Friday, February 22, 2013

IJUMAA YA MWISHO YA MWEZI HUU WA PILI TUIMALIZE NA UJUMBE HUU:- KILA BINADAMU ANA MAPUNGUFU YAKE!!!

Sisi binadamu tumeumbwa na mapungufu, Hakuna aliyekamilika kila mmoja ni tofauti na mwingine. Kuanzia kimawazo, kimatendo pia kitabia. Na kwa kuwa kama tulivyo, hii ndio maana tuna hitaji pale jambo linapopinda, tuchukue jukumu na kujaribu kuliweka sawa na pia KUSAMEHEANA. Ila KUMSAMEHE mtu si jambo dogo maana kama kweli unamsamehe mtu basi umsamehe KIDHATI/TOKA ROHONI. Au hata kumpa yule mtu aliyekosea/uliyepishana naye mawazo nafasi ya pili/ajaribu tena. Sababu yeye ni banadamu kama wewe, yule, mimi na wao. NACHOTAKA KUSEMA HAPA:- KAMA UMEHITILAFINA NA MTU JARIBU KUONGEA NAYE ILI KUSHULUHISHA NA UTAOANA MAISHA YANAKWENDA SAFI. KWANI KUKAA NA KITU MOYONI HAISAIDII KITU. Binafsi kama kuna kitu nimemkosea mtu/nimemdanganya mtu basi NASEMA SAMAHANI SANA, SANA, SANA, SANA....kwani hata mie ni binadamu na nina mapungufu.NA NINGEOMBA TUANZE UPYA/SECOND CHANCE. IJUMAA NJEMA!!

11 comments:

Rachel siwa Isaac said...

Asante KADALA kwa ujumbe mwema....

jee inakuwaje kama kunamtu amekukosea na umesikia kutoka kwa watu tuu..lakini ukamuita ili umsikilize na kusahihishana na akakataa jee huyu mtu ni wakumuweka fungu Gani?

Yasinta Ngonyani said...

Kachiki! mimi kama mimi basi nitamweka huyu mtu katika kundi la sio rafiki mwema na pia ni mkolofi/mnafiki. Maana akiwa nawe anakuwa mwema akiwa na wengine anakuteta...

Rachel siwa Isaac said...

Asante KADALA kwa Maoni yako!!!

Yasinta Ngonyani said...

KACHIKA AHSANTE NAWE PIA KWA SWALI NZURI NATUMAINI NA WASOMAJI WENGINE WATATUSAIDIA HAPA NI BONGE LA SWALI KWA KWELI...

Shalom said...

Yani mtu kama huyo unamsamehe moyoni mwako lkn unampotezea maana tayari ni adui mtu gani hapendi suluhisho isitoshe yy ndie anakuwa mgovi alafu ww wajishusha yy hataki mpotezee huyo.

Rachel siwa Isaac said...

Asante sana Shalom...da'kadala..Pamoja sana! !

Shalom said...

Poa mdada.

Anonymous said...

kweli hii mada imenigusa haswa kwa swali la Rachel siwa na mimi napitia ktk situation kama yake mimi nina mdogo wangu amekuwa mtu wa kinyongo sana mkikosana kidogo tu yeye hubeba rohoni hata kama unataka usulihisho yy hatakisaa nyingi utakuta ni kosa ni lake lakini hakubali kuwa amekukosea na mbaya zaidi hataki suluhu je ni mfanyeje ndugu yangu huyu wa damu moja?ananipa majaribu sana mimi sipendi ugomvi

Shalom said...

Huyo inabidi umuombee tu kwani ndungu wakati mwingine wanauzi sana alafu isitoshe yy ni mdogo alafu hataki suluhisho pole sana

sam mbogo said...

Safi sana wa dada wapendwa mnavyo jadilili hoja hii na kuwa wakweli kutoka katika nafsi zenu jinsi mnavyo jisikia kwa kila mmoja wenu ju ya ujumbe huu hapo juu. ni ngumu sana" kumpenda jirani yako kama unavyo jipenda wewe" kimsingi lazima ujitambue/ujijuwe wewe binafsi/wewe mwenyewe ninani? ukoje, unapenda nini, hutaki nini,? na kwa hali ya kawaida ya kibinaadam wengi wanajaribu kuwa wema na msaada mkubwa tu, kwa jamii ila kunapo tokea kutoelewana ndo utajuwa kipimo sahihi cha mtuhuyo atakavyo shughulikia tatizo hil. mara nyingi huwa tunatanguliza ubinafsi mbele kabla ya kujiuliza imekuwaje sam kunifanyia jambo hili,na ukini uliza naweza nikakosa jibu kwani tayari kwa upande wangu hujuwi nini kimenisibu.kwa hiyo nitahukumiwa bila kujuwa upande wapili nini tatizo.nahili maranyingi husababisha mtafaruku mkubwa miongoni mwetu na jamii kwa ujumla. kumalizia kwa mfano-kulikuwa na jamaa mmoja alikuwa na miadi na mwenake wakutane saa8 mwenzi wake akafika saa 9!? aliyekuwa anasubiri ,yule mchelewaji alipo fika alimpokea na kumwambia pole sana kaa na tuendele na kikao chetu.yule mtu wa pili aliye chelewa hakuamini alijuwa jamaa ange foka,na mkutano haungekuwepo.unafikiri kwa nini jamaa haku foka bali alimpokea na kumpa pole ya kuchelewa.? kaka s

Rachel siwa Isaac said...

Pole sana Mpendwa yanayokusibu na ndugu yako..MUNGU yu mwema na usikate tamaa ipo Siku....

Kaka S. Asante sana kwa Maoni yako..Huyu mtu Alitumia BUSARA/HEKIMA kwa Mtazamo wangu.