Friday, May 4, 2012

CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA PICHA YA WIKI :- JE? HUU NI UBUNIFU AU?

Nimetumiwa picha hii na msomaji wa Maisha na Mafanikio kwanza nikashikwa na butwaa, na pili nikajiuliza ni ubunifu? Na tatu nikajiuliza kukosa mtu wa kumtunza mtoto au chekechea? Nawaachia mwenzangu tusaidiana kujadili hapa...Duh! ila sidhali kama mtoto huyo anapata raha hapo.....MCHANA MWEMA MAJEMANI!!!

17 comments:

ray njau said...

Hapa hakuna ubunifu bli ukatili kwa watoto.

ray njau said...

HUU NI UKATILI MKUBWA SANA HUYU MTOTO.

Anonymous said...

Mwenye huyu mtoto anastahili kushitakiwa kwa ukatili wa watoto. Wanaharkati mpo!!!!!!!!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray na usiye na jina nakubalina nanyi ni UKATILI wa hali ya juu mno..Kama watu hawawapendi watoto kwa nini wanatafuta watoto? Ukiangalia kwa makini utaona katika sura ya huyo mtoto kuna machozi analia maskini malaika wa watu..Nashindwa kufikiria jinsi atakavyopata mikwaruzo hapo:-(

John Mwaipopo said...

kwani mtoto anabebwa mgongoni kwa kuwa ni mgongo wa mwanadamu au kwa kuwa anaweza kutulia? kama mti umefanya kazi ile ile ya mwanadamu, basi huu ni ubunifu uliotukuka.

ray njau said...

Yasinta ukiwa wewe ni mama nafahamu kuwa umepata hisia kamili za maumivu yanayompata huyo mtoto.Hakuna sentensi wala fungu la maneno la kuelezea ukatili huo unaompata huyo mtoto kwa kuwa yeye muathirika katika matatizo yaliyosababishwa na wengine.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka John! mtoto abebwapo na mama/au na binadamu kubwa hapo ni ule ukaribu au mnuso kujua huyo mama, baba , dada au kaka ila kujua kutofautisha na kupata ukaribu pia joto.

Kaka Ray! kama vile uliingia rohoni mwangu na kuona jinsi maumivu yalivyo ila basi tu..

DOROTHY MARTIN NDUNGURU said...

kiujumla huu si ubunifu wenye manufaa, na tukiliangalia hili swala kwa undani, huyu mtoto ana reflect maisha halisi ya wanawake WAZAZI wa kijijini... wanakuwa na majukum mengi na kwa wakati mwingine wengi wao hukosa wasaidizi wa kuwalelea watoto wao wakati wakiwa kwenye shughuli zao za kila siku. inawezekana kabisa mama hapo yupo anaendelea na kazi ambayo kuifanya akiwa na mtoto mgongoni, ni kama hatofanya vizuri na pili kumweka chini atambae...labda ni mtundu sana anajua atamsumbua kumtafuta au hata anaweza kutambaa akaokota chochote na kula... kwa upande ule mwingine, mama huyu kwa kufanya hivyo pamoja na sababu zake nzuri za kumweka hapo alipomweka, amesahau kuwa mtoto huyu anamtesa. mti ni mgumu, tofauti na mwili wa binadamu, PIA vipi usalama wake? ikitokea mdudu tofauti na nyoka akamng'ata? (wanadai nyoka hang'ati watoto) na vipi hiyo mbeleko ikilegea ama kwa juhudi za mtoto kujinasua ama kwa bahati mbaya, akateleza akaanguka....itakuwaje? SIO WAZO ZURI SANA, NA KAMA NI UBUNIFU, BASI SIO UBUNIFU WA MANUFAA KWANI UNA HASARA NYINGI KULIKO FAIDA...

emu-three said...

Hapana huko ni kukiukahaki za mtoto,hata kama....

sam mbogo said...

Hakuna anaye juwa sababu iliyo mfanya huyo mtu,mama/baba kumweka mtoto kwenye mti. mimi namsifu mtu huyo kwa kujuwa umuhimu wa mtoto na usalama wake. mateso au maumivu ya kuwa mgongoni kwenye mti ni mtoto anaye juwa. swali kwanini mtoto huwa analia akiwekwa mgongoni? mnacho kizungumza nima tokeo ya hisia kuwa mtoto anateseka kwakuwa yuko kwenye mti,lakini huwezi juwa nikwa kiasi gani mama/baba huyu ameokoa mengi katika kuamua kwake kufanya hivyo. kaka s.

Mija Shija Sayi said...

Ni kweli kabisa hakuna ajuaye aliyemweka alikuwa katika hali gani..

Doroth Ndunguru na Kaka S yaani kama mlikuwa mawazoni mwangu..

Mija Shija Sayi said...

Doroth Ndunguru wapi blogu yako sasa? tunahamu nayo..

Stay blessed.

chib said...

Unyanyasaji kwa watoto

Anonymous said...

ILA HAPO NINAWASIWASI NA ZILE NAZI ZINAZODONDOKA ZENYEWE NDO ITAKUWA HATARI ZAIDI

Anonymous said...

nivile tu watoto hawjiwezi kujitetea lakini chungu huiona ya unyanasaji ikubukwe kuna wazazi HATARI KWA WATOTO.Wanachofanyiwawatoto angalia mama anfanya nngono na mtoto mdogo anaangalia,anafunikwa kwa tenga ili asitembee yaani asizurure.wale wa mashambani huwachimbia chini wengine huwapa hadi pombe ili mtoto alale wao wafanye mambo yao.

Anonymous said...

jamani binadamu tuache ukatili kama mtu hampendi huyo mtoto apeleke hata kanisani watalea ni ktendo kibovu kabisa tutampata wapi huyo tumfunge

cytotec said...

obat telat bulan i think your blog very informative obat penggugur thanks for sharing obat cytotec