Monday, May 14, 2012

JUMATATU HII AU WIKI HII TUANZE NA:- DONGI DONGI EMBE!!!

Leo nimeona tuelekee Mbamba bay kula embe. Je mpo nami au? Yaani hapa nimetamani kweli hizi embe  ....Haya nawatakieni mwanzo wa juma mwema na  DONGI DONGI JE UNAKUMBUKA MCHEZO HUU UJIPATA KITU BASI NDIYO NDONGI DONGI!!!!

5 comments:

Ester Ulaya said...

embe lina utamu wake jamani, sijui hata nielezeaje, nendeni Tabora, kila ukigusa mti ni mwembe, dodo, bolibo,embe kimavi, embe sindano n.k

sam mbogo said...

Weeeee! Ester kuna embe kimavi? do misijawahi sikia.safari hii nikienda nitaulizia hiyo embe kinyes/mavi kiboko,huko kwenye embe hizo nimoja ya mitaa ya nyumbani kiasili. haya asante kwa majina ya embe. kaka s.

Yasinta Ngonyani said...

Ester! Duh! Kaaazi kwelikweli embe kimavi? hii sijawahi kuisikia nami naahidi nitakapoenda nitaifafuta hiyo embe.

ngaizaskids said...

Napenda harufu ya embe sindano nimemiss kwa bibi yangu ghafla make maembe tulikiwa tunayarushiana kama mpira. Da Ester Hilo embe kimavi likoje sidhani km Bukoba yapo au ndo Yale ya kawaida?

Vitus Matembo said...

KWETU NYASA HAYO MAEMBE KIMAVI MBONA YAPO ILA NIMEBATIZA MIMI YALE MAEMBE NUNGA!!!!