Thursday, January 20, 2011

PICHA YA WIKI: ALA ZETU

Picha hii imenifanya nimkumbeke baba mmoja kule Madaba alikuwa akitoka Madaba mpaka Songea na Zeze yake kwa mguu. Walikuwa wakimwita Perege alikuwa akipita kila kijiji na kupiga zeze yake. Baada ya kukumbuka hivi nikaona si mbaya kama ikiwa picha ya wiki. TUKUTANE TENA WAKATI MWINGINE:-)



Tanzanian traditional instruments Zeze from Martin Neil on Vimeo.

7 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Zeze? Au ngoma?


Haya basi, haina haja kuuliza; maana yake mlio huyu bwana kaisha pata!

Simon Kitururu said...

Picha Nzuri ! Ni nani kaipiga ?Ingekuwa vyema kweli kumjua maana nahisi anapicha zaidi mwanana.


DUh umenikumbusha mabali na stori za MADABA! Nakumbuka sana enzi za MADABA , LUKUMBULU ile ya zamani enzi kwenda Songea hakuna LAMI.

Aliko Mwakanjuki upo?

Upepo Mwanana said...

Safi sana ...zana za jadi hizo

Yasinta Ngonyani said...

Kaka GMP! ni zeze na ukiisikia utapenda.

Simon! akubali ni picha nzuri ndo maana nimeipenda aliyepiga picha simjui. Nafurahi kama umekumbuka za MADABA, LUKUMBULU NA SONGEA pia ila sasa kuna lami mpaka mujini:-)

Upepo Mwanana. Zana za jadi ni kweli zilikuwa bombi... karibu tena mwana kwetu.

Anonymous said...

HAKIKA PICHA NINZURI,LAKINI SINA HAKIKA KAMA WENGI WALIVYO SEMA,JINA LA KIFAA/CHOMBO HICHO.NADHANI KINAITWA NDONO,NASI ZEZE .
KAKA S

Goodman Manyanya Phiri said...

Haya, basi! Nimesikia jinsi Zeze inavyopigwa. Kazi unayofanya Dada Yasinta unaijua mwenyewe na Mungu wako, na ubarikiwe sana kwa jitihada zako za kumwendeleza Mwafrika na utamaduni wake!!!

Nyimbo kama hiyo ??SING FOR THE WELL pitia VIMEO?? hatusikiagi Barani mwetu lakini ni tamu kama nini!!!!

Lala salama na wasomaji wablogi yako wanaonifurahisha!

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Sidhani kama hii ni zeze. Wasukuma huiita ala hii Ndono. Zeze naifahamu sana na hata mimi mwenyewe ni fundi wa kuicheza. Nitajaribu kuitengeneza halafu ntawaonjesha!!!