Wednesday, May 30, 2012

UNATAKA KUMUACHA MKE MKOROFI? FANYA HIVI.........!


Ni ile JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO NA LEO NIMEIKUTA HII KWA KAKA YANGU WA HIARI KALUSE Hebu soma na halafu tujadili kwa pamoja.KARIBU...



Kuna wanaume ambao wametokea kuoa wanawake ambao wana tabia mbaya . ninaposema kuwa na tabia mbaya sina maana ya mwanamke kuwa Malaya, maana hiyo ni fasili rahisi ya tabia mbaya kwa watu walio wengi. Ninaposema tabia mbaya nina maana kwenda kinyume na matarajio ya mume na pengine hata kwenda kinyume na matarajio ya jamii. Mwanamke ambaye ana tabia kama ghubu, mdomo mdomo (mkosoaji), mtapanyaji wa mali, mpenda makuu na tabia nyingine za aina hiyo, ni mwanamke ambaye kwa kiasi kikubwa anaweza kumsababishia mume matatizo ya kimwili na kisaikolojia. Mwanamke wa aina hii anaweza hata kuathiri makuzi ya watoto na kuathiri uhusiano na mume na watu wengine waliyo karibu yake. Kama mwanamke wa aina hii ameolewa na mume mweledi ndoa inaweza isiyumbe sana, lakini hii ina mipaka na kiwango chake.

Kuna wakati matatizo haya huweza kufika mbali zaidi kiasi kwamba huanza kumwathiri mume. Mwanaume ambaye huchukua kila uamuzi unaohusu maisha yake kwa hadhari kubwa, anaweza kuendelea kuishi na mke huyu. Lakini mara nyingi kuendelea kuishi na mke huyu kuna maana ya matatizo zaidi kuliko ufumbuzi. Bila shaka mmeshawahi kusikia wanaume ambao wanalalamika kuhusu tabia mbaya za wake zao (hata hapa JF wapo wengi sana), lakini huku wakiendelea bado kuwa na wake hao. Ukiacha sababu ya kugawana mali, wanaume wengi huwa wanafikiria mambo mengi ambayo huwazuia kuchukua uamuzi wa kuachana na wake hao.

Nimeona itakuwa vizuri kuwaambia wanaume hawa kwamba, kama ndoa zao zimefikia mahali ambapo zinataka kuwatia kichaa, wakiwa na uhakika kwamba wake zao ndio wenye matatizo na sio wao, (hili inabidi waliangalie kwa makini) inabidi wafanye uamuzi kwa kujiangalia wao na watoto wao zaidi kuliko watu au vitu vingine. Baadhi ya mambo ya kuangalia ni haya:

1. Kuathirika kwao: wajiulize wanaumia kiasi gani kimwili na kisaikolojia kwa kuendelea kuishi kwao na wanwake hawa. Kama ni ghubu na kukosolewa, kunawaathiri kiasi gani,? Na kama ni utumiaji mbaya wa mali unawaathiri kwa kiasi gani? Kama athari za tabia mbaya alizo nazo mwanamke zinafaa kudharauliwa na mume anaweza kuzidharau ni vyema akafanya hivyo, na kuendelea na maisha. Na kama akiona kuzidharau tabia hizo itakuwa na maana ya angamio kwake na pengine mbaya zaidi kwa watoto, inabidi hiyo iwe ni sababu ya msingi kuachana na mke huyo.

2. Ndugu watasemaje: wanaume wengi hukwamia hapo. Kama wake zao wanaelewana vizuri na baadhi ya ndugu, au hata wazazi wao, wanaume hushindwa kutoa maamuzi wa kuwaacha kwa hofu ya kulaumiwa na kushangawa. Wakati mwingine mume huyu anaelewena sana na watu wa upande wa pili, yaani ndugu wa mke na hasa wazazi na pengine wote. Hiki nacho ni kikwazo kikbwa sana, kwani mume hufikiria jinsi atakavyoonekana kwa watu hawa, pale atakapoamua kuchukua uamuzi wa kumuacha mkewe.

3. Sifa moja nzuri: pamoja na kuwa na matatizo, kila binadamu anaweza kuwa na upande mzuri. Kama mwanamke huyu ana sifa fulani ambayo ni nzuri sana, tuseme ni mpishi hodari sana na mkarinu kwa wageni , au labda ni mwaminifu sana katika ndoa, mwanaume anaweza kukwama kutoa uamuzi kwa kudhani au kujidanganya kwamba huenda anaweza asipate mwanamke mwingine mwenye sifa kama hizo. Huku ni kujidanganya kwa sababu kila sifa aliyo nayo binadamu fulani, ya kitabia, ipo kwa binadamu mwingine hata kama siyo wengi.

Ukweli ni kwamba mwanaume anaweza kushindwa kumpa talaka mkewe ambaye anakaribia kumuuwa kwa matatizo yake kwa sababu ambazo mtu mwingine anaweza kuzishangaa. Lakini jambo la msingi kwa mwanaume kama huyu ni kujaribu kupima kwa makini, je hizo sababu zinazomfanya asite kuachana na mkewe huyu zina nguvu au maana kuliko maisha yake, hasa mwili na akili yake?.
Angalizo: Sishauri watu kuachana, lakini nashauri watu kujua kwamba ndoa zenye mashaka makubwa ni hatari kwa afya na maisha yao. 
TUKUTANE TENA PANAPO MAJALIWA..JUMATANO NJEMA.

5 comments:

nyahbingi worrior. said...

Sina maoni ila nimepita na kujisomea.

ray njau said...

Ni lazima wenzi wa ndoa wawe waaminifu kwa mmoja na mwenzake. Uzinzi ni dhambi dhidi ya Mungu na dhidi ya mwenzi wa mtu. (Waebrania 13:4) Mahusiano ya kingono nje ya ndoa ndio msingi pekee wa Kimaandiko kwa talaka inayoruhusu mtu aoe au aolewe tena. (Mathayo 19:6-9; Warumi 7:2, 3) Yehova huchukizwa wakati watu wanapotalikana bila misingi ya Kimaandiko na kuoa au kuolewa na mtu mwingine.—Malaki 2:14-16.

Yasinta Ngonyani said...

nyahbingi worrior...Ahsante kwa kupita na kusoma na pia umeshatoa maoni..
Ray ulichosema ni kweli na pia naongezea katika ndoa mawasiliano na uvumilivvu ni muhimu sana.

Mija Shija Sayi said...

Nami nimepita nakujisomea..

Asante kwa maarifa haya dada..

ray njau said...

@Umesema kweli Kadala.
Mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika ndoa na iwapo netiweki ikiwa chini unyumba unabomoka na hitimisho ni:"UKISEMA CHA NINI NA MWENZIO ANASEMA NITAKIPATA LINI?