Saturday, May 1, 2010

WANASIASA WASIO NA HURUMA NA NIA YA KUSAIDIA WALEMAVU HAWAFAI KUCHAGULIWA

WATANZANIA wametakiwa kutowachagua wanasiasa wasioonyesha utashi wa wazi katika kuwasaidia na kuwatetea walemavu wa aina mbali mbali nchini.

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na ndugu Jacob Malihoja Mwezeshaji katika mafunzo ya siku nne juu ya Uongozi na Utawala Bora yaliyoandaliwa kwajili ya viongozi wa chama cha wasioona nchini Tanzania League of the Blind (TLB) Wilaya ya Temeke.

Ndugu Malihoja alitoa kauli hiyo kwa masikitiko baada ya wafanyabiashara, wanasiasa na viongozi kadhaa waliolikwa kwenye hafla ya kufunga mafunzo hayo ya wasioona kutotokea kwenye shughuli hiyo jambo ambalo liliwafanya Walemavu hao kujikuta wako peke yao kwa ufariji wa wajumbe wa Serikali ya Mtaa waliyejitokeza na kumua kumwakilisha Mgeni rasmi Mbunge wa jimbo la Temeke Mhe. Abasi Mtemvu ambaye alipata dharula ya kutembelea wananchi wake walioathirika na mafuriko.

Aidha ndugu Malihoja amesema Watanzania wanapaswa kuelewa kuwa sisi sote hatuoni, alitolea mfano Mhe. Mudhihiri alikuwa salama na viungo vyake vyote lakini alikuwa haoni, kwani laiti angekuwa anaona asingefanya safari ambayo ilisababisha na yeye sasa awe mmoja wa walemavu nchini.

Kwa kutambua hilo amesema Watanzania na wote tunawajibu wa msingi sana kuwasaidia walemavu kwani hakuna anayeona kesho atakuwaje.

Aidha amesema mbali na hilo walemavu wana akili na uwezo mkubwa sana katika kuchangia maendeleo yao wenyewe na maendeleo ya Taifa na kwamba kinachohitajika ni kuwawezesha washiriki maendeleo yao na maendeleo ya taifa kimamilifu kwama watu wengine..

Zaidi unaweza kusoma hapa.

3 comments:

chib said...

natumaini walaghai watasoma ujumbe huu na kugeuza dhamira zao mbaya

Jacob Malihoja said...

Kwakweli kuna haja kwa Serikali kuwa na sera maalumu ya Kutoa ruzuku kwa vyama vya walemavu. Ikiwa Serikali inatoa Ruzuku kwa vyama vya siasa na Asasi nyingine za Kijamii basi ifanye hivyo na kwa walemavu. Aidha tanzania ina matajiri wengi lakini sioni juhudi za kweli za matajiri hao kusaidia Walemavu, kuwajengea uwezo ili nao washiriki katika maendeleo ya nchi yetu. mimi nimejifunza Mengi sana katika Mafunzohaya ambayo nimeyaendesha kwa Wasioona kwa siku nne. Ndugu zetu hawa wana akili za ajabu tena wana upeo mkubwa kuliko watu wengi wenye kuona kawaida.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

@Malihoja: Hao wasioona Wanaona tusivooona siye wenye macho