---na hapa tayari mishkaki imeiva ..nimechoma kwenye oveni kwa vile huko nje bado kuna baridi na theruji nyingi sana ....
Na hapa mlo mzima ndivyo ulivyokuwa wali, njegere, salmon,cod na mchuzi ulioungwa kwa nazi jioni ya jana ilikwisha safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii sana...
Na baada ya kula chakula kilibaki basi Kapulya akapata kutengeneza la kwa ajili ya kula leo jumatatu awapo kazini.Huwa sipendi kununua chakula kazini---kama unavyona hapo ndo mlo umekamilika nitakula leo jioni niwapo kazini ...JUMATATU NJEMA KWA WOTE.
16 comments:
Dada kwa mtindo huu wa kutamanishana siku nyingine nitakudai unitumie kwenye e-mail as an attachment, ha ha ha ha ha. Inaonekana Jumapili ilikuwa nzuri sana, nimetamani kama ningekuwepo vile na mie "nipochoe". Wacha ninywe maji nishushie haya mate. teh teh teh teh!!
chakula kitamu umepika. hongera kwa kupata muda wa kufanya hivyo.kwa maana hiyo kilicho baki jana unakila leo kama KIPOLO??.haya kazi njema DA YASINTA. kaka s
Kumbe ni mpishi mzuri sana, sasa itabidi nikaribie kwako Yasinta, kwa chakula hicho hicho. Mh! nimekipenda sana ila ukiweza unipikie na chapati zakukanda. Siku njema.
Kaka yangu Mhagama wenga nywi tu maji ago kuhelelesa ..usipate shida karibu kipo kwa ajili yako pia
Kaka Sam Yaani kama ulikuwepo kilikuwa bongo la utamu..KIPOLO hahahaaaa kaaazi kwelikweli
Usiye na jina! Umenichekesha kweli kupika nilianza nikiwa na miaka mitano. Hakuna shida ww karibu sana na wala usikonde chapati utapata ..siku njema nawe pia ila ningefurahi kujua jina lako...kupata mgeni bila kujua jina kweli???
Yani asiye na jina huyu, ndiye huyohuyo uliyemuuliza jina kwenye ile habari ya wanawake wanao onewa ruhuwiko, sijapata mda wa kukupa jina langu ila utalijua tu.
Safi sana msosi unavutia
Mmmhhh tamu saana..Hongera kwa mapishi KADALA..
Oh! kumbe ni wewe usiye na jina ..haya ntafurahi sana kukufahamu....
Kaka Isaack! sio kuvutia tu ulikuwa mtamu sana pia:-)
KACHIK! YAANI SI UWONGO ULIKUWA MTAMU MNO ..AHSANTE kwa hongera...
Habari.
Hongera kwa kujali afya
Kila la kheri
mweh mweh.......mbona njaa imeumaaaaaa
Asante sana kwa mlo mzuri na yenye kuzingatia viwango na masharti ya tasnia ya mapishi.
Kaka Salehe! Afya ni muhimu katika maisha..ahsante kwa mchango wako.
Ester! nakuambia chakula kilikuwa kitamu si mchezo siku tukikutana ntakupikia kama hiki najua utakipenda...pole kwa kuwa na njaaaa baada ya kuona makulaji haya...
Kaka Ray...Mwanamke na mapichi si ndio:-)
Yasinta imebaki kuanzisha Restaurant tu...
Unasubiri nini?
Mija Mija Dada msaidizi...oh ni dada msaidizi kwa maana hiyo utakuja kunisaidia dada mkuu au sio?
Dah! umenitamanisha sana... Udendaaaaa
Shem Cathbert! karibu sana hapa kibarza cha maisha na mafanikio..na pole kwa kukutamanisha ila karibu ushiriki nasi:-)
Post a Comment