Tuesday, May 1, 2012

BADO NIPO! NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA JUMATATU YANGU MDADA MIMI!!!


 HAPA NI JANA JUMATATU KATIKA KANYUMBA KADOGO KA JOTO(SUMMER HOUSE)
Maji yanaonekana swali lakini baridi kivumbi kwa hiyo......
....nilishindwa kuogelea wala. Jumatatu iliisha vizuri namshukuru Mungu na natumaini nanyi pia mlikuwa na Jumatatu njema.PAMOJA DAIMA NA WOTE MNAPENDWA SANA. 

9 comments:

EDNA said...

Umependezaaaaaa!

batamwa said...

asante kwa dua zako za jumatatu ila picha ya chini kabisa umekuwa kabinti kadogo sana na umependeza sana uwe na mchana mwema!!!

Anonymous said...

Yasinta mimi nazimikiaga rasta zako tu. Wallah tena ungekuwa mke wangu au girl friend wangu ningekuwa nahakikisha rasta full time kwa gharama yoyote.

Pamoja na hayo, hata pic zako ambazo huna rasta bado waonekana mrembo, japo ukiweka rasta ndo unakuwa mrembo zaidi. Keep It Up mtoto wa Kingoni!

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante Edna!

batamwa! umenichekesha kweli eti nipo kama kabinti..haya ila kwangu zaote ni sifa tu...ahsante kwa yote.

Usiye na jina! ningependa kweli kujua jina lako:-) Ahsante kwa mtazamo wako:

Anonymous said...

Yasinta unajua umenipa mtihani mgumu sana wa kusema jina langu, na unajua kwamba siwezi kukataa, ila naomba uniruhusu nisiliweke hapa.

Kama kuna njia yoyote nyingine ya kukuambia hilo jina nitaitumia. Ila usije ukahisi kwamba mimi ni mtu ambaye unanifahamu; ukweli ni kwamba mimi ni mteja wako wa kudumu kwenye blogs zako ambazo huwa zinanipa kumbukumbu nzuri za Songea hasa ile blog ya Vangoni.

NB: Kule VANGONI usiwe unatumia kingoni kigumu wengine sio wangoni japo tunaipenda Songea kwa sababu tumepitia huko kimaisha na tusingependa historia hiyo ifutike kwenye maisha yetu.

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu wa mimi usiye na jina ..mmmhhh, Mtihani? Nafurahi kama unapenda VANGONI blog kingoni hiki niandikacho mie ni rahisi mbona?

Phocus Lukanazya said...

NAAMINI MAPUMZIKO YA JANA (MEI MOSI) YALIKUWA MAZURI KWAKO PAMOJA NA UWAPENDAO HIVYO BASI, NAMI PIA NAKUTAKIA JIONI NJEMA YA MWISHO WA SIKU YA LEO (JUMATANO)

ASANTE KWA TIPS ZAKO NZURI NA ZENYE MAFUNZO KWA JAMII YETU.
PAMOJA SANA...........

Mija Shija Sayi said...

Yasinta umetoka CHICHA ni balaaa..
unazidi kuwa mwali tu yaani..

Siku njema mama C.

Anonymous said...

Umependezaajee, mwaa!