Tuesday, March 5, 2013

PICHA YA/ZA WIKI MAZOEZI NI MUHIMU KATIKA AFYA ZETU TUZINGATIE!!!!

 Mchaka mchaka chinja....aaah ebu tuchukue wimbo huu Idi amini akifa mimi siwezi kulia nitamtupa Kagera awe chakula cha mamba....
Dada mkuu msaidizi naye hayuko nyuma kabisa ..Haya dada mkuu msaidizi msimu wa kuanza mazoezi unakaribia ,,wewe endelea  usitazame nyuma ..haya alisema, alisema, alisema Nyerere alisema vijana wangu wote mwalegea sharti tuanze mchakamchaka....mmmmhhh ngoja niwaachie na wengine waanzishe kuimba maaana mapumzi hapa  yanasumbua kweli....Sijui mnawafahau wadada hawa?:-) JUMANNE IWE NJEMA SANA KWA KILA MMOJA!!!!!

10 comments:

Shalom said...

Jamani mazoezi na mawani haya hongereni wadada.

ray njau said...

Hongera kwenu mama na binti!!

Ester Ulaya said...

hehehehehe kama nawaona vileeeeee, safi sana nimeipenda hiyo jamani, mazoezi kwa afya

Yasinta Ngonyani said...

Shalom! kuna wengine ni lazima wawe na miwani wakati wote...Ahsante

Kaka Ray! Naona umepotea kabisa ..sasa hapa sijui nani ni mama na nani ni binti?

Yasinta Ngonyani said...

Oh! Ester yaani ni kweli kabisa mazoezi kwa afya..unakaribishwa kujiunga nasi...

ray njau said...

Sijapotea kabisa bali tu nimepepesa macho na kung'ata maneno.@Yasiii!!!

Mija Shija Sayi said...

Unajua ukiizoea sana miwani unasahau kama umevaa.

Nina swali, hivi ni kwa nini dunia ya sasa hivi inachukulia kufanya mazoezi ni kutafuta wembamba? na si kutafuta afya kwa ujumla?

Cathbert Kajuna said...

Hongera sana.... endelea kupasha ili mwaka ujao uje tushiriki mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2014

Yasinta Ngonyani said...

Mija! baridi inakweisha kwa hiyo mambo kama kawa na wengine wote...
Cathbert! karibu sana katika kibaraza hiki..Wala usikondo tutakuja katika haya mashindano au Mija wasemaje?--ila mie ntakuja...ngoja nianze kujipanga

ray njau said...

Dunia inahisi mazoezi ni kutafuta wembamba kutokana na mabadiliko katika mchakato wa maisha na mafanikio.Teknolojia inazidi kuwafanya watu wasitumie nishati nyingi katika miili na vyakula vinavyoinenepesha miili.Hapa sasa ili mambo yaende sawa suluhisho ni watu wanalazimika kubuni mazoezi kama hizi za Yasii& Mija mini marathon.