Friday, July 11, 2008

JULAI 11, 2008 NYOKA


Sijui kama wasomaji mtanielewa. Hawa nyoka anatunzwa ndani ya nyumba analishwa na kutunzwa kama mtu. Wakati ni adui mkubwa wa binadamu. Na pia ni nyoka aliwadanganya Adamu na Eva. Nyoka analala safi wakati kuna watu wengine hawana sehemu ya kulala. Wanateseka na njaa pia baridi. Ila bahati mbaya sijui jina lake je? mnaweza kunisaidia halafu wapo wawili hapo. Haya kazi kwenu.

5 comments:

Anonymous said...

Daima labda nahisi kuchanganyikiwa kuhusu haya mambo.Ilikuwaje nyoka akaweza kuongea na kuwadanganya hawa jamaa kule Eden?Aliongea lugha gani?Ilikuwaje huyu jamaa akafananishwa na shetani wakati yeye ni nyoka?Hivi shetani ni nini?Nyoka au?Mmm hata sielewi haya mambo yanakuwaje na yalikuwaje hapo hadi nyoka akaongea na kuwahadaa kwa majigambo yale...tusaidiane hapo labda...aaaah nimeanza mjadala mwingine.Ngoja nizame katika hoja kuu,Kuhusu kuwatunza wanyama au nyoka ni hulka ya jamii na utamaduni wake.Kimsingi hii naweza ni kutokana na utamaduni wa wazungu wengi,inawezekana wako sahihi lakini kwangu naona nyoka anapaswa kuishi maisha yake porini.Na ukiona wanatunza sijui niseme kuchanganyikiwa au vipi.Kifupi ni utamaduni wa jamii husika na hulka zao...nimejieleza vizuri au nimekosea

Anonymous said...

Ilikuwaje nyoka akaongea na akina adamu na eva?Tunasema ni uwezo wa mungu,sasa ilikuwaje hawa wa sasa wasiongee kama binadamu? au hata ng'ombe ambaye ni kitoweo asiongee kwa huruma pale anapoandaliwa kitoweo?Ilikuwaje chatu au nyoka akapata upendeleo huo?Kwanini alipewa wakati alikuwa mwovu?
jamani nyoka aliongeaje huyu.....nahisi uchizi mbona. tafakuri inatakiwa na falsafa juu yake

Yasinta Ngonyani said...

Haya nikuambia haya mambo ya nyoka kuwadanganya adam na eva ni fumbo ambalo sijui kama kuna mtu anaweza kufumbua ila kama mimi nilivyoelewa ni kwa sababu watu wengi wanajua nyoka ni hatari. au vipi

Geraldo Paratinga said...

This is an african language? I am brazilian. My grandfathers were rapted to job as slavers. So i love an land that i don't know her language, smell and voice.
Cogratulations for write at a not singular language.
From Brazil,
Geraldo Santana

Yasinta Ngonyani said...

muchas gracias! Geraldo Santana