Thursday, May 3, 2012

IMETOKEA TU KWAMBA NAPENDA SANA MAMBO YA ASILI KAMA UTAMADUNI HUU!!


 Katika ukuaji wangu nimekuwa nikipenda sana kuva urembo uliotengenezwa kiasili  NAPENDA MNO juzi juzi tu tamaduni yangu ya mkononi imekatika nimelia kweli :-(....

....ni hapa chini kulia ila hicho kidani/cha shingoni bado ninacho...ila nitajitahidi kutengeneza au kutafuta mpya:-)

8 comments:

Mija Shija Sayi said...

Nimelipenda hilo jina la Tamaduni yangu....(imekatika) Hongera sana Yasinta kwa kupenda vitu vya nyumbani ndo kuuenzi uafrika.

Uwe na siku njema.

ISSACK CHE JIAH said...

jANA ULISEMA HATUJUWI KISWAHULI LEO UNARUDIA TAMADUNI KWANI WEWE UMEGEUKA KUWA MUHA MTU WA KIGOMA? HAO NDIYO HAWAJUWI KISWAHILI JAPO NI WATANGANYIKA HALISI WEWE NI YULE WA KUSINI MWA AFRIKA YAANI MZULU JE UPO TAYARI TUFUATILIE URAIA WAKO KISA HUJUWI KISWAHILI SEMA UTAMADUNI WETU
CHE JIAH

Yasinta Ngonyani said...

Mija na kaka Che Jiah nisemapo Tamaduni nilikuwa nikimaanisha BANGILI. Na nyia bwana. Kiswahili sanifu U-tamaduni ni:- mila, saili, jadi na desturi za kundi la jamii fulani . je mpo nami hapa?

ray njau said...

Jasiri na asili yake!!!!!!

Ester Ulaya said...

KWAKWELI VITU VYA NYUMBANI VINA UZITO SANA, TUNA HAKI YA KUJIDAI NAVYO, HONGERA SANA KUJIVINIA NA VYA KWETU

Mtani said...

Mambo ya mila na utamaduni hayo.

Swali la kizushi kwa wataalam wa kiswahili na mambo ya utamaduni:

Yasinta amesema kwamba hicho kinachovaliwa mkononi kinaitwa "tamaduni", kinachovaliwa shingoni amekiita "kidani", lakini vyote vimetengenezwa kwa shanga ambazo zikivaliwa kiunoni zinaitwa shanga a.k.a "chachandu". Swali: kwanini hivyo vyote visiitwe shanga? Mfano: shanga ya mkononi au shanga za kiunoni au shanga za shingoni?

Siku hizi watu wanavaa chain "mikufu" shingoni, mikononi, kiunoni na miguuni, lakini zote hizo zinaitwa chain "cheni" with some ufafanuzi, mfano "cheni ya mguuni" au maarufu kama "kikuku".

Yasinta Ngonyani said...

Ray! umenena!
Ester! Ahsante Pamoja daima!
Mtani! nimekuelewa labda nimetumia kiswahili kigumu kidogo ningeweza kusema kama ulivyosema au pia bangili ya shanga au shanga ya mkononi na shanga ya shingoni au kidani cha shanga ya shingoni lakini inarudi paleple ni U-tamaduni si kama "mikufu ya dhahabu"...

ray njau said...

Wadau wa Kiswahili ni muhimu kwetu tukubaliane kuwa tunazingatia usanifu wa lugha pale tunapowasilisha taarifa rasmi.Lakini katika mazungumzo ya kawaida tunatumia Kiswahili mazungumzo na usanifu wa lugha hauzingatiwi.
-------------------------------
Ray Ephraim Ndewingiya Njau
Mdau na mtetezi wa Lugha ya Kiswahili
Dar es salaam,Tanzania.
Barua pepe:raynjau@gmail.com