ndefu na mwisho wake ni kifo!!

ray njau said...

Hii picha ya Yasinta binti Ngonyani ina raha zake na mwenye kujua raha ni lazima aipende.

Kabinti ni karembo kwa uasilia kutoka Ruhuwiko katika ardhi ya wandendeule na kaumbile kaduuuuuuuuuuuchu kalikohanikizwa na wembamba maridhawa.

Mavazi ya kawaida tu lakini kamependeza kwa mkanda kipepeo na sukuna viatu kutukumbushia maisha na mafanikio safari yake ni ndefu na kilomita zake kamwe hazina idadi.

Je mwanaume yeyote mwenye ufahamu wa mapendo ya kwetu Afrika ruksa kutangaza nia au kuangalia tu na kuondoka?

Yasinta Ngonyani said...

Mija, Mwal. Mhango, Ester,Rachel na Ray ..Ahsanteni sana kwa yote. Na karibuni sana na sana..Picha ni kumbukumbu nzuri sana na hasa picha za zamani ..nimefurahi hapo juu Rachel amesema hivyo viatu vilikuwa vikiitwa Chips..mimi nakumbuka jina jingine kama kaka Ray alivyosema Sukuna. Ni kweli vilikuwa vinatingisha...