Tuesday, May 22, 2012

TUIMALIZE SIKU/JIONI HII NA MWIMBO HUU:- MWANAMKE HAPIGWI!!


Binafsi leo nipo napumzika, ila ndo nini vijishughuli kibao.  Na wakati najipumzisha na hivyo vishughuli nikaona nisikilize kidogo mziki.Katika kusikiliza nikafika hapa, hakika nakuambia mpaka nimelia...NIMEGUSWA  sana  kuona/kusikia  hii. Mara nyingi inakuwa kweli kabisa ...kazi kwelikweli. JIONI NJEMA MUNGU AKIPENDA TUTAONANA KESHO.

15 comments:

Unknown said...

Ni siku nyingi sijapita hapa. Leo imebidi kwa kweli.

Jioni njema na kwako Dada Yasinta.

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kaka Yusuph! nafurahi upo mzima. Jioni njema nawe pia..Na karibu tena sana sana!!

Mija Shija Sayi said...

Mapumziko mema mama C, hivi kumbe tuko wengi tusioishiwa na vishughuli siku za mapumziko...

Asante kwa ujumbe...Mwanamke apigwi,

Mtani umepata ujumbe?

Yasinta Ngonyani said...

Mija/mama M! yaani we acha tu hata hamu ya kupumzika sina nipo hoi mpaka nimetafuta mkongojo...Nakwambia Mwanamke apigwi sijui nimesikiliza mara ngapi na kila nikizikiliza nasikia uchungu kweli hasa hako kakijana kanavyomkana huyo binti nusu niingia kwenye kompyuta na kumzaba kofi...Kweli wanawake wavulivu..

John Mwaipopo said...

kwa nini wanawake hupigwa?

ila kunja njemba zinadundwa kichizi na waifu zao. the good thing hazingung'uniki mitaani. sijui sinaona aibu.

je ni sawa mwanaume kupigwa?

Mtani said...

@Da Mija ujumbe umefika ingawa sijasikiliza wimbo ... watani zangu wa ukanda wa Pwani husema kwamba Mwanamke hapigwi makofi wala bakora, bali hupigwa kwa upande wa khanga!

Mke ni pambo la nyumba, "akikuboa" nenda Kariakoo tafuta khanga nzuri yenye ujumbe murua unaoendana na kile kilichokuboa. Yeye mwenyewe utaona anarudi mstarini.

Ili mradi isije ikawa zile msg zinaoashiria shari, mfano, "mtaa wa pili mtanikoma" au "Ala kumbe!" na nyingine.

Swali la kizushi kwa akina dada: kuna perception kwamba khanga zenye rangi na maua mazuri huwa zina msg chafu/mbaya na zile ambazo zina maneno mazuri huwa hazivutii. Kuna sababu yoyote?

ray njau said...

Nyumba hujengwa kwa mawe na matofali lakini unyumba[ndoa] hujengwa/hudumishwa kwa UPENDO pekee yake.
-----------------------------------
Enyi waume, endeleeni kukaa nao vivyo hivyo kulingana na ujuzi, mkiwapa heshima kama chombo dhaifu zaidi, yaani, mwanamke, kwa kuwa ninyi pia ni warithi pamoja nao wa pendeleo lisilostahiliwa la uzima, kusudi sala zenu zisizuiwe._1Petro 3:7
=================================

ray njau said...

Angalizo:
------------
Dhana inayotuzunguka ni ile kuendelea kuwabebesha lawama wanaume kuwa ndiyo chanzo kikuu za changamoto ndani ya maisha ya ndoa na familia.Lakini inasahaulika kuwa ni jukumu la mke na mume kufahamu uhuru na majukumu yake katika mpango wa ndoa.Uhuru wa mmoja huishia pale wa mwingine unapoanzia na kila mmoja ana wajibu wa kuwekeza katika kujenga na kudumusha mpango wa ndoa na hapa kunyoosheana vidole siyo suluhisho.Inasikitisha kuona kuwa utandawazi na teknohama vimebadili mazingira yetu katika maisha ya familia na sasa wanawake wanapaza sauti za kunyimwa uhuru na haki bila ya kuthibitisha iwapo kwa ukamili wametimiza wajibu wao katika ndoa kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mpango wa Mungu katika ndoa na siyo dhana na mifumo ya kibinadamu.

Yasinta Ngonyani said...

Kupiga/kupigwa kwangu hainipi maana kwanini kumtesa, kumpiga mwenzako, kwanini msiongee na yakaisha. Hapa Si kwamba ni wanaume wote wanaweza/wapigaji hapana. Au sio wanaume wote wanawapa wanawake mimba na kuwakana hapana. Nimeshawahi kushuhudia mwanamume analea mimba ambayo si yake na kutunza mtoto si wake..kwa hiyo kuna wanaume ambao hawapigi..Jambo kubwa katika ndoa ni mawasilino/kuongea/kujadili kwa pamoja hapo utaona UTAMU WA NDOA.

ray njau said...

Wawili ni afadhali kuliko mmoja, kwa maana wana thawabu nzuri kwa ajili ya kazi yao ngumu.Kwa maana mmoja wao akianguka, yule mwingine anaweza kumwinua mwenzake. Lakini itakuwaje kwa yule aliye peke yake akianguka wakati ambapo hakuna mwingine wa kumwinua?
Tena, wawili wakilala pamoja, watapata joto;lakini aliye peke yake anawezaje kupata joto? Na mtu akiweza kumshinda nguvu mmoja aliye peke yake, wawili wakiwa pamoja wataweza kusimama dhidi yake. Nayo kamba yenye nyuzi tatu haiwezi kukatika upesi. _Mhubiri 4:9-12

Yasinta Ngonyani said...

Hakika kaka Ray! hii sura ya Mhubiri imemaliza yote....Lakini je wengi wanajua hili?

ray njau said...

@Yasinta;
Acha ukapulya wako.
Wajerumani walipokuja walianzisha mfumo wa elimu ambao ulipewa jina la shule na waingereza wakaita skuli.Sasa watu wakifahamu wenyewe bila kufundishwa hiyo programu ya shule haitakuwa na umuhimu tena.Tuendelee kujifunza na kufundishana bila nukta.
Lakini je wengi wanajua hili?
Yasinta;wewe unajua mangapi wakati elimu ni bahari.Kumbuka kila mtu ni mahari katika wake tu na si katika uga wa watu wengine.
----------------------------------
Chuma hunolewa kwa chuma. Ndivyo mtu anavyounoa uso wa mwingine._Methali 27:17
-----------------------------------

ray njau said...

"Kila mtu ni mahiri katika uga wake mwenyewe na si katika uga wa mwenzake"

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray hapa nilikuwa namaanisha ningependa wengi wangesoma hicho ulichoandika hapo juu Mhubiri 4:9-12

ray njau said...

@Wadau wote;
Asanteni na karibu nyote katika usomaji biblia.Soma na uje na madokezo muhimu kwa ajili ya kuendeleza mada yetu.
Mhubiri sura 4.Mistari tunayozingatia hapa ni 9 hadi 12.
KARIBU NYOTE!!