Sunday, January 16, 2011

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI HII YA TATU YA MWAKA HUU KWA SALA HII!!!!

Mungu nakuomba unisaidie niwakumbuke wenye njaa ninapokuwa na chakula, wagonjwa nianpokuwa na afya nzuri, wote wanaoteseka kwa sababu ya vita ninapokuwa na amani, wasio na nyumba ninapokuwa nimelala na pia kuwa ndani ya nyumba yenye joto, pia nakuomba unisaidia niwakumbuke yatima kila ninapokuwa na wazazi wangu.

Na pia nakuomba:

Bikira Maria mama wa msaada na uibariki familia yangu, kaka zangu, dada zangu, wazazi wangu na watu wote dunia hii katika dhambi: AMINA

JUMAPILI/DOMINIKA NJEMA KWA WOTE JAMANI!!!!

14 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Amina!!!!


Imani pekee ndio itatufikisha mbinguni siku moja. Hata kabla ya kufika mbinguni, imani ndio itatupatia suluhisho ya matatizo yetu mengi (kama siyo yote) maishani mwetu.


Kumshukuru na kumwomba ya ziada Mungu ni lazima kwani kwa neema Yake tayari katuwezesha wote wasomaji wa POST hii ya Dada Yasinta kupunguza tena kwa mafanikio makubwa asilimia kubwa ya wakati wetu wa mwaka 2011 na badala ya 365 tayari tumebakia na 348 ya siku kabla tuanze tena ku hesabu baraka zetu.

Fadhy Mtanga said...

ahsante sana da Yasinta. Nami nakutakia Jumapili njema wewe na familia yako..

Ubarikiwe sana. Pia ahsante sana kwa kutochoka kupita pale kijiweni pangu.

Simon Kitururu said...

Nimechanganyikiwa tu katika ya MUNGU bikira MARIA alipoingizwa kwenye shughuli!

Jumapili njema Dada Yasinta!

Unknown said...

Amina. Mune na atujalie moyo wa shukrani kwa yale anayotujalia kila siku na tukumbuke kuwa hatustahili 'makombo ya mezani kwake'

EDNA said...

kwako pia Da YASINTA.

Mtesuka said...

Amina. Baraka zake Mungu mwenyezi ziwe nasi siku zote.

Jacob Malihoja said...

Nimeipenda sala hii, nasema AMINA. Lakini pia nimependa ulivyovaa .. sio tu umependeza..bali pia unawakilisha Uzalendo ulio ndani ya Moyo wako, nasema AMINA kwa hilo. Mungu akubariki sana, Mungu Atubariki sana Sote... Ubinadamu na Uzalendo Daima uwe ndani ya mioyo yetu!

malkiory said...

Angalia usijeshambuliwa kama pengo kwa salamu hizi za kikatoliki!

WA UKAE said...

plaese, naomba niichukue na hii picha kama ileee

Yasinta Ngonyani said...

Natumaini wote tulikuwa na jumapili yenye amani na upendo. Ingawa wengine tulikuwa kazini lakini ni moja ya maisha bila kazi hakuna kitu mezani. Ahsanteni sana wote kwa kutochoka kuchangia hapa kibarazani. Mwenyezi Mungu awe nanyi. karibuni tena na tena na tena.

Wa Ukae! sijakuelewa unaweza kufafanua?

Penina Simon said...

mh!! umependeza jama, kumbe rangi zetu nazo wamo

Medson Chengula said...

Mungu akubariki kwa sala nzuri kwani ni wachache ambao huwa wanakumbuka kuwatanguliza wezao wanapo kuwa kwenye mafanikio fulani. Mungu akubariki na abariki kazizako na familia yako. Akutimizie mahitaji yako. Amen.

Matha Malima said...

aiseee hii picha ulinoga sanaaaaaaaaaaaaa.kweli unaipenda Tanzania uluipenda nimeipenda

WA UKAE said...

Kuna ile picha yako niliyoitumia kwenye desktop yangu, nadhani unaikumbuka. kwa hii 2011 naomba unipe ridhaa ya kuitumia hii.